TFF yafungua shauri dhidi ya Ofisa wa Yanga, Haji Manara baada ya kudaiwa kuzozana na Rais Karia

TFF yafungua shauri dhidi ya Ofisa wa Yanga, Haji Manara baada ya kudaiwa kuzozana na Rais Karia

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Sekretarieti ya TFF imefungua shauri mbele ya kamati ya maadili dhidi ya Ofisa wa Klabu ya Yanga Haji Manara, kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Manara alionekana akijibishana na kiongozi wa juu wa TFF ambaye ni Rais Wallace Karia, jana Julai 2,2022 wakati wa fainali la Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup Jijini Arusha, jambo ambalo linaonekana ni kinyume na maadili ya mpira wa miguu Nchini.

FB_IMG_1656834501724.jpg
 
Hahaha ila manara ni mnafiki aisee yani kwa ile makala aliyoiandika leo akimlalamikia jemedari ujue mi nilianza kuingia kingi kumuamini kuwa anasingiziwa?

Kwanza nilisita kuamini ile clip iliyodaiwa kuwa haji kamtolea matusi ya nguoni Karia kwasababu hayo matusi kwenye hiyo clip hayasikiki.

Manara kwenye article yake ameonesha kukereka sana na jemedari kiasi ambacho hadi uongozi wa Yanga umemshauri apeleke hili jambo kwenye ngazi za sheria.

Lakini nilivyoona hiyo statement ya TFF hapo ndio nineanza kuamini kuwa hata ile video iliyodaiwa kuwa manara anamtukana karia ni ya kweli.

Sasa ni muda wa wana Yanga kuonesha mapenzi kwa msemaji wao kwa kumsimamia kwenye hii kesi ashinde ili aendelee kuwapa makombe
 
Sekretarieti ya TFF imefungua shauri mbele ya kamati ya maadili dhidi ya Ofisa wa Klabu ya Yanga Haji Manara, katokana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Manara alionekana akijibishana na kiongozi wa juu wa TFF jana wakati wa fainali la Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup, jambo ambalo linaonekana ni kinyume na maadili ya mpira Nchini.

View attachment 2279726
Ajiandae kulipa fine tu au akae mkao wa kupigwa 'ban' .
 
Hahaha ila manara ni mnafiki aisee yani kwa ile makala aliyoiandika leo akimlalamikia jemedari ujue mi nilianza kuingia kingi kumuamini kuwa anasingiziwa?

Kwanza nilisita kuamini ile clip iliyodaiwa kuwa haji kamtolea matusi ya nguoni Karia kwasababu hayo matusi kwenye hiyo clip hayasikiki.

Manara kwenye article yake ameonesha kukereka sana na jemedari kiasi ambacho hadi uongozi wa Yanga umemshauri apeleke hili jambo kwenye ngazi za sheria.

Lakini nilivyoona hiyo statement ya TFF hapo ndio nineanza kuamini kuwa hata ile video iliyodaiwa kuwa manara anamtukana karia ni ya kweli.

Sasa ni muda wa wana Yanga kuonesha mapenzi kwa msemaji wao kwa kumsimamia kwenye hii kesi ashinde ili aendelee kuwapa makombe
nimekua na mtazamo km wako
 
TFF imemlea sana Manara. ni mtu hatari asie na akili na anatumia mdomo wake kwa vyovyote vile kupata mlo. ikumbukwe aliichafua sana sura ya mpira wa tanzania alipopost Simba inatumia madawa na hujuma kwa timu za wageni. majhuzi kasema sajili zetu kuna watu wanaleta mchezaji dola laki moja arobaini ya kwao ambayo tafsiri yake kuna rushwa kubwa sana kwenye mpira wa Tanzania. Hata kama madai hayo yana ukweli lakini sio kwa njia ya kuchafua nchi nzima. TFF imuondoe kabisa Manara kwenye mira wa Tanzania ni sawa na kufuga Mbwa aje akuume msikitini.
 
Manara ni limbukeni, anadhani kila atakachofanya ataaminiwa zaidi na mashabiki wa utopolo kumbe anajitafutia balaa, amekuwa mropokaji mjinga asiyetumia akili kabisa.

Sasa kama TFF walimfungia Shafii Dauda kwa kosa dogo kama lile, huyu Manara wasipomfungia zaidi ya miaka saba nitaamini TFF wanatumiwa na GSM, na Shafii walimuonea.
 
Kwa kila story ina two sides, Mr.Manara hakukurupuka tu ,na hatujui Mr.Kiria alimwambia nini Mr.Manara, Ile mentality tuliyokua nayo kuwa viongozi hawakosei ndio inatuweka hapa tulipo, hivi kuna leader yeyote kwenye historia ya nchi yetu ambaye alishawahi to apologize ?,nikipewa hata mfano mmoja hapa,nita withdraw na to apologize kwa comment yangu hii.
 
Back
Top Bottom