Bachelor ll
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 4,106
- 6,678
Sawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Angekuja urambo ningempora demu wakeKweli huyu ange enda Urambo, nani angemkamata?
Jamaa alikosea kwenda arusha , Arusha ni mji wenye wageni wengi so ukaguzi wake kwa wageni ni intesive tofaut na miji mingine akijificha Mwanza huko angetoboa ,Thabo Bester aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba na mamlaka za afrika ya kusini amekamatwa leo asubuhi huko mkoani Arusha, Bester maarufu kama Facebook rapist anatuhumiwa kwa makosa kadhaa yakiwemo ubakaji,utapeli na mauaji,
Kabla ya kukamatiwa Tanzania, Bester alikuwa akitumikia kifungo jela ya Mangaung huko nchini Afrika Kusini ambapo iliripotiwa kuwa Bester alifariki akiwa gerezani, na ndipo dada mmoja daktari aitwaye Nandipha Magudumana alijitokeza kuomba kupewa mwili wa Bester ili akauzike akidai kuwa ni mke wa Thabo Bester, ambapo alikubaliwa na kuuchukua mwili kutoka kwenye hospitali ya Mangaung na kwenda kuuchoma siku hiyo hiyo.
Lakini siku kadhaa baadae camera za usalama kwenye mall moja hukohuko SA zilimwonesha mtu anayefanana na Bester akiwa na ndevu nyingi na kujitanda kiajemi, ndipo tetesi za kuwa Bester yupo hai zilipozagaa na kuishtua polisi ya SA (SAPS)na kuanzisha msako mkali
------
View attachment 2594086
Thabo Bester na Dkt. Nandipha Magudumana
Ijumaa ya tarehe 7 April 2023, umma wa watumiaji wa mitandao ya kijamii kutokea Afrika Kusini na Tanzania kiupekee na duniani kwa ujumla waliimba wimbo moja unaofanana. Hii ni baada ya kutapakaa kwa habari juu ya kukamatwa kwa mfungwa mtoro maarufu kama mbakaji wa Facebook. Hapa tunamuongelea Thabo Bester kijana wa miaka 35 mwenye mama aitwaye Maria Mabaso.
Details of his father are not well known, lakini mtoto huyu alilelewa na mama yake mpaka alipotimiza umri wa mwaka mmoja tu na mama yake akaenda kumtelekeza kwa mama yake (Bibi wa Thabo). Mtoto huyu alilelewa katika mazingira ya dhiki kubwa bila kumjua mama yale ambaye alipotelea kusikojulikana.
In a nutshell, ni kwamba bibi huyu alifariki na kumwacha mjukuu wake akirandaranda pasipo na makazi na mwisho kujikuta katika matukio ya ukatili mwingi hadi kumpelekea kubakwa kinyume na maumbile akiwa mdogo.
Nyamela huyu ambaye alishajiingiza kwenye uhalifu wa kimtandao, mwaka 2009 alifungwa kifungo cha miezi 6 kwa kisa la flaud ambapo wakati anatumikia kifungo hicho alilalamika kuingiliwa kinyume na maumbike na watu zaidi ya mmoja(Gang raped)
Mwaka 2011 ndipo akapata mashtaka makubwa ya kubaka wanawake wawili na wizi wa maungoni pamoja na kumuua mwanamke Nomfundo Tyhulu. Hawa wanawake wote ni wakiokuwa na ndoto ya kuwa wanamtindo ambao aliwarubuni kupitia mtandao wa Facebook kuwa atatimiza ndoto zao.
Katika kesi hii Thabo alihukumiwa kifungo cha maisha. Ingawa katika utetezi wake Thabo alijitetea kuwa makosa yake yanahusiana na maisha aliyopitia. Jaji alidai Mahakama haiwezi kuwa lenient kwa mtu ambaye alimpiga mwanamke(Nomfundo Tyhulu) hadi kusababisha kifo chake. Thabo akala umeme wa kifungo cha maisha.
This meant Thabo would spend the rest of his life eating semi-cooked beans for a thing that only a soap would suffice.
Alitumikia kifungo chake kwa miaka zaidi ya 9. Ndipo katika mazingira yasiyojulikana akajikuta anajuana na daktari Nandipha Magudumana. Hawakukutana kwa bahati mbaya. Walishajuana tangu mwaka 2006 miaka ikiwa ni miaka mitano kabla ya kifungo cha pili cha Thabo.
Ni kwamba mwaka 2006 Dkt. Nandipha akiwa bado ni mwanafunzi wa chuo cha udaktari cha Wits, Thabo alikuwa anaendesha kampuni ya kuwapromote wanamitindo na Dkt. Nandipha akiwa ni mmoja wa wanamitindo wa kampuni ile. Kazi zilienda vizuri mpaka mwaka 2011 Thabo alipofungwa hivyo wakapoteza mawasiliano.
