Kupitia ukurasa wake Mtandao wa Instagram Jemedari Said amechapisha:
"TFF imewaruhusu wachezaji 4 wa YANGA SC walioko kambini Morocco na Taifa Stars kurudi Dar es Salaam ili wajiunge na Kambi ya timu yao inayojiandaa na mchezo dhidi ya Simba SC hapo tarehe 10.10.2026. Yanga SC waliomba wachezaji wao hao waruhusiwe baada ya mchezo na Madagascar na TFF imewaruhusu, huku kukiwa na michezo 2 imebaki kipindi hiki cha FIFA Dates.
Wachezaji hao Mudathiri Yahya, Ibrahim Hamad Bacca, Seleman Mwalimu na Mohamed Hussein walipaswa kuondoka kambini tarehe 2.10.2026 saa 1:00 asubuhi, lakini sasa wataondoka baada ya mchezo kati ya Stars na FAR RABAT utakaochezwa jioni ya leo.
Kocha wa Stars Miguel Gamond amepinga vikali kitendo hicho cha TFF kuruhusu wachezaji wa Yanga na akafikia hatua ya kutaka kujiondoa kama sio busara kubwa kutoka kwa viongozi walioko na timu. Gamondi analalamikia wachezaji kuondoshwa Stars wakati akiwahitaji kufanya nao mazoezi ikizingatiwa hajapata nafasi ya kutosha kukaa na timu tangu baada ya Machi mwaka huu, mwezi Juni alikaa nao kidogo sana kambi ikavunjwa wakiwa Morocco kwa sababu za Ebola.
Kocha anahoji kwanini wakati huu wa FIFA Dates bado hapewi nafasi ya kutosha kukaa na wachezaji wake wote na kuelekeza mbinu muhimu kuelekea AFCON 2027? Kwanini hakushirikishwa kufikia maamuzi ya kuwaruhusu? Kwanini wachezaji wa timu moja tu, Azam wanacheza tarehe 8, wachezaji wao wapo kambini, Singida wanacheza tarehe 9, wachezaji wapo kambini, Simba wanacheza na Yanga hiyo tarehe 10, wachezaji wapo kambini?
Amewauliza TFF wanapeleka ujumbe gani kwa Watanzania, kwamba yeye Kocha ni Yanga sana kiasi ameamua kuachia wachezaji wa klabu hiyo aliyowahi kuitumikia ili wajiandae vya kutosha kupambana na mahasimu wao Simba SC? Program za maandalizi ya Stars za Kocha sio muhimu sana kulinganisha na mechi ya Simba na Yanga?
Kuna vitu vingine unajitahidi kuvumilia lakini unaona havivumiliki, kama mechi ya leo na ile ya tarehe 5 Oktaba dhidi ya Morocco sio muhimu si kambi ivunjwe kila timu ibebe wachezaji wake kama ilivyokuwa mwezi Juni wajiandae na Ligi tu."