TFF, Wizara ya Michezo na wahusika mmewahi kushiriki kongamano la Soccerex?

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Hili ni kongamano la kimataifa ambalo hufanyika kwa minajili ya kujadili soka katika mtizamo wa kibiashara. Mwaka huu liifanyika Afrika Kusini katika Uwanja wa Moses Mabhida.

Kama inavyoelezwa hapo chini, wahudhuriaji walikuwa ni pamoja na mawaziri wa michezo wa nchi husika, nadhani pamoja na wadau wengine kutoka taasisi za soka.

Swali langu kwa wadau, nchi yetu ilipata ushiriki katika kongamano hili muhimu kwa mustakabali wa soka la nchi?

The third edition of the Soccerex African Forum, 4-5 November 2014, consolidated the event as the largest and leading football business conference in the continent and the premier meeting place for the industry to come together to learn, network and do business.

Held in partnership with the KwaZulu-Natal Provincial Government and eThekwini Municipality, at the magnificent Moses Mabhida Stadium, it gathered the game’s leading administrators, national sports ministers, key business figures and football legends, all with the same objective of growing the business side of football on the continent.

In 2014, the Forum built on the success of the two previous editions and attracted once again the industry’s key stakeholders to Durban. Institutionally supported by theConfederation of African Football (CAF) and South African Football Association, it provided a platform for the key issues to be addressed including club licensing, league development, major event delivery, commercial best practice as well as a large emphasis on the relationship between sport and governance, seeing key government representatives and national FA ministers in attendance.

Chanzo: African Forum 2014 « Soccerex

Waione: Jamal Malinzi, lonestiker, mzabzab, mwangalingimungu, Mamndenyi, Malafyale, EMT, Gang Chomba, Kipaji Halisi, Nakapanya, RUCCI, vanmedy
 
Last edited by a moderator:
Mphamvu Tanzania tumekuwa tukishiriki mara kwa mara.Mwezi juni nilihudhuria soccerex Asia mjini Amman Jordan,September Mh Waziri Dr Mukangara alihudhuria soccerex Europe huko Manchester,na mwaka huu tulialikwa Durban na mimi nilikuwa mtoa mada ila dharura ilinipata nikashindwa kuhudhuria.Ni kweli soccerex ni forum nzuri inakutanisha wadau wa soka.
 
Nadhani kongamano kuwa la Asia au Europe kuna maana yake, kwani changamoto na mazingira ya Afrika si sawa na ya huko kwa hiyo nadhani haya makongamano ya Afrika ndio muhimu sana kwetu.

Kingine, Fenela Mukangara ni mwanasiasa, pengine hajui lolote kuhusu biashara ya soka wala utendaji wake, kumfanya kuwa mwakilishi wetu kwenye makongamano ya kiutendaji sio ishu, maana tutakuwa tumepeleka washiriki tu na sio kwenda kujifunza.

Hongera sana kwa juhudi zako binafsi za kuhudhuria shughuli za muhimu kama hizi, lakini vipi mrejesho? Na kwanini watendaji ndani ya shirikisho na vyombo husika wakashirikishwa zaidi kwenye mambo kama haya yenye muelekeo chanya?
 
Last edited by a moderator:
Hili ni kongamano la kimataifa ambalo hufanyika kwa minajili ya kujadili soka katika mtizamo wa kibiashara. Mwaka huu liifanyika Afrika Kusini katika Uwanja wa Moses Mabhida.

Kama inavyoelezwa hapo chini, wahudhuriaji walikuwa ni pamoja na mawaziri wa michezo wa nchi husika, nadhani pamoja na wadau wengine kutoka taasisi za soka.

Swali langu kwa wadau, nchi yetu ilipata ushiriki katika kongamano hili muhimu kwa mustakabali wa soka la nchi?

Chanzo: African Forum 2014 « Soccerex

Waione: Jamal Malinzi, lonestiker, mzabzab, mwangalingimungu, Mamndenyi, Malafyale, EMT, Gang Chomba, Kipaji Halisi, Nakapanya, RUCCI, vanmedy

Kwenye zama hizi za utandawazi, inawezekana kuhudhuria kongamano, warsha au semina bila ya kuweko huko inakofanyikia (video conferencing, webinars, n.k.) kwa hivyo mahudhurio sio jambo muhimu sana. Muhimu ni kinachotekelezwa kutokana na mikutano hiyo. Kwanza, anayehudhuria anafikishaje ujumbe wa mkutano huo kwa wadau anaporudi nyumbani. Pili, kilichofunzwa, kuelimishwa, kuazimiwa au kushauriwa kwenye mikutano hiyo kimetekelezwa na kutekelezekaje hapa nchini. Nadhani TFF watueleze hayo, kuliko kama wamehudhuria ama la.
 
Ndio mkuu, lakini kwa kizazi hiki kizembe walau wangetuambia kama walihudhuria kwanza. Kisha tuwahoji mrejesho... Sijui ni wadau wangapi wanajua kama kuna mambo chanya kma haya huku Afrika!
 
Nakubaliana nawe mkuu, lakini baadhi yetu huogopa kujulikana kama tumerudi safari kwa kuhofia kudaiwa zawadi (hasa na nyumba ndogo!). Lakini si kuna msemaji wa TFF anayetoa taarifa za kila wiki? Imekuwaje taarifa nzuri kama hiihaikutoka?
 
Mrejesho wa taarifa ni tatizo la taasisi za serikali na hata watu binafsi, hata baba kutoa mrejesho wa safari kwa mama ni ishu.

Teh!
 
Back
Top Bottom