Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Soma: Baada ya mechi ya Tabora na Yanga kukaribia TFF waufungia Uwanja waAlly Hasani Mwinyi uliokua unatumiwa na Tabora United
Uwanja huo ulifungiwa awali kutokana na miundombinu yake kutokuwa katika hali inayoruhusu kutumika, kama ilivyoainishwa katika masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu. Hata hivyo, baada ya kufanyiwa ukaguzi na kuthibitishwa kuwa marekebisho yaliyoelekezwa yamekamilika, TFF imeurudisha rasmi kwenye matumizi ya mashindano.
Katika taarifa yake, TFF imezikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja hivyo, hasa kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja vyao. Shirikisho hilo limeeleza kuwa viwanja bora vina mchango mkubwa katika kuongeza ushindani na thamani ya Ligi.