Mwaka 2013, Dkt. Nandipha akamaliza chuo akiwa mahili kwenye mambo ya Aesetics. Taaluma hii ilikuja kufanya kazi kubwa kumnasua Thabo kifungoni. Mwaka huo huo Daktari huyu akaolewa na Dkt. Mkhuseli Magudumana
Kwa mwaka mmoja tangu mwaka 2014 mpaka 2015 daktari huyu akawa anafanya kazi katika hospitali ya Edenvale nchini Afrika kusini. Mwaka 2016 akahamia hospitali ya Far East Rand kisha akafungua facility yake iitwayo Optimum Medical Solution
Ni katika mwaka huohuo akaanza kumtembelea Thabo akiwa jela akitumikia kifungi chake cha maisha. Mwaka 2020 kwenye hati ya kiapo (affidavit) akatamka kwamba ni mchumba wa Thabo.
Mwaka 2021 chama chama cha madaktari Afrika Kusini kikamzuia Nandipha kufanya kazi za udaktari kwa kuwa hakuhuisha leseni yake. Pia mwaka huo, akafungua kampuni ya kukarabati nyumba kwa msaada wa Thabo iliyotwa Arum properties.
Then came the drama, May 3, 2022, 0325HRS Thabo akiwa kifungoni katika gereza la Mangaungaung akadanganya kuwa amejiua kwa moto akiwa katika chumba chake. Saa tatu na dakika 25 asubuhi Thabo akadanganya mamlaka ya Magereza kuwa amekufa kwa kujichoma moto. Yes! He set himself ablaze!
Mpango huu ulifanywa kisayansi kwa kuwatumia walinzi wa jela pamoja na kampuni ya ulinzi ya G4S waliokuwa na tenda ya ulinzi katika gereza lile.
Siku tatu baadae yaani tarehe 6 May 2023 akaenda kuchukua mwili ule katika mortuary kama mke wa marehemu lakini baadaye akanyang’anywa mwili ule.
Taarifa juu ya kifo cha Thabo akiwa jela zikazaa kelele kutoka mashirika ya kutetea haki za wanawake wengi wakipiga kelele kuwa wamemuona katika maduka ya Sundtown akivinjari pamoja na mrembo Nandipha. Baadae taarifa zikadokeza kuwa Thabo alifadhili event ya Nandipha ya madaktari ambayo ilifanyikia kwenye mansion yao ha Hyde park
Kelele hizi zikachagizwa na ujumbe ambao kaka wa Nandipha alipost kwenye account yake ya facebook. Kaka huyu aitwaye Nkosinathi Sekeleni aliandika hivi akimuongelea dada yake👇
“Its time to name and shame. Don’t be fooled by her looks and charms. Very evil this girl Dr. Nandipha Sekeleni Magudumana. She is in daily contact with this moster by the name Thabo Bester, Once dubbed the Facebook rapist. This guy is doing life sentence. She even exposes her two little daughters with this monster. In the outside world he goes by the name of TK Nkwana he was sponsor of her event of doctors network. Bester has been laundering money through her business of Optimum Medical Aesetics''
View attachment 2594079
Kwa ufupi ujumbe huu ulimaanisha kuwa
'Watu wasihadaike na muonekano na urembo wa dada yake kwani dada yake anawasiliana kila siku na Thabo mbakaji wa Facebook anayetumikia kifungo cha maisha jela. Kwamba mtu huyu ambaye sasa anatumia jina la TK Nkwana ndiye aliyefadhili event ya madaktari iliyoendeshwa na dada yake. Kwamba Thabo anatakatisha fedha zake akitumia kampuni ya dada yake ya Optimum Medical Aesetics.
Ujumbe huu ukawafungua macho maafisa vipenyo wa South Africa. This forced them to exhume the dead body who was allegedly to be Thabo. Yes! Wakaenda kufukua mwili uliodaiwa kuwa ni wa Thabo ili ufanyiwe upya autopsy
Katika uchunguzi wakabaini kuwa mwili ule ulishakutwa na umauti kabla hata ya kuunguzwa na moto. Hii ni kwa sababu walibaini maiti ile haikuwa imevuta moshi kabla ya kifo kama kweli alikufa na moto. Ugunduzi huu ukawafanya wachukue samples ili wakafanye DNA profiling kwa kumtumia mama wa Bester ambaye alishajitokeza muda mrefu tangu anafungwa.
The results were negative. Then the new Murder case was re-opened in March this year.
The manhunt was as well launched as well to seek the fugitive.
Ni katika wakati huu huu kampuni binafsi ya ulinzi ya FIDELITY ADT ambayo ilikuwa ikifanya kazi bega kwa bega na polisi wa Afrika Kusini wakatoa tangazo lenge dau nono kwenye mtandao wa Facebook.
Nanukuu Tangazo
“Help us to bring this criminal to the book. We are offering R 100,000 to anyone who can provide us with information that leads us to the successful arrest and conviction of Thabo Bester alias Facebook rapist.
Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo bwana Wahl Bartman akawataka watu wenye taarifa zozote juu wa Thabo wasisite kuziwasilisha kwake.
Ni katika muda mfupi toka tangazo hili mwezi June ikavuja cctv footage iliyomwoshesha Dr. Nandipha akiwa na Thabo pamoja na binti yao katika maduka ya Sunsdtown. Habari pia zikaeleza wawili hao wanakaa katika jumba la kifahari la Hyde Park Afrika Kusini.
The information came too late as the duo vacated their mansion at Hyde Park. Ndipo wakaja Darisalama Bongo!
Inaonekana wawili hawa walishindwa kuchanga karata zao vulizuri wakiwa Dar! Tangu wanaingia Rotana hotel vichomi wa kamanda Murilo wakawa wanawachora tu! Timu ya makachero wasio na papara ikaweka kambi hotelini pale ikiwafatilia mienendo yao yote.
Mbaya zaidi walibaini Passport zao hazikuwa zimegongwa mhuri popote kuonyesha kuwa waliingia nchini wakitokea Afrika Kusini.
Hii ina maana maafisa uhamiaji mpakani walikanyaga katiba.
Makachero wakagundua watu wale wapo kwenye company ya mtu mwingine raia wa Msumbiji aitwaye Zakaria Arbeto.
Huyu ndiye aliyekuja pale Hotelini akiitumi gari la Landcruiser nyeusi.
2023, Aprili, Thabo Bester, Dokta Nandipa Magudumana pamoja na Zakaria Arbeto wakakamatwa Tanzania wakiwa kwenye harakati za kutorokea nchini Kenya.
Na Buyobe
Pia soma
Dreva wa Lissu angebaki nchini angeuliwa na watu wa Magufuli. Tumia akili kwenye argument ya Lissu wacha kuchukua majibu mepesi ya Kamanda SirroMr Bester ni mhalifu na tayari alikuwa ashahukumiwa kwa uhalifu wake, hivyo kukamatwa kwake ni halali.
Dereva wa Lisu sio mhalifu, bali ni mtu muhimu alietakiwa ahojiwe ili kumpata mhusika wa tukio hilo la Lisu.
Cha kushangaza mshambuliwaji mwenyewe akiwa ameshikiwa akili na uongozi wa chama chake akaamua kumtorosha dereva huyo ambae angeisaidia polisi kuufahamu ukweli wa shambulio lile.
Polisi sio Mungu ambae ana uwezo wa kujua kila kitu cha sirini na cha dhahiri.
Ili waweze kupata ukweli wa jambo ni lazima kwanza washirikiane na muhusika au shahidi ili kupata taarifa za kuwasaidia kupata chanzo cha jambo husika.
Sasa muhusika unapoamua kumtorosha mtu ambae angeisaidia polisi kupata mwelekeo wa kesi yako, unatarajia nini tena kutoka kwao?
Hapo unakuwa umewakomoa wao au umejikomoa wewe mwenyewe?
Thabo akili nyingi lakini kazitumia kijinaiHuyo Doctor ni Mke wa Mtu, ana watoto 2 na Mume wake, ila alikua anamsaliti Mume wake kwa Kutembea na Msela kabla Msela hajafungwa Jela!
Coz Msela kafungwa 2012, kabla ya hapo walikua Wapenzi tayari, na Doctor akaachana na Mume wake kwa ajiri ya Msela, ila huyo mwana kitambo alikua na Michongo ya kwenda Mbele, anaenda anarudi, akifanya issue za Modeling, akaja kupata pesa nyingi (anajua mwenyewe alikozipata).
So vile alikua anajulikana ni Model na ana connection Ulaya, akawa anawadanganya Wadada kuwafanyia mpango wakawe Model Ulaya, hasa kupitia facebook, na alikua anawalenga wale high class tu, ndo hivyo akawa anawabaka wengine kuwaua, so kuna Mdada mmoja alibakwa akasalimika kuuwa huyo ndo alimfungulia kesi, na hata wakati tukio la moto linatokea, baadye Serikali kutoa taarifa kuwa aliyekufa sio yeye, bado wananchi wengi waliamini ni yeye ndo alikufa!
Doctor keshamfungulia Mashtaka Kaka ake wa kuzaliwa, kwa madai anataka kumdhuru!
Kaka ake aliitisha Mkutano na wana habari akimtuhumu Dada ake kwa kusaliti Ndoa yake, na kwamba anatumika Kuziingiza Pesa chafu za Mhalifu kwenye Mzunguko, ni kama vile Doctor alikua na Access ya pesa za Mwana, coz alianza kununua Nyumba za kifahari kwa bei mbaya!
Mwisho akamtaka Dada ake arudi kwa Mumewe...!