Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa changamoto na mjadala unaoendelea kuhusu jezi rasmi za Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ hivi sasa unashughulikiwa na mamlaka za juu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Msemaji wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, wakati akijibu swali la mwandishi wa habari wa Ayo TV aliyetaka ufafanuzi kuhusu jezi sahihi wanazopaswa kununua mashabiki, kufuatia sintofahamu na mijadala iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Ndimbo amewatoa hofu mashabiki na kuwasihi kuwa wavumilivu wakati jambo hilo likifanyiwa kazi, akisisitiza kuwa timu ya taifa haijawahi kukabiliwa na uhaba wa mavazi ya michezo wakati wa mechi zake.

Aliposisitizwa kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu jezi rasmi ya kununuliwa sokoni, Ndimbo alihitimisha kwa kusema: "Nimeshasema linafanyiwa kazi na Mamlaka za Juu, nadhani kauli yangu inaeleweka kabisa.""Kuhusu mavazi, Timu ya Taifa haijawahi kukosa mavazi. Siku zote tumekuwa tunatumia jezi ambazo zinatumika mara zote. Kwa hiyo suala hilo lipo mtandaoni na tusingependa kulizungumza sana kwa sababu linafanyiwa kazi na Mamlaka za Juu," alisema Ndimbo.