TFF, TPLB na JUSTFIT wazindua Mpira rasmi wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26

TFF, TPLB na JUSTFIT wazindua Mpira rasmi wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi (TPLB) na Kampuni ya JUSTFIT, leo Septemba 22, 2025 wamezindua rasmi mpira maalumu utakaotumika katika michezo yote ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026.

IMG_6279.jpeg
Mpira huo, ambao umebuniwa na msanii na mbunifu maarufu Masoud Kipanya, umepewa mwonekano wa kipekee unaoendana na hadhi ya ligi kuu nchini.

1758538171116.png

Uzinduzi huo umefanyika katika ofisi za JUSTFIT zilizopo Masaki, Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na viongozi wa TFF, TPLB, wadhamini pamoja na wapenzi wa soka.
 
Picha zipo wapi? Hatutaki video weka picha tu inatosha
 
Ubora wa huo mpira ukoje, maana nautizama hizo nyuzi kwa mbali tu zipo zipo tu
 
Back
Top Bottom