atapigwa pini wait..Kazi ipo Manara ajiandae kisaikolojia..
Ajiandae kulipa fine tu au akae mkao wa kupigwa 'ban' .Sekretarieti ya TFF imefungua shauri mbele ya kamati ya maadili dhidi ya Ofisa wa Klabu ya Yanga Haji Manara, katokana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.
Manara alionekana akijibishana na kiongozi wa juu wa TFF jana wakati wa fainali la Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup, jambo ambalo linaonekana ni kinyume na maadili ya mpira Nchini.
View attachment 2279726
nimekua na mtazamo km wakoHahaha ila manara ni mnafiki aisee yani kwa ile makala aliyoiandika leo akimlalamikia jemedari ujue mi nilianza kuingia kingi kumuamini kuwa anasingiziwa?
Kwanza nilisita kuamini ile clip iliyodaiwa kuwa haji kamtolea matusi ya nguoni Karia kwasababu hayo matusi kwenye hiyo clip hayasikiki.
Manara kwenye article yake ameonesha kukereka sana na jemedari kiasi ambacho hadi uongozi wa Yanga umemshauri apeleke hili jambo kwenye ngazi za sheria.
Lakini nilivyoona hiyo statement ya TFF hapo ndio nineanza kuamini kuwa hata ile video iliyodaiwa kuwa manara anamtukana karia ni ya kweli.
Sasa ni muda wa wana Yanga kuonesha mapenzi kwa msemaji wao kwa kumsimamia kwenye hii kesi ashinde ili aendelee kuwapa makombe