TFF zingatieni usalama wa wachezaji

TFF zingatieni usalama wa wachezaji

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Jana baada ya game ya Yanga kwisha na Yanga kupoteza mchezo kwa Ujumla ya goli 1,Kuna kitendo kilichotokea ambacho sio kizuri.

Baada ya mwamuzi wa mchezo ule kupuliza kipenga cha mwsho kuashiria mchezo umekwisha Ghafla MASHABIKI WAKAANZA KUINGIA ENEO LA KUCHEZEA MPIRA hata kabla wachezaji hawajatoka.

Kitendo hicho sio kizuri kwani kinahatarisha usalama wa wachezaji huezi jua lengo la washabiki ni nini na pia wamebeba nini.

Hali hii imekua ikitokea sana hasa viwanja vya mikoani sana sana timu mwenyeji inaposhinda.

Mwisho naishauri Tff kuzingatia suala la usalama wa wachezaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi Viwanjani na mashabiki kupewa Elimu juu ya ivyo vitendo.
 
Hongereni Tff jana baada ya game ya Azam sijaona hali ile ikijirudia badala yake police ndo walikua wakwanza kuingia kiwanjani...hongeni kwa hilo
 
TFF zingatieni usalama was Shiza Kichuya.. amekua akikwatuliwa sana siku hizi.. alafu marefa kama hawaoni vile.
Nakala; Jamal Malinzi
 
Back
Top Bottom