TFF yaingiza mguu rasmi sakata la Yanga, yamtaka Katibu Mkuu aonyeshe mkataba

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Taarifa za Yanga kuingia mkataba wa kuikodisha timu kwa miaka kumi kwa Kampuni ya Yanga Yetu zimezidi kuchukua sura mpya ambapo licha ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kupinga utaratibu uliotumika, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nalo limefunguka kuhusu jambo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amezungumza kuhusu mabadiliko ambayo wameyafanya na kusema wao kama TFF bado hawajayatambua mabadiliko hayo na wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit ya kumtaka aonyesha mkataba ambao wameingia na kampuni ya Yanga Yetu.

“Nimemuandika barua Katibu Mkuu wa Yanga atupe nakala ya mkataba ule (wa Yanga na Kampuni ya Yanga Yetu), ili kama kuna wasiwasi hilo tatizo lishughulikiwe mapema maana hizi klabu niza wanachama, wanaweza kuingia mikataba na wanachama wengine wakaja na mambo mengine,

“Tunataka mkataba uwe wazi ili hata klabu zingine zijifunze, kwahiyo Yanga tumewaomba walete copy ya huo mkataba nini kinaazimwa na kipi kinauzwa, klabu itaendeshwaje na baada ya hapo kamati za TFF zitakaa kulijadili jambo hilo, kama itakuwa tofauti na kanuni zetu tutarudi kwao warekebishe mambo ambayo hayapo sawa,” alisema Mwesigwa na kuongeza.

“Uendeshwaji lazima ubadilike kuendana na wakati lakini hatutaki mabadiliko yasababishe mvurugano ambao haukuwepo kwa muda mrefu na tumeshapokea barua nyingi za wanachama wa Yanga hadi wazee wamekuja wanasema wanataka kwenda kumwona mkuu wa nchi”

Aidha alisema TFF bado inatambua Yanga inasimamiwa na uongozi wa klabu kama ilivyokuwa awali ikiongozwa na Mwenyekiti, Yusuph Manji na kama kutakuwa na jambo la tofauti watatoa taarifa baada ya kujiridhisha mfumo ambao Yanga itakuwa inautumia kukodisha timu kwa Kampuni ya Yanga Yetu.

Chanzo: Dewji Blog
 
TFF kaeni pembeni chama liendeshwe kisasa.au mnataka nasi tuwe hiovyo kiutendaji kama hilo litff lenu?
Mkuu tuweke mapenzi yetu kwa Yanga pembeni.
Kwa jicho la kibiashara kuna tatizo mahali,tusubiri kuona hiyo nakala ya mkataba ikoje.
Halafu miaka 10 ni mingi sana.
Tungefanya japo miwili kisha tukijiridhisha na hao Yanga Yetu tuongeze mkataba.
 
Mkuu chanzo dewji
 
Wewe acha unafiki mpaka sasa umeichangia yanga kiasi gani mpaka useme hivyo?
 
Mkuu tuweke mapenzi yetu kwa Yanga pembeni.
Kwa jicho la kibiashara kuna tatizo mahali,tusubiri kuona hiyo nakala ya mkataba ikoje.
Halafu miaka 10 ni mingi sana.
Tungefanya japo miwili kisha tukijiridhisha na hao Yanga Yetu tuongeze mkataba.
 
Mkuu tuweke mapenzi yetu kwa Yanga pembeni.
Kwa jicho la kibiashara kuna tatizo mahali,tusubiri kuona hiyo nakala ya mkataba ikoje.
Halafu miaka 10 ni mingi sana.
Tungefanya japo miwili kisha tukijiridhisha na hao Yanga Yetu tuongeze mkataba.
Kanjubai anataka 10 kinyume na hapo hatoi mpunga, na anajua ndani ya miaka 10 amerudisha pesa yake na faida kibao, Hakuna muhindi fala
 
Mkuu tuweke mapenzi yetu kwa Yanga pembeni.
Kwa jicho la kibiashara kuna tatizo mahali,tusubiri kuona hiyo nakala ya mkataba ikoje.
Halafu miaka 10 ni mingi sana.
Tungefanya japo miwili kisha tukijiridhisha na hao Yanga Yetu tuongeze mkataba.

Yanga mwenzangu hebu nikuulize, hii nembo ambayo Manji anataka kuichukua kwa miaka 10 tunasema Mingi, Nembo hii hii Yanga wanayo inakaribia Miaka 80 sasa, hatujaona lolote.
Ipi miaka mingi kati ya 10 aliyoomba Manji ambayo hatujajua anataka kuifanyia nini Yanga, na Miaka karibu 70 na ushee ambayo akina mzee Akilimali walikuwa na hiyo nembo kwa muda wote huo bila ya kufanya chochote?
 
