TFF ya Malinzi Imepoteza Uhalali wa Kutawala Muhula wa Pili

TFF ya Malinzi Imepoteza Uhalali wa Kutawala Muhula wa Pili

Tatizo ukiwa shabiki wa yanga akili huwa iko pembeni kabisa.Jamaa anakosoa TFF,mtu anakuja na hoja ya point za mezani. Hoja hupingwa kwa hoja.Hivi hii TFF iliyoshusha kiwango cha timu ya taifa unawezaje kuitetea. Yaani kuwa na ligi kubwa kama hii na kutoa wawakilishi hafifi wanao tolewa kwa vipigo vya mbwa mwizi ni TFF ya kutetewa.Naona hapa kunashida kwenye ufahamu.Point za mezani hazifai lakini kama kanuni inatoa point hizo, si swala la simba pekee maana hata timu zingine ziliipoka simba point mezani.Tujaribu kujibu hoja na si vioja.

Mkuu uwezo wa watu wengi kujadili hoja unapungua sana siku hizi.

Kila linalozungumzwa litajibiwa na matusi, kashfa na ujinga mwingine wowote. Halafu mbaya zaidi hawa hawa watukanaji ndio wanakuja kuwa viongozi wa vilabu vyetu, kamati na hata TFF yenyewe!!!! Na hawa ndio wapiga kura wanaoingiza madarakani viongozi aina ya hawa waliopo TFF. Unategemea nini? Fikiria michango yote hii, ni michango miwili tu ndio imekosoa hoja wengine ni ndio kama unavyoona hoja zao.
 
Back
Top Bottom