Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Jamal Malinzi na TFF hii . mbona jambo hili umeliangalia na kulifumbia macho? tumeona jinsi ambavyo Yanga wamefanya vitendo hivyo kwenye mechi nyingi sana. ikiwepo hii ya juzi juzi kwenda kutoa maji ya golikipa jambo ambalo kikanuni si kosa golikipa kuwa na maji ya kunywa pemben as long as hayana madawa ya kuongeza nguvu. inakuaje kchezaji wa timu nyingine anaruhusiwa kuyaondoa maji hayo ? huoni kuwa hii ina athari kisaikolojia kwa yule ambaye maji yake yameondoloewa? tumeona jinsi ambavyo wachezaji katika karne hii wanaogopa taulo la EVo Mapunda. hili ni jambo la kijinga kabisa katika ulimwengu wa sasa. kama refarii naye anahusika kwenda kuondoa taulo langoni mwa kipa wa simba kwa imani za kishirikina na TFF Msikemee mambo haya hamwoni tutafika hatua timu X itaomba mechi yake isogezwe mbele kwa kuwa Mpiga ramli kasema kuwa siku hiyo iliyopangwa hawatashinda?
si tumeona timu ikitaka uwanja ubadilishwe kwa kuwa inalogwa? hamuoni hili jambo lina athari kwa timu ambazo zilikuwa tayari zimepanga bajeti yake zikijua kuwa zinaenda kucheza uwanja husika? Jamal Malinzi TFF kanuni zake zinasemaje au kanuni za FIFA au hata za CUF? haya ni mambo yanayoruhusiwa?
kama msipokemea mambo haya mi nasema tutafika hatua mbaya sana na ndo maana hata mpira wetu hautaweza kukua.