Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
hili linatokana na matamko ambayo Yanga mara kadhaa inatoa pale inapokosa ushindi. mara watasema walionewa na mwamuzi. mara watasema uwanja ulikuwa mbovu, mara watasema walilazwa hotel mbaya n.k. TFF mara nyingi imekuwa ikionekana kuwaogopa Yanga. hii mechi yao na maafande ilichezwa wiki moja iliyopita .tulitegemea mapema sana jambo lao kama lilikuwa hivyo walivyosema siku ile mara baada ya mechi wawasiliane na TFF. Je ina maana makamisaa hawakutoa report hiyo mpaka Yanga walipolalamika na kutoa vitisho? kama kuna makosa yalifanywa na wachezaji wa police yalipaswa kushughulikiwa mapema kabla malalamiko hayajatolewa. sasa hii itajenga hofu kwa marefarii wanaochezesha mechi za yanga kwa maana kama yanga isipofunga itaonekana hawakuchezesha vizuri na hivyo kutafutia sababu. hii itawajenga wachezaji wa Yanga kuwana kibri sana na kulazimisha ushindi, kila mara kumzonga mwamuzi kutaka matakwa yao yatimizwe na pia kuwafanya waamuzi wachezeshe mech za yanga kwa woga sana.
TFF msifanye maamuzi kwa pressure ingekuwa jambo la ajabu kwa yangakujitoa ligi. mbali na kucheza ligi yanga inafanya nini zaidi? ina michezo gani zaidi ya mpira wa miguu? hilo lilikuwa tishio la kijinga. kanuni zifatwe na si team hizi kubwa kuish kama zitakavyo.lakini pia team zote ziwe na nidhamu