Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

MBIO ZA UTORO ZA THABO BESTER ZAISHIA SAKAFUNI TANZANIA

Waziri Ronald Ozzy Lamola wa wizara ya katiba na vyuo vya mafunzo (magereza) Afrika ya Kusini athiibithisha kukamatwa Thabo Bester nchini Tanzania na tayari mipango ya mchakato wa kisheria ili Thabo Bester awe deported kurudishwa Tanzania imeanza.

Thabo Bester akiwa na mpenzi wake wa kike Dr Nandipha Magudumana pamoja na raia mwingine wa Mozambique wamekamatwa mkoani Arusha wakiwa na hati kadhaa za kusafiria amesema Mh. Bheki Cele waziri wa Polisi wa Afrika ya Kusini.

Mbali ya kutoroka toka jela moja yenye ulinzi mkali Afrika ya Kusini alikokuwa akitumikia kesi za mauaji na ubakaji Thabo Bester pia alikuwa anaendesha biashara za kitapeli za udalali wa majumba na magari ya kifahari kwa kushirikiana girlfriend wake Dr Nandipha Magudumana.


Picha : Jela ya ulinzi mkali ya Mangaung ya Bloemfontein Afrika ya Kusini alipotoroka Thabo Bester mwaka 2022.

Dr. Nandipha Magudumana aliweza wakati mmoja kufanikisha Thabo Bester kuongea kupitia mtandao wa Zoom akiwa ktk chumba cha ulinzi wa juu jela na mkurugenzi wa kampuni moja iliyopo jijini New York Marekani inayomilikiwa na bilionea Tom Motsepe.

Mkurugezi huyo alichukua hatua za tahadhari na kuomba huduma za makachero binafsi / private detective kuweza kumchunguza mtu aliyeongea naye ni nani ktk zoom ndipo alipobaini anaongea na mhalifu aliye jela nchini Afrika ya Kusini akitumikia kifungo kirefu hivyo mkurugenzi huyo kuachana naye mazungumzo ya biashara alizokuwa akizinadi pengine kwa uhakika zingekuwa haramu na za kitapeli....

Dr. Nandipha Magudumana ni msichana msomi wa elimu ya juu, ana digrii mbili za fani ya utabibu na sayansi ya Afya ambazo ni Bachelor of Health Sciences (BHSc) in Biomedical Sciences na Bachelor of Medicine and Bachelor of Surgery (MBChB), toka chuo kikuu tajwa cha University of the Witwatersrand, Johannesburg almaaruf Wits cha nchini Afrika ya Kusini.

Baada ya unaosemekana mwili wa Thabo Bester kugundulika ukiwa umeungua vibaya kiasi cha kutotambulika kati selo ya jela maarufu yenye ulinzi mkali huko Bloemfontein nchini Afrika ya Kusini, Dr. Nandipha Magudumana alitayarisha ombi la affidavit la kupewa mwili wa aliyekuwa mpenzi wake ili ukafanyiwe maziko Soweto.

Lakini katika hali ya kushangaza baadaye Thabo Bester alionekana akiwa ameongozana na Dr. Nandipha Magudumana wakifanya shopping ktk supermarket moja karibu na walipopana jumba la kifahari la kodi mbaya lililopo Sandton mitaa ya matajiri kilometa moja toka makazi ya Rais Cyril Ramaphosa, na ndipo uchunguzi kuhusu 'kifo' cha Thabo Bester ulipoanza tena.


Picha : Jumba la kifahari alilokodisha tapeli Dr. Nandipha Magudumana kupata muonekano wa kufanikisha madili ya kutapeli ya udalali wa magari na majumba ya kifahari


Uchunguzi huo kwa kutumia picha za CCTV zilizowachukua wapenzi hao supermarket na pia kutaka kufahamu kwa kina vinasaba DNA vya mwili ulio uliungua vibaya jela ulikuwa ni wa nani, ulifikaje vipi ktk selo ya jela na kuzua taharuki kuwa jambazi sugu Thabo Bester ametoroka jela akiwa hai .. hatimaye wapenzi hao wawili katika uhalifu na wakiongozana na jamaa mmoja Zakaria Alberto raia wa Mozambique kunaswa nchini Tanzania.

Thabo Bester | Lamola says Bester and Magudumana were arrested in Tanzania on Friday night

 
Majeshi yetu hapa TZ yanafanyakazi nzuri na kubwa sana ila kuna wajinga fulani hapa TZ huwa wanayabeza sana. Sasa wasikilize SA wanavyowasifia.
 
Majeshi yetu hapa TZ yanafayakazi nzuri na kubwa sana ila kuna wajinga fulani hapa TZ huwa wanayabeza sana. Sasa wasikilize SA wanavyowasifia.
Unaweza kuwa uko sahihi lakini sema issue kama hii wanashirikiana na INTERPOL ndiyo maana hawana budi kuwajibika!!!!!! ila bado tuna kazi kubwa kuboresha weledi wa TANPOL kufikia japo 50%
 
In short, amekua convict wa pili kuweza ku escape from maximum security prison in SA,na jinsi alivyo escape ni kama movie from Mars, kwanza tuthibitishe hili kuwa amekamatwa hapo A town
Aisee..
 
