Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Pia soma ~ Serikali iingilie kati haraka, kuna Mawakala wanaopandisha bei ya mbolea kiholela
Akizungumza ofisini kwake, Meneja wa TFRA Kanda ya Ziwa, Michael Sanga, amesema wafanyabiashara hao walikamatwa baada ya maafisa wa mamlaka hiyo kufanya operesheni maalumu ya mtego iliyofanikisha kuwabaini wakiuza mbolea hizo kwa bei isiyo rasmi.
Aidha, amewatahadharisha wafanyabiashara wote wa pembejeo za kilimo kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia biashara ya mbolea, huku akiwahimiza wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini ukiukwaji wa bei elekezi au changamoto nyingine zinazohusu upatikanaji wa mbolea za ruzuku.
TFRA imesisitiza kuwa haitamvumilia mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu wa uuzaji wa mbolea za ruzuku, ikieleza kuwa ushirikiano wa wananchi katika kutoa taarifa utasaidia kuhakikisha ruzuku ya Serikali inanufaisha wakulima waliokusudiwa na kuongeza tija katika sekta ya kilimo.
Pia soma
~ Kupanda kwa mbolea ya ruzuku
~ Mbona bei ya mbolea inazidi kupanda kila siku huku Dakawa?
~ Wizara ya Kilimo tuambieni wakulima kuwa Tanzania hakuna mbolea tujue moja ila sio kwa mateso haya