TFF yaufungulia Uwanja wa Tabora United (Ali Hassan Mwinyi) kwa michezo ya Ligi baada ya Marekebisho

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Soma: Baada ya mechi ya Tabora na Yanga kukaribia TFF waufungia Uwanja waAlly Hasani Mwinyi uliokua unatumiwa na Tabora United

Uwanja huo ulifungiwa awali kutokana na miundombinu yake kutokuwa katika hali inayoruhusu kutumika, kama ilivyoainishwa katika masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu. Hata hivyo, baada ya kufanyiwa ukaguzi na kuthibitishwa kuwa marekebisho yaliyoelekezwa yamekamilika, TFF imeurudisha rasmi kwenye matumizi ya mashindano.

Your browser is not able to display this video.

Katika taarifa yake, TFF imezikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja hivyo, hasa kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja vyao. Shirikisho hilo limeeleza kuwa viwanja bora vina mchango mkubwa katika kuongeza ushindani na thamani ya Ligi.

 
Wafanye tu wanavyotaka timu yao pendwa isile kichapo nje ndani
 
Kuna timu itachezea si chini ya goli tano apo Tabora.
 
🤣🤣
Yanga tumebaki yatima TFF inapambana kwa kila njia kumbeba kolo, ushahidi wa kimazingira unaonesha dhahiri😀😀
 
Taarifa mbaya kwetu Utopolo.
Siyo taarifa mbaya kwenu nyinyi mliotokwa na mapovu kipindi kile eti kwa nini huo uwanja ulifungiwa kabla ya mechi dhidi ya Yanga!! Aibu imekuwa upande wenu bila shaka.

Mliambie hilo tawi lenu likamie kama kawaida yake pale linapocheza na Yanga, halafu tuone kama litaepukana na kichapo cha mbwa mwizi.
 
Vp mbona kama wasiwasi umekujaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…