Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Shirikisho la soka nchini TFF kupitia Kamati ya Maadili, limewafungia Mwenyekiti wa matawi ya klabu ya Yanga, Bakili Makele na Katibu wa matawi ya klabu hiyo Boaz Ikupilika kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitatu kwa kukaidi maamuzi ya Serikali na Shirikisho hilo.
Maamuzi hayo yametolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Hamidu Mbwezeleni katika mkutano na wanahabari uliofanyika katika ofisi za Shirikisho hilo Ilala jijini Dar es salaam.
Viongozi hao wanadaiwa kupinga maagizo ya Serikali na TFF ya kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ambazo ziko wazi ndani ya klabu ya Yanga.
Pamoja na adhabu hiyo waliopewa, pia wanatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni mbili kwa kila mmoja.
Hivi karibuni Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka ya TFF kupitia Mwenyekiti wake Malangwe Mchungahela ilitangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu ya Yanga ambayo ni Januari 13, 2019 na kuagiza klabu hiyo kuanza mchakato wa kutoa fomu za wagombea mara moja.
Nafasi zinazogombewa katika klabu hiyo ni nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.