TFF, Ubovu wa sehemu ya kuchezea mpira (Pitch) lawama juu yenu

TFF, Ubovu wa sehemu ya kuchezea mpira (Pitch) lawama juu yenu

Mbegu Jr

Senior Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
152
Reaction score
178
Tayari mnaendeleza kufungia viwanja mlianza na Gwambina sasa mmesha shika kasi.

Hiyo haitakuja kuwa dawa ya viwanja viwe vizuri sehemu za kuchezea pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo Never.

Watu wengi wanajua kiwanja kizuri ni kilichomwagiwa maji ya kutosha lahasha tumieni wataalamu mlionao kufanya mageuzi

Zitakeni timu zote za ligi kuu kuajiri watu kwa ajili ya nyasi utunzaji na itifaki zote zinazohusiana na pitch.

Watu hao watakao ajiriwa wapewe mafunzo ya muda mfupi na mrefu, wapatiwe vifaa vya kuwezesha utunzaji wa nyasi.

Nyasi za hivyo viwanja zilizopo kama viwanja vingi mnavyo vifungia sio za kiwango kuchezewa mpira wa kisasa

Watu wanaotunza uwanja wa Benjamin Mkapa wanajitahidi lakini sio kwa kiwango kinacho paswa kwa maana wanaachaga nyasi zinakuwa mpaka zina funika kiatu cha mchezaji, professional haitakiwi iwe vile mfano ulikuwa ni ile mechi ya Simba Sc na Biashara Fc kumbukeni kiwanja mlivyokiweka wakati wa mashindano ya Afcon ya vijana kiwanja kilikuwa bora sana wakati ule nini kinachoshindikana sasa.

Turudi kidogo kwenye Mada wekezeni kwenye eneo la kuchezea hapo ndio ubora wa mchezaji mmoja mmoja unaonekana mahitaji mengine kama kurekebisha changing rooms sio kazi ya kutisha sana kwakuwa watanzania wengi wana ujuzi kwa ujenzi na ukarabati wa majengo ni rahisi kupata hao watu.

Nawasilisha
 
Ushauri mzuri,

Tff kwa kushirikiana na wamiliki wa uwanja wahakikishe wanakuwa na proffesionals wa kuvitunza viwanja,maana unakuta kiwanja kizuri ikipita wiki 3 kishakuwa zizi.

Halafu kingine viwanja ni vya mechi na sio mazoezi,timu zije na viwanja vya mazoezi
 
Watu wengi wanaongoza mpira kwa mapenzi, bahati mbaya kuingia kwenye mfumo wa uongozi wa mpira ni kitu kigumu hawataki professionals wanataka watu wao
Sio kila kitu ni kibaya yapo mazuri mengi wanafanya lakini hili jambo ndio moja ya msingi.
Ushauri mzuri,

Tff kwa kushirikiana na wamiliki wa uwanja wahakikishe wanakuwa na proffesionals wa kuvitunza viwanja,maana unakuta kiwanja kizuri ikipita wiki 3 kishakuwa zizi.

Halafu kingine viwanja ni vya mechi na sio mazoezi,timu zije na viwanja vya mazoezi
 
Tatizo la nchi yetu kila kitu wanaingiza siasa tff na bodi ya ligi walitakiwa kufungia viwanja mapema kabla ya ligi kuanza na sio baada ya ligi kuanza.
Ligi sio lazima ichezwe kwenye mkoa wa timu inakotoka kama hawajakidhi vigezo viwanja vyao vifungiwe wajifunze kwa caf wanavyofanya ukaguzi hivyo viwanja walivyopitisha wakija caf viwanja vyenye kukidhi vigezo havitazidi vitano
 
Nchi hii viongozi wote wajuu ni mashabiki wa mpira hasa Simba na Yanga.Lakini hawana msaada wowote linapokuja swala la kuboresha viwanja. Aaafu bila aibu kuna mechi huwa wanaalikwa km wageni rasmi.
 
