TFF Yatangaza Uchaguzi Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Novemba 29, 2025

TFF Yatangaza Uchaguzi Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Novemba 29, 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utafanyika Novemba 29, 2025, jijini Dar es Salaam.

Nafasi zinazogombewa ni pamoja na: Mwenyekiti mmoja, Makamu Mwenyekiti mmoja, wajumbe watatu kutoka Klabu za Ligi Kuu ya NBC, wajumbe wawili kutoka Klabu za NBC Championship, na mjumbe mmoja kutoka Klabu za First League.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, gharama za kuchukua fomu kwa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni Shilingi 200,000, huku fomu za wagombea wajumbe wa Kamati ya Uongozi zikiwa Shilingi 100,000. Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF na kwenye tovuti yake kuanzia Oktoba 2 hadi Oktoba 6, 2025.

Malipo ya fomu yanapaswa kufanywa kupitia akaunti ya TFF TZ Premier League katika Benki ya CRDB, na wagombea wanatakiwa kurejesha fomu zao wakiwa wameambatanisha risiti ya malipo (Pay-in Slip).
1759304410196.png
 
Safari hii wapiga kura chagueni watu wa kusimamia mpira kwa haki, na pasipo upendeleo, au kushikiliwa masikio na wanasiasa.
 
Back
Top Bottom