TFF : wafute mechi ya Simba na Yanga.

TFF : wafute mechi ya Simba na Yanga.

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
mechi ya ligi kuu Tanzania bara baina ya watani wa jadi na timu zenye mashabiki wengi kabisa hapa nchini Simba na Yanga inatarajiwa kupigwa mnamo tarehe 1 oktoba,2016.

Kumekua na fununu kua baadhi ya viongozi wa juu wa vyama vya upinzani wamealikwa na wamekubali kuwa wageni wa heshima katika mtanange huo.

binafsi kama mdau wa michezo nimestushwa kidogo na fununu hiyo, ambayo haijawa confirmed ila nimesikitishwa pia kwa kuona michezo ikigeuzwa uchochoro wa siasa.

Huzuni hiyo sio kwakua viongozi watakaoshiriki ni toka upinzani, hapana ila ni baada ya kukumbuka tangazo la wahusika hao kusitisha maandamano yao ya Ukuta yaliyokua yafanyike tarehe 1 September na kuya hamishia tarehe 1 oktoba.

Kwa kua maandamano yaliyositishwa yalishakatazwa, kuna kila dalili ya siku hiyo ya mechi ya watani wajadi kugeuzwa sehemu ya wahusika kutimiza malengo yao. Kwa kua kusanyiko la michezo ni shughuli halali kabisa ni sehemu nzuri sana ya kutimiza kusudio bila pingamizi

Kama ni kweli hili jambo litafanyika basi naomba TFF ijitoe katika jambo hili na kutiachia wapenzi wa soka tuendelee na burudani yetu.
 
Kuanzishwa kwa timu hizo kulikuwa na malengo ya kisiasa, kama hujui basi michubuko ya nepi haijakuisha.
Simba na yanga sio vyama vya siasa wala hazikusajiliwa kwa malengo ya kisiasa. Msajili wa vyama vya siasa hazitambui kama moja ya wateja wake. Sio Simba na Yanga wala sio TFF.
 
mbona Halima Mdee ni YANGA??sasa hao wanaosema ni timu za vyama za siasa...sasa sijui 1936 Chadema ilikuwepo!!
 
Nyie mna majeshi yoooote na vyombo vyombo vyote vya dola kwa nini mnawaogopa wapinzani ambao hawana hata kikosi kimoja? Wacheni woga wa kitoto siasa za kizamani sana hizo.
Sidhani kama ni sahihi kuingiza siasa kwenye michezo.
 
Wewe ndiye unaleta siasa zako za kishamba michezoni, kwani hao wanasiaa wakienda uwanjani wanaenda kuhutubia? Jamani wakati mwingine jaribuni kuficha ujinga wenu.
Kwa post yako hii umedhihirisha kua wewe ndie mjinga zaidi yangu.
 
Uyo anajiita stroke of heart attack uyo ni gamba aliekubuhu halafu ni kipozeo wakubwa kwahiyo lazima apate waswas na ujio wa ukawa kwenye mechi hyo.
Wacha wee, Hongera kwa kupost.
 
1.hao viongozi wa vyama vya siasa ni watanzania au sio watanzania?

2.kuwa mwanasiasa ni dhambi?

3.je wanamichezo huwa wanafukuzwa wakija kwenye mikutano ya siasa?

4. How old are you??
 
Simba na yanga sio vyama vya siasa wala hazikusajiliwa kwa malengo ya kisiasa. Msajili wa vyama vya siasa hazitambui kama moja ya wateja wake. Sio Simba na Yanga wala sio TFF.
Uelewa wako ni mdogo.
 
Tunajua viongozi wote wanashabikia timu moja ama nyingine. Waende kama mashabiki na hakutakuwa na tatizo lolote. Miaka yote akina Kapuya walikuwa wakienda kama mashabiki wa Simba japo walikuwa viongozi wa serikali. Wakati huu, Mwigulu anaenda kama shabiki wa Yanga na hakuna ugomvi.

Tatizo linaweza kuja kama watadiriki kuhusisha vyama vyao na timu fulani. Wakumbuke mashabiki wapo vyote! Wakienda kama UKAWA na si mashabiki binafsi, watakaa upande gani uwanjani?
 
Hakuna mtu anaekuzidi ujinga humu Jf,labda kwa mbali ni Lizaboni.
Mkuu, kwa kusoma argument zako, napata mashaka namna ubongo wako unavyofanya kazi. Kama una familia inayokutegemea. Basi imekula hasara.
 
Back
Top Bottom