Miaka 70 iliyopita ni tofauti na sasa na hiyo 10 ijayo.
Kiukweli miaka 10 ni mingi sana...kwanini tunataka kuitupa timu yetu bila ya kujua mkataba unasemaje?
Mkataba uwekwe wazi,hatutaki madudu ya mikataba feki na kandamizi ndani ya club yetu kipenzi.

Namkubali sana Manji...sana tu.Ila kwa hili tunatakiwa tutumie jicho la kibiashara katika ulimwengu wa sasa na sio mapenzi na mihemuko.
Mwisho ifike miaka mitatu tuanze kutafutana mchawi huku ikiwa imebaki miaka 7!
Miaka 10 sio mchezo mkuu.

Halafu ona unavyosema "miaka 10 aliyoomba Manji ambayo hatujui anataka kuifanyia nini Yanga"
Like serious jamani?
Tuingie mkataba na mtu ambaye hajaweka wazi anataka kuifanyia nini Club yetu?
Nimesikitika sana.
 
Uko sawa dada, huwezi kuingia mkataba na club halafu wanachama hwajui huo mkatabata unasema nini juu ya club.
Tumeona kwa simba angalau huyo jamaa kanunua hisa zinajulikana.
Manji anaskendal nyingi za kununua viwanja vya wazi kama cocobeach na sehemu nyingine kiujanjaujanja tu.
Akitaka kununua Yanga basi mkataba uwe wazi.
 
Mkuu tuweke mapenzi yetu kwa Yanga pembeni.
Kwa jicho la kibiashara kuna tatizo mahali,tusubiri kuona hiyo nakala ya mkataba ikoje.
Halafu miaka 10 ni mingi sana.
Tungefanya japo miwili kisha tukijiridhisha na hao Yanga Yetu tuongeze mkataba.
Halafu watu sicho jua ni kwamba TFF na BMT wanayo haki ya kujua kilichopo kwenye mkataba na kufatilia kwa karibu kila hatua kwa kuwa hao ndio wenye dhamana ya mpira na vialabu. Kwanza pia Yanga na simba wanatakiwa kufanya mabadiliko ya katiba zao ili kuendana na wanayo yahitaji na hilo lazima TFF na BMT wajue kwa kina na wanatakiwa washirikishwe kwenye kila jambo kuanzia utathmini wa mali za klabu na madeni na lazima wajue vyanzo vya fedha za hao wanao taka kuwekeza.... hili ni jambo la kawaida nashangaa wanao pinga.

Kama kweli wawekezaji wana nia njema basi watatoa ushirikiano na hakuna ubaya.
 
Miaka 70 iliyopita ni tofauti na sasa na hiyo 10 ijayo.
Kiukweli miaka 10 ni mingi sana...kwanini tunataka kuitupa timu yetu bila ya kujua mkataba unasemaje?
Mkataba uwekwe wazi,hatutaki madudu ya mikataba feki na kandamizi ndani ya club yetu kipenzi.

Namkubali sana Manji...sana tu.Ila kwa hili tunatakiwa tutumie jicho la kibiashara katika ulimwengu wa sasa na sio mapenzi na mihemuko.
Mwisho ifike miaka mitatu tuanze kutafutana mchawi huku ikiwa imebaki miaka 7!
Miaka 10 sio mchezo mkuu.

Halafu ona unavyosema "miaka 10 aliyoomba Manji ambayo hatujui anataka kuifanyia nini Yanga"
Like serious jamani?
Tuingie mkataba na mtu ambaye hajaweka wazi anataka kuifanyia nini Club yetu?
Nimesikitika sana.
halafu kilicho nishangaza kwenye ule mkataba ni kipengele kinacho sema baada ya kumalizika mkataba mali zilizo patikana chini ya yanga yetu company zitabaki kuwa za mkodishaji,,,,,kimsingi Yanga hawatonufaika nachochote kwenye huu makataba na kama akijenga uwanja na mkataba ukaisha basi uwanja utabaki wa Manji......
 
Manji ashamwaga pesa kwa wanachama wote vidomodomo wapo kimyaaa,sijasikia wakiupinga huo mkataba WA ukodishaji ambao Una dariri zote wa kufanana na mkataba WA chief Mangungo wa Msovelo.
 
TFF kaeni pembeni chama liendeshwe kisasa.au mnataka nasi tuwe hiovyo kiutendaji kama hilo litff lenu?
NADHANI NI WAKATI MUAFAKA KABISA KUFIKIRIA NAMNA YA KUIKODISHA TFF KWANI KWA KUFANYA HIVYO PENGINE ITAONDOA FIGISUFIGISU, UBABE, UPENDELEO ETC ETC
 
hahahaa mliokula pesa za manji utakunya pili pili
 
Back
Top Bottom