Sheria za bodi ya ligi Tz inaruhusu kama una match ya kimataifa kutocheza match yoyote ya VPL ndani ya siku 6, nadhani walivyokuwa wanaweka hizi sheria waliangalia zaidi mazingira yetu Tz na Africa kwa ujumla. Mfano, Namungo unaweza mwambia acheze match jumanne Lindi halafu jmosi ana match ya Kimataifa? Miundombinu yetu ya usafiri bado ni duni, safari zinachukua muda mrefu wakati hizo timu za Ulaya zinatumia tu chartered flights tena kwa ndege zinazomilikiwa na timu kabisa, wao watatumia 4hrs while Tz/ africa mtatumia ma siku na uchovu juu.