TFF yarudisha kombe la FA (FA CUP) rasmi, AZAM MEDIA yadhamini kwa Billion 3.3

TFF yarudisha kombe la FA (FA CUP) rasmi, AZAM MEDIA yadhamini kwa Billion 3.3

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Shirikisho la soka nchi limefanikiwa kuingia mkataba wa miaka 4 na azam media wenye thamani ya tsh bil 3.3 kwa ajili ya mashindano ya kombe la shilikisho. Mashindano hayo yataendeshwa kwa njia ya mtoano , huku timu 64 zikitarajiwa kushiriki mashindano hayo, timu 16 za ligi kuu, timu 24 za ligi daraja la 1 na timu 24 za ligi daraja la 2, timu za ligi kuu zitaanzia raundi ya 2 ambayo itajumuisha timu 32, timu mwenyeji itakuwa inapata tsh. mil 1 kwa ajili za maandalizi huku timu ya ugenini itakuwa inapata tsh. mil 3 kwa ajili ya maandalizi hii ni kwa kila mechi, timu zitakazo fanikiwa kufika fainali zitakuwa zimecheza mechi 7(Mechi zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini kasoro mechi ya fainali tu), bingwa wa mashindano haya atapata zawadi ya tsh. mil 50 na atapata nafasi za kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kombe la shilikisho barani africa.. Hongereni sana TFF kwa hili mnastahili pongezi

=========================
TFF2.jpg

Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington (kulia) akibadilishana mikataba na Rais wa TFF, Jamal Malinzi

KAMPUNI ya Azam Media Limited, imesaini Mkataba wa miaka minne na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kudhamini michuano ya Kombe la Shirikisho, zamani (FA) wenye thamani ya Sh. Bilioni 3.3.

Katika halfa iloyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa jengo la Kisenga LAPF, Kijitonyama, Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amesema kwamba amefurahia kufanikisha azma ya kurejesha mashindano hayo.

Malinzi amesema kwamba duniani kote maendeleo ya soka yanatokana na kuwepo na mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kombe la Shirikisho la nchi, ambayo yanashirikisha na klabu za chini hadi zile zinazoshiriki Ligi Kuu.

"Nitafurahi sana kuona klabu ya Daraja la Pili inashinda Kombe hilo, duniani kote Kombe hili lipo na klabu za chini zimekuwa zikiwapiga ‘visu' wale wakubwa," alisema Malinzi.

Aliongeza kuwa bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha Sh. Milioni 50 wakati kila timu itakayokwenda kucheza ugenini itapata Sh. Milioni tatu za safari na mwenyejii atapewa Sh. Milioni 1 ya maandalizi.

"Tumeona bingwa wa michuano hii apate Sh. Milioni 50 kwa sababu atakuwa amecheza mechi saba na yule wa Vodacom anayecheza michezo 30 anapata Sh. Milioni 70," Malinzi aliongeza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, Geoffrey Nyange ‘Kaburu' alisema jana kuwa mashindano ya mwaka huu yatashirikisha klabu 64 na yataendeshwa kwa njia ya mtoano.

Kaburu, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Simba SC, amezitaja timu hizo kuwa ni pamoja klabu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara, timu 24 za Daraja la Kwanza na idadi kama hiyo za Daraja la Pili.

Alisema kwamba mshindi wa kombe hilo atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) mwaka 2017.

RATIBA YA MECHI ZA RAUNDI YA KWANZA

AFC vs Polisi Mara

Polisi Tabora vs Green Warriors

Kariakoo Lindi vs Changanyikeni Dar

Mkamba Rangers vs Ruvuma FC ya Kigoma

Rhino ya Tabora vs Alliance FC ya Mwanza

Panone vs Cocacola Kwanza ya Mbeya

Polisi Moro vs Mshikamano Sports

Sabasaba Utd vs Abdajalo ya Tabora

Magereza Iringa vs Polisi Dar

Mirambo vs Town Small Boys Ruvuma

Abdajalo Dar vs Transcamp

Ruvu Shooting vs Cosmopolitan

Singida Utd vs Bulyhanhulu

JKT Rwamkoma vs Villa Squad

Wenda vs Madini Sports Arusha

Pamba vs Polisi Dodoma.

Chanzo: Binzubeiry
 
kwa hili TFF hongereni sana cha msingi wekeni usimamizi imara, huko ndo mtavipata vipaji na sio kuendelea na maboresho ...
 
Mathalani ktk Vpl na Fa kote bingwa akawa Azam,Simba au Yanga je ataiwakilisha nchi ktk makombe yote mawili yaan champions na shirikisho au ni vipi???



Mwenye uelewa anieleweshe
 
duh! kwa mwendo huu kuna timu naiona hapa kupåndå ndege kwendå kushiriki måshindåno yå kimåtåiffå itakuwa stori wåtabaki kuyåsikiliziå kwenye redio nå kuyåonå kwenye luninga tu


#team wåmchångåni fc#
 
Mathalani ktk Vpl na Fa kote bingwa akawa Azam,Simba au Yanga je ataiwakilisha nchi ktk makombe yote mawili yaan champions na shirikisho au ni vipi???



Mwenye uelewa anieleweshe
Mathalani timu ya wananchi dar young africans amekuwa bingwa wa makombe yote mawili yaani bingwa wa ligi kuu Tanzania bara na bingwa wa kombe la Azam sports federation cup (Asfc) basi mshindi wapili wa kombe la shirikisho ataiwakilisha tz katika mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Nadhani nimeeleweka vya kutosha.
 
TFF kwanini wameliita FA Cup?

FA nijuavyo ni Football Association.

Kwanini wasiliite FF Cup?

Tanzania ni Football Federation,

FF ndiyo sahihi.
 
Mathalani timu ya wananchi dar young africans amekuwa bingwa wa makombe yote mawili yaani bingwa wa ligi kuu Tanzania bara na bingwa wa kombe la Azam sports federation cup (Asfc) basi mshindi wapili wa kombe la shirikisho ataiwakilisha tz katika mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Nadhani nimeeleweka vya kutosha.

Nimekupata mkuu mkolaj,
Kumbe ataenda kushiriki kwa hisani ya Yanga
 
TFF kwanini wameliita FA Cup?

FA nijuavyo ni Football Association.

Kwanini wasiliite FF Cup?

Tanzania ni Football Federation,

FF ndiyo sahihi.

Bibie nimekupenda bure kwa kuwakwako kwenye Michezo, Hata hivyo kuna point unaikosa hapa.

Kwasasa kombe hili linaitwa KOMBE LA SHIRIKISHO LA MIGUU TANZANIA. yaani TANZANIA FOOTBALL FEDERATION CUP.

Hapo awali ndio lilikuwa likiitwa FA cup kwakuwa TFF hapo awali ilikuwa ikijiita TFA (Tanzania Football Association)

Najua humkubali Malinzi, ila mpongeze kwa hili. Halafu hivi we ni Fan wa club gani hapa nchini? Hop isijekuwa Yanga kwasababu ya rangi ya jezi wanayovaa?

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom