Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuiondoa Mahakamani kesi ya Madai Namba 14708 ya 2024 iliyofunguliwa na Kocha Liston Katabazi ambaye anaidai fidia ya Shilingi 700,000,000 kutokana na TFF kuchapisha taarifa ya kufungiwa maisha kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi, Anna Magutu, awali ilianza kutajwa Julai 17, 2024, leo iliitwa kwa ajili ya kutajwa ambapo ambapo TFF wamewasilisha pingamizi hilo ikidai kwamba Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na Mahakama hiyo imepanga kusikiliza pingamizi hilo Septemba 11, 2024.
Katabazi katika shauri hilo anawakilishwa na Wakili Peter Majanjala kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC), malalamiko yake ni kwamba ameadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Juni 23, 2021 ilhali yeye si mwanachama wa Shirikisho hilo
Pia Kanuni za Maadili ya TFF, Toleo la 2021 zilizotumika kumuadhibu ziko kinyume cha Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Namba 12 ya Mwaka 1967 na marekebisho yake Namba 6 ya Mwaka 1971, rejea kanuni za usajili za vyama vya michezo Tanzania za 1999 zikisomwa pamoja na kanuni za BMT za mwaka 1999 na marekebisho yake 2020.
Shauri lililosomwa leo Agosti 20, 2024, TFF iliwakilishwa na mwanasheria wake, Rahim Shabani.