mechi ya ligi kuu Tanzania bara baina ya watani wa jadi na timu zenye mashabiki wengi kabisa hapa nchini Simba na Yanga inatarajiwa kupigwa mnamo tarehe 1 oktoba,2016.
Kumekua na fununu kua baadhi ya viongozi wa juu wa vyama vya upinzani wamealikwa na wamekubali kuwa wageni wa heshima katika mtanange huo.
binafsi kama mdau wa michezo nimestushwa kidogo na fununu hiyo, ambayo haijawa confirmed ila nimesikitishwa pia kwa kuona michezo ikigeuzwa uchochoro wa siasa.
Huzuni hiyo sio kwakua viongozi watakaoshiriki ni toka upinzani, hapana ila ni baada ya kukumbuka tangazo la wahusika hao kusitisha maandamano yao ya Ukuta yaliyokua yafanyike tarehe 1 September na kuya hamishia tarehe 1 oktoba.
Kwa kua maandamano yaliyositishwa yalishakatazwa, kuna kila dalili ya siku hiyo ya mechi ya watani wajadi kugeuzwa sehemu ya wahusika kutimiza malengo yao. Kwa kua kusanyiko la michezo ni shughuli halali kabisa ni sehemu nzuri sana ya kutimiza kusudio bila pingamizi
Kama ni kweli hili jambo litafanyika basi naomba TFF ijitoe katika jambo hili na kutiachia wapenzi wa soka tuendelee na burudani yetu.