brave one
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 4,879
- 7,386
Shirikisho la soka nchi limefanikiwa kuingia mkataba wa miaka 4 na azam media wenye thamani ya tsh bil 3.3 kwa ajili ya mashindano ya kombe la shilikisho. Mashindano hayo yataendeshwa kwa njia ya mtoano , huku timu 64 zikitarajiwa kushiriki mashindano hayo, timu 16 za ligi kuu, timu 24 za ligi daraja la 1 na timu 24 za ligi daraja la 2, timu za ligi kuu zitaanzia raundi ya 2 ambayo itajumuisha timu 32, timu mwenyeji itakuwa inapata tsh. mil 1 kwa ajili za maandalizi huku timu ya ugenini itakuwa inapata tsh. mil 3 kwa ajili ya maandalizi hii ni kwa kila mechi, timu zitakazo fanikiwa kufika fainali zitakuwa zimecheza mechi 7(Mechi zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini kasoro mechi ya fainali tu), bingwa wa mashindano haya atapata zawadi ya tsh. mil 50 na atapata nafasi za kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kombe la shilikisho barani africa.. Hongereni sana TFF kwa hili mnastahili pongezi
=========================
Chanzo: Binzubeiry
=========================
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington (kulia) akibadilishana mikataba na Rais wa TFF, Jamal Malinzi
KAMPUNI ya Azam Media Limited, imesaini Mkataba wa miaka minne na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kudhamini michuano ya Kombe la Shirikisho, zamani (FA) wenye thamani ya Sh. Bilioni 3.3.
Katika halfa iloyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa jengo la Kisenga LAPF, Kijitonyama, Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amesema kwamba amefurahia kufanikisha azma ya kurejesha mashindano hayo.
Malinzi amesema kwamba duniani kote maendeleo ya soka yanatokana na kuwepo na mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kombe la Shirikisho la nchi, ambayo yanashirikisha na klabu za chini hadi zile zinazoshiriki Ligi Kuu.
"Nitafurahi sana kuona klabu ya Daraja la Pili inashinda Kombe hilo, duniani kote Kombe hili lipo na klabu za chini zimekuwa zikiwapiga ‘visu' wale wakubwa," alisema Malinzi.
Aliongeza kuwa bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha Sh. Milioni 50 wakati kila timu itakayokwenda kucheza ugenini itapata Sh. Milioni tatu za safari na mwenyejii atapewa Sh. Milioni 1 ya maandalizi.
"Tumeona bingwa wa michuano hii apate Sh. Milioni 50 kwa sababu atakuwa amecheza mechi saba na yule wa Vodacom anayecheza michezo 30 anapata Sh. Milioni 70," Malinzi aliongeza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, Geoffrey Nyange ‘Kaburu' alisema jana kuwa mashindano ya mwaka huu yatashirikisha klabu 64 na yataendeshwa kwa njia ya mtoano.
Kaburu, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Simba SC, amezitaja timu hizo kuwa ni pamoja klabu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara, timu 24 za Daraja la Kwanza na idadi kama hiyo za Daraja la Pili.
Alisema kwamba mshindi wa kombe hilo atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) mwaka 2017.
RATIBA YA MECHI ZA RAUNDI YA KWANZA
AFC vs Polisi Mara
Polisi Tabora vs Green Warriors
Kariakoo Lindi vs Changanyikeni Dar
Mkamba Rangers vs Ruvuma FC ya Kigoma
Rhino ya Tabora vs Alliance FC ya Mwanza
Panone vs Cocacola Kwanza ya Mbeya
Polisi Moro vs Mshikamano Sports
Sabasaba Utd vs Abdajalo ya Tabora
Magereza Iringa vs Polisi Dar
Mirambo vs Town Small Boys Ruvuma
Abdajalo Dar vs Transcamp
Ruvu Shooting vs Cosmopolitan
Singida Utd vs Bulyhanhulu
JKT Rwamkoma vs Villa Squad
Wenda vs Madini Sports Arusha
Pamba vs Polisi Dodoma.
Chanzo: Binzubeiry