Unaweza kuwa uko sahihi lakini sema issue kama hii wanashirikiana na INTERPOL ndiyo maana hawana budi kuwajibika!!!!!! ila bado tuna kazi kubwa kuboresha weledi wa TANPOL kufikia japo 50%
Kwani INTERPOL ndio wamekuja kukamata!!? Wakati mwingine tuwapongeze wakifanya vizuri. Nenda Youtube ukaone wa South wanavyopongeza TANPOL.
 
Sorry,nilishindwa kuweka mwendelezo na pia kujibu maswali kadhaa kutokana na kubanwa na shughuli nyingine,wa South wanasema ni bora bester afungwe hukohuko tanzania kwani hawaiamini SAPS kabisa,wana mashaka kuwa anaweza kutoroshwa tena kutoka gerezani huko SA, kuna jambo nililiona tokea habari za bester kuonekana akiwa na Dr Nandipha kwenye supermarket,huku ikiaminika kuwa alishafariki kwa kujichoma moto akiwa gerezani na baadaye akafanyiwa cremation rasmi, thabo bester na Nandipha walikuwa ni wapenzi zamani,lakini waliachana muda mrefu kabla ya bester kuhukumiwa,inasemekana Dr Nandipha alikuwa akimpenda sana jambazi bester, hivyo aliposikia kuwa bester amehukumiwa altona ndiyo gap la kurudisha penzi Lao kwa gharama yoyote,ndipo alipoanza kusuka mipango ya kumtoa bester gerezani,so plan yote ya kumchomoa bester gerezani aliisuka Nandipha,hadi kuwahonga askari wa G4s waliokuwa wanaendesha gereza hilo,kununua maiti waliyoichoma moto wakidai ni ya bester, akagharimia kila kitu ikiwemo nyumba,gari,na expenses zote zitakazomfanya bester kuufurahia uhuru huo bandia,na hata baada ya picha za bester kusambaa akiwa kwenye Mall na nyingine ikimuonyesha akiwa nje ya duka jingine kubwa kusambaa,Nandipha alimhamishia bester kwenye nyumba ya kifahari aliyoipanga kwenye eneo la brooklyn huko Pretoria,baadaye tetesi zikachomoza kuhusu uwepo wa bester kwenye eneo hilo,mwandishi wa habari za kiuchunguzi aitwaye Barry roux ndiye aliyetoa hint kuhusu besters whereabouts, hivyo Dr Nandipha akalazimika kumhamisha tena bester na kumpeleka sehemu isiyojulikana!! Hadi walipokamatwa huko arusha usiku wa jana wakiwa na mtu mwingine ambaye ametambulika kama raia wa Mozambique, pia polisi wa arusha wanasema kuna mtuhumiwa mwingine mmoja ambaye alikuwa pamoja na bester ila bado hajakamatwa, hayo ndiyo mapenzi! Kuna mtu hapo juu aliuliza jinsi ambavyo bester alifanikisha uhalifu wake,bester anajulikana kama Facebook rapist!! Sababu ni hii,bester alikuwa akitumia mtandao wa Facebook kuweka matangazo ya nafasi za ajira nzuri nzuri,alikuwa akiweka na address za kuweza kuwasiliana naye ikiwa utavutiwa na ajira alizotangaza,sasa ukiwasiliana naye anakupa location ya kwenda kwa ajili ya interview na mengineyo,huku akiahidi kuwa gharama za usafiri na malazi utarudishiwa ukishafika kituoni,hapo ndipo watu walijichomeka bila kujua! Kwani baada ya kufika ulikoelekezwa ungepokelewa na bester mwenyewe,atakuonyesha sehemu ya kufikia na kula na kila kitu,sasa hapo ndipo atakuja kukupa interview, atakubaka,atakupora kila kitu,na kama Huna bahati anakuua kabisa!! Umeelewa sasa? Swali ni kuwa Dr Nandipha aliipata wapi maiti aliyoichoma kwa jina la bester? Maskini Dr Nandipha ndiyo ameshaharibu career yake kwa ajili ya mapenzi ya jambazi,muuaji na mbakaji bester, umeona kitu hapo?
 
Kwani INTERPOL ndio wamekuja kukamata!!? Wakati mwingine tuwapongeze wakifanya vizuri. Nenda Youtube ukaone wa South wanavyopongeza TANPOL.
Mkuu,SAPS ni takataka kabisaa,huwezi kuofananisha na @tanpol kwa namna yoyote,SAPS ni kitengo cha majizi tu,juzi hapo wamekamatwa wakihusishwa na utekaji wa magari ya kusafirisha fedha CIT,polisi wa South ni certified criminal,angalau bongo kuna polisi wanajali kidogo,ila sio hawa wa south
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…