TFS safisheni madudu ya Vikindu ecological Garden ni aibu

TFS safisheni madudu ya Vikindu ecological Garden ni aibu

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,943
Reaction score
1,015
Kwa waliowahi kutembelea Vikindu Ecologial garden watakuwa wamewahi kukutana na ujinga fulani wa wafanyakazi wa pale. Unapokuwa mkimya basi wao wanadhani wamekupata kwelikweli na hudhani wanajua mengi. Inasikitisha kuwa hawawezi kusoma uso wa mtu au hata namna anavyouliza maswali kujua kuwa huyu mtu ni anaufahamu mkubwa.

Ukiingia getini, wanakupa taarifa ya kiingilio na na charges nyingine ikiwa pamoja na kuwa garden guider na camera. Kwao hata kama utatembea bila garden guider, lazima ulipie charges zake (10000/=), ukiwa na camera lazima uilipie (hata kama ina megapixel 13) utalipia na simu (yenye megapixel 64) haulipii. Watakwambia lipa, tunaandaa control number ukitoka kwenye matembezi huko utapitia kuchukua risiti yako.
Utakapotoka kwenye matembezi, utaambiwa mtandao unasumbua tumeshindwa kuitengeneza, wewe nenda, kwakuwa tunanamba yako ya simu utaupata ujumbe tukiisha kukulipia.
Sahau, kimeshakwenda kwa mganga hicho.

Mchezo huu uko sana siku za weekend (maana nimekwenda hapo mara nyingi) kuliko siku za kawaida.

Ukitembelea huko ndani, uwezo wa kimajukumu nikimaanisha uelewa wa masuala ya ecological reservations wa garden guiders na historia ya Vikindu garden ni wa chini. Hawakupi hamu kwa mtu ambaye si hobby yako kutembelea maeneo kama hayo kurudi tena siku nyingine. Na kuna sehemu unagundua kabisa hapa nadanganywa, unauchuna kinamna. (ukienda na wale rastafarians kule ziwa Ngosi Mbeya, lazima utake kurudi tena pamoja na kwamba ziwa liko mbali na barabara kuu ya Uyole - Malawi, kuliko hawa ambao barabara ya Kilwa inapita mbele yao).
 
Back
Top Bottom