TFF wamewadhulumu Costal Union

TFF wamewadhulumu Costal Union

Hoja yako ni mfu na inakosa mashiko.

Kuingia fainali hakukunufaishi kivyovyote vile kikanuni. Chukua kombe ufaidike.

Na hili swala si Tanzania pekee. Bali ulimwenguni pote.

Kama utakuwa mfuatiliaji wa Michuano Ulaya, Bingwa wa Europa atapata nafasi ya kushiriki moja kwa moja michuano ya UEFA hata kama katika nchi yake amekosa nafasi.

Lakini ukiingia fainali ukakosa kitu, watachukuliwa wale wanne wa mbele katika msimamo wa ligi.

Coastal Union hajadhulumiwa. Hakuna kanuni zilizotenguliwa ili kumpitisha Geita.
 
Hapa umemaliza kila kitu, Ni kama umemkata nyoka kichwa.
 
Nafikiri mfumo uko vizuri tu ligi ni mbio ndefu sana nafikiri ndio kipimo kizuri kiliko mechi chache za FA ambazo mtu anaweza kufluke akaingia fainali.
 
TFF wapo sahihi kikanuni ila huo mfumo wao ni wa ovyo sana! Sidhani kama TFF wanafikiria katika viwango ambavyo viongozi wa taasisi kama hiyo wanapaswa kufanya.
 
Azam federation n kikombe kidogo ambacho hakiwezi kutoa timu mbili!!
Nimekupata mkuu,minapenda kujifunza sana mkuu.
embu nipe elimu nijue,udogo wa michuano ya Azam ni upi mpaka kushindwa kutoa timu mbili kwenda caf?
 
Mara ya kwanza Namungo alishirikia akiwa mshindi wa pili Kwa sababu kulikuwa hamna kanuni baada ya hapo wakatengeneza kanuni hivyo timu zote zilishiriki zikijua hiyo kanuni labda hushauri wabadilishe hizo kanuni badala ya kukimbilia kulalamika.
 
Msingi wa mtoa hoja ni kuwa kanuni zipo na ndizo zilizompeleka Geita Gold kimataifa, ila anaziona kuwa ni kandamizi na dhulumishi. Sasa remedy ni ipi?

Suluhu ni Kubadili kanuni hizo. Aombe TFF wabadili kanuni. Kanuni zilizopo maana yake zilikubaliwa na kupitishwa na timu zote zilizo kwenye mashindano, kwa hiyo ni kanuni halali.

Sheria ikiwa imepitishwa kihalali, iwe mbaya au la inabaki kuwa ni sheria halali. Njia pekee ya kuifanya iwe batili ni kwa kuifuta au kurekebisha vifungu katili, kwa hiyo hizo kanuni zinazoonekana kandamizi, omba zifanyiwe marekebisho kupitia vikao halali.
 
Back
Top Bottom