Viwanja vyote vikabiziwe jeshi na hata ukusanyaji wa mapato wapewe wanajeshi.hawa viongozi wa ccm na tff wanakusanya hela ila hawaendelezi viwanja vyao. Yaani hata kuweka maji ya kumwagilia uwanja hawawezi kuweka huu ni ubumbav kabisa
 
Tatizo la nchi yetu kila kitu wanaingiza siasa tff na bodi ya ligi walitakiwa kufungia viwanja mapema kabla ya ligi kuanza na sio baada ya ligi kuanza.
Ligi sio lazima ichezwe kwenye mkoa wa timu inakotoka kama hawajakidhi vigezo viwanja vyao vifungiwe wajifunze kwa caf wanavyofanya ukaguzi hivyo viwanja walivyopitisha wakija caf viwanja vyenye kukidhi vigezo havitazidi vitano
Jamani CAF njoni TZ mfungie viwanja maana timu zetu zinacheza kwenye mashamba ya viazi chonde chonde CAF njooni haraka mtusaidie wapenda soka wa TZ
 
Tff tatizo kila kitu anaviachia vilabu ..yeye ndo alipaswa kutoa muongozo na wataalamu kusaidia utunzaji mzuri wa viwanja
 
Viwanja vingekuwa bora sana kama vingekuwa vinamilikiwa na clubs za soka.na TFF ingekuwa na udhibiti dhidi ya standard za viwanja. Changamoto iliyopo viwanja vingi nchini vinamilikiwa na chama. Chama hakina interest na michezo na vilabu ni wapangishaji tu wa viwanja husika...leo club inaweza ikatumia gharama kubwa kutengeneza pitch ya uwanja...ila kesho chama ikajaza watu uwanjani kwaajili ya kampeni za mgombea ...tatizo ndo linapoanzia hapo.

Kwahili vilabu havitakiwi kupewa lawama. TFF wakae na wamiliki wa viwanja ikibidi waingie mikataba kabisa ya kuwabana juu ya standards
 
Referee na Commissars hutakiwa kukagua kiwanja 48-24hrs kabla ya mechi. Kwanini wanaruhusu mechi zichezwe??
Wangekuwa wanavikataa viwanja, TFF wangetia akili.
 
Viwanja vingekuwa bora sana kama vingekuwa vinamilikiwa na clubs za soka.na TFF ingekuwa na udhibiti dhidi ya standard za viwanja. Changamoto iliyopo viwanja vingi nchini vinamilikiwa na chama. Chama hakina interest na michezo na vilabu ni wapangishaji tu wa viwanja husika...leo club inaweza ikatumia gharama kubwa kutengeneza pitch ya uwanja...ila kesho chama ikajaza watu uwanjani kwaajili ya kampeni za mgombea ...tatizo ndo linapoanzia hapo.

Kwahili vilabu havitakiwi kupewa lawama. TFF wakae na wamiliki wa viwanja ikibidi waingie mikataba kabisa ya kuwabana juu ya standards
CHAMA CHA MAPINDUZI KINAUA SOKA LA NCHI HII. KINAMILIKI VIWANJA KARIBU VYOTE LAKINI KINASHINDWA KUVIENDELEZA....

Ccm ni TAKATAKA
#Chagua Lissu kwa Maendeleo ya Soka
 
Unailaumu bure TFF, Inachoweza kufanya ni kuvifungia tu.....
Haina uwezo juu ya hapo. TFF haimiliki kiwanja chochote nadhani.
 
CHAMA CHA MAPINDUZI KINAUA SOKA LA NCHI HII. KINAMILIKI VIWANJA KARIBU VYOTE LAKINI KINASHINDWA KUVIENDELEZA....

Ccm ni TAKATAKA
#Chagua Lissu kwa Maendeleo ya Soka
Sio kila sehemu muweke siasa zenu tunawachoka sasa....

CCM ndio inamiliki uwanja wa Gwambina? Mbona umefungiwa?
Hivi Samora si ni wa CCM?, mbona ulikuwa ni kati ya Viwanja bora?
 
Katika kitu ambacho mnailaumu bure TFF ni kwenye viwanja, na katika kitu ambacho TFF wanapaswa kupongezwa ni ili la kufungia viwanja visivyokizi, japo wamechelewa ila wanastahili pongezi.
Inabidi wavifungia viwanja vyote ili CCM wajue umuhimu wa kutunza uwanja sio kukusanya tu mapato.
 
Sio kila sehemu muweke siasa zenu tunawachoka sasa....

CCM ndio inamiliki uwanja wa Gwambina? Mbona umefungiwa?
Hivi Samora si ni wa CCM?, mbona ulikuwa ni kati ya Viwanja bora?
Hivi unaitenganisha vipi CCM na ubovu wa viwanja nchini?
Hivi viwanja vilijengwa enzi za chama kimoja, TANU ka viwanja vya wananchi. CCM imejimilikisha lakini haina hata mpango wa kuviendeleza.
Viwanja vinachakaa lakini hamna hata mpango wa kuviendeleza
 
Back
Top Bottom