Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetupilia mbali shauri la klabu ya Simba lililokuwa likipinga uhalali wa usajili wa mchezaji Mohamed Damaro Camara, ikieleza kuwa halina msingi wa kikanuni.
Awali, Simba iliwasilisha malalamiko ikidai kuwa usajili wa Camara unaifanya Yanga kuwa na jumla ya wachezaji 13 wa kigeni, kinyume na idadi inayoruhusiwa ya 12, hatua ambayo walidai inakiuka Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu pamoja na kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Soma zaidi: Mwanasheria wa Simba SC: Damaro na Yanga SC wao hawajafika, Sheria inaruhusu kwenda CAS kama tusiporidhishwa
Hata hivyo, kamati hiyo katika uamuzi wake ilibainisha kuwa usajili wa Camara haukiuki kanuni zozote zilizotajwa, na hivyo kuthibitisha kuwa ni halali, huku ikieleza kuwa uamuzi kamili wa shauri hilo utawasilishwa rasmi kwa klabu ya Simba.