TFF yaitwa tena mahakamani kesi yakumfungia kocha Liston Katabazi

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mchakato usikilizwaji wa kesi ya madai inayolikabili Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyofunguliwa na Kocha Liston Katabazi akihoji uhalali wa kanuni za maadili zilizotumika kumuadhibu kifungo cha maisha kutojishughulisha na soka, sasa umeanza rasmi upya.

Tayari Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, imetoa hati za wito kwa wadaiwa, wadhamini waliosajiliwa wa TFF na TFF yenyewe ikiwataka kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kujitetea.

Kwa mujibu wa hati hizo za wito kwa wadaiwa zilizosainiwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Hakimu Mkazi Mkuu Franco Kiswaga, Oktoba 13, 2025, kesi hiyo imepangwa Oktoba 21, 2025, saa 3:00 asubuhi.

"Unatakiwa kufika katika mahakama hii bila kukosa na siku hiyo unatakiwa kutoa nyaraka zako zote unazokusudia kuzitimia katika kesi yako", zinasomeka hayo hizo ambazo pia TFF ilizipokea jana hiyo.

Hatua hiyo ya Mahakama ya Kisutu kuanza upya mchakato wa usikilizwaji wa kesi hiyo ni utekelezaji wa maelekezo na amri ya Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.

Mahakama Kuu iliiamuru mahakama hiyo kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo baada ya kukubali rufaa aliyoikata Katabazi kupinga uamuzi huo wa Kisutu ulioitupilia mbali kesi hiyo awali.

Pia Soma: Liston Katabazi kuiburuta TFF Mahakamani na kuidai Sh Milioni 700
1760427684844.png
 
Masuala ya football hayaendi mahakama za kiraia Bali mahakama za michezo kama CAS
 
Huyo kocha ni ng'ombe kabisa , masuala ya mpira anaenda mahakama za ki rahia? Kwanini asiende CAS?
 
Hizi adhabu za kufungia maisha kufungia kuanzi mwaka mzima hadi kufungia maisha siyo za kusaidia kuendeleza mpira ila ni za kukomoa. TFF waachane na ujinga huo. Hatujasikia weneztu Ulaya wakifungiwa maisha, hata timu za EPL ambazo mashabiki wake huwa na vurugu sana huwa hazipewi adhabu za kijinga hivyo.
 
Back
Top Bottom