Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

Kwa sababu taasisi zao ziko corrupt

Ova
Basi Kama kweli Serekali ya South inamtaka Mfungwa wao,bas na sisi watukamatie lile jizi alilosema Mama kua limekopa pesa kibao kwenye Bank zetu 5 na likakimbilia huko South,ili tubadilishane nao na hakuna kuwapa Mfungwa wao bure, au watulipe kwa hiyo kazi iliowashinda wao sisi tumeiweza!!
 
Gupta family ya huko S/Africa unaifahamu?
 
Ila mambo mengine bwana basi tu nchi ya south Africa raia wake Wana shida nadhani ni mental problem Kuna vitu vinafanyika kweny ile nchi mpaka unabakia unashangaaa yani, Sasa ndo wamekuja kudakiwa bongo land wao walijuwa wako salama
Yawezekana, hata mimi huwa naona kila mkazi wa Dar hayuko sawa kiakili, sijui ni jua lile.
 
Huyo jamaa alizaliwa baada ya mama yake kubakwa akiwa na miaka 17. Hajwahi kumjua baba yake ni nani. Mama mtu alimtelekeza kwa bibi akiwa mdogo. Jamaa naye alibakwa mara nyingi utotoni na ukubwani.
 
Hii hollywood lazima waiweke kwenye filamu
 
Bongo Muvi wangekuwa na jicho la kuona mbali, wangechangamkia hii kesi kwa kutengeneza muvi kali na ya kusisimua sana kuhusiana na hili sakata la Dokta na jamaa yake mbakaji.

Muhimu tu polisi na magereza, watoe ushirikiano kwenye ishu ya majengo yao, na pia kutoa wataalam wa kusaidia hiyo muvi.

Ila kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena! Muda huu watakuwa wanasubiria tu 2025 ifike, ili watumiwe na ccm kwenye kampeni za uchaguzi mkuu kwa malipo kiduchu.
 
Wanapenda sana kufanya hivyo ila tatizo linarudi kwa Watanzania. Watatumia pesa ndefu mpaka kukamilisha movie nzuri ila walaji ndio nyie mnaenda 'kuchoma' na kuuziana kwa 1,500 movie nzima.
 
Wanapenda sana kufanya hivyo ila tatizo linarudi kwa Watanzania. Watatumia pesa ndefu mpaka kukamilisha movie nzuri ila walaji ndio nyie mnaenda 'kuchoma' na kuuziana kwa 1,500 movie nzima.
Siku hizi teknolojia imebadilika. Na wenyewe wanatakiwa kuingia huko.
 
Hapa nimegundua mambo kadhaa kwamba:-

1. Huyu mwanamke ambaye ni Doctor ndiyo mtu mwenye akili nyingi kuliko huyu mhalifu

2. Mwanamke huyu anafanya haya Kwa sababu tu anampenda jamaa, lakini pia ana tamaa na maisha mazuri ya kutumia akili bila kujitesa na kazi kwa mafanikio ya muda mrefu, Nigerian style

3. Walifanya kosa kubwa sana baada ya mpango wao kutimia, mhalifu alitakiwa kua mafichoni zaidi ya miaka mitano mpaka kumi ndiyo atoke nje ya nchi , kwa tamaa zao wakawahi kutumia pesa na starehe ambazo zimewaponza

4. Huyu mwanamke atatumikia kifungo ambacho ni cha wakati fulani na atakuja kutoka kwa sababu yeye si mhalifu halisi isipokua muwezeshi, ila huyu jamaa yake yamkini akifika huko S.A akapotezwa mazima.

5. Iko hatari kubwa ya ajira kwa mkuu wa gereza na maafisa wa zamu wa siku ambayo mhalifu alitoroka
 
Pamoja na hawa fugitives kukamatiwa hapa nchini, ni muhimu mno sheria zetu zikafuatwa, tusi just roll over ili kuwafurahisha SA, kwanza wajibu ilikuaje waukesha mpaka wao bila wahusika kujua, Mr.Bester ndiye pekee aliyehukumiwa, Dr.Nandipa na Mozambique citizen hawa ni illegal immigrants, wapelekwe mahakama na sheria ichukue mkondo wake, kuwa deport SA straight haitakua sawa
 
Sawa ila hiyo no 4 sio sahihi, Dr.Nandipa ni illegal immigrant kama wengine, ni LAZIMA ahukumiwe kwa sheria zetu za uhamiaji, Tanzania iheshimu sheria zake
 
Ukichunguza vizuri unaona Baster ni kama ni mtu kichaa
 
Sawa ila hiyo no 4 sio sahihi, Dr.Nandipa ni illegal immigrant kama wengine, ni LAZIMA ahukumiwe kwa sheria zetu za uhamiaji, Tanzania iheshimu sheria zake
Wala hahukumiwi hapa huyo, hao ni wahalifu ambao Serikali ya S. A itatuma maafisa wa usalama kuwafata na kurejeshwa kwao, hakuna hukumu yoyote wala kesi watakutana nayo hapa kwetu
 
Wala hahukumiwi hapa huyo, hao ni wahalifu ambao Serikali ya S. A itatuma maafisa wa usalama kuwafata na kurejeshwa kwao, hakuna hukumu yoyote wala kesi watakutana nayo hapa kwetu
Why mkuu ?,huyu raia wa Mozambique na Dr. Nandipa kosa lao hapa ni kuingia nchini kwa njia za panya, kama wasomali/Ethiopians wanavyofanya, sasa why hawa wawe tofauti?,SA lazima waheshimu sheria zetu na elewa hawa wawili hawana cases kule SA, but Mr. Bester ni tofauti maana yupo convicted kwa rapes na murder
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…