Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

CB1C4009-DB3B-4408-A4A1-3B35BDB59BE8.png


Jeshi la polisi Tanzania limewakamata mbakaji maarufu wa Afrika Kusini, Thabo
Bester, na mpenzi wake Dokta Nandipa Magudumana.

Stori ikoje?

2000s Thabo Bester alikuwa anabaka, kupora vitu, na kuwauwa wanawake ambao alikuwa anawatongoza kupitia mitandao ya kijamii. Alikua anaangalia wenye magari na vitu vya thamani.

2012 akafungwa miaka 50 gerezani.

2013 Nandipha ambaye ni daktari wa watoto aliolewa na bwana Oscar Magudumana na wakazaa watoto wawili. Wakatengana bila kupeana talaka; wakati huo dokta alikuwa kashazama penzini na mhuni Bester anayeny** debe gerezani. Yaani walianza mahusiano akiwa bado kwenye ndoa.

Kulingana na ripoti, Bester alikuwa akiwasiliana na Dk Nandipha akiwa bado gerezani. Mrembo akasuka mpango wa kutafuta mahali pa kujificha akitoroka gerezani.

2020, Septemba, Mrembo huyo alikodi nyumba kupitia kampuni ya 4Tune Property Smiths; mkataba ukawa na majina yake na mumewe Bester (ila jina likaandikwa lingine na kazi ikawa ni mtaalamu anayefanya kazi ulaya). Kodi ilikuwa ni Tshs Milioni 5 kwa mwezi (R 4000).

2021 Mei, Kakake Dk. Nandipha, Nkosinathi Sekeleni, alimtuhumu kwa kumsaliti mumewe na kulala na mbakaji Bester. akamtuhumu pia kuwa anatakatisha fedha za Bester kupitia kampuni yake ya Optimum Medical Solutions. Dokta akafungua kesi mahakamani ya kuharibiwa jina na kutishiwa kuuwawa na kaka yake.

2022, Mei, ulitokea moto gerezani na Bester akajumuishwa kuwa mmoja ya waliochomwa vibaya na kufariki.

Dokta Nandipha alienda kudai mabaki ya Bester ayazike akiwa kama "mke wake wa sheria ya kimila".

2022, Juni, kuna watu waliwatonya Polisi Afrika Kusini kuwa mfungwa aliyedhaniwa kuwa amefia kwenye moto gerezani yuko anafanya shopping ya nguo akiwa na dokta Nandipha. Msako ndio ukaanza.

2022, Mwishoni, Nandipa alinunua gari la kifahari la Tshs milioni 170 na akaliendesha mpaka mpaka wa Zimbabwe kisha akalitelekeza huko.

2023, Aprili, Thabo Bester, Dokta Nandipa Magudumana pamoja na mwingine ambaye inasemekana ni mfanyakazi wa dokta wakakamatwa Tanzania wakitoroka.
------------
Mapenzi.

 
Dah!,watu wanatumia hela

Na hapo ni kupiga mbupu tu na demu hapati mimba sio hawa wa kwetu vizazi vyao vipo karibu kama panya,wiki moja tu mimba hata hamjafaidi kulana
Demu fight huyo, sio hawa matapeli wetu kila kukicha invoice kwenye majangaaa anakula hivi au hata anakuletea msala
 
Back
Top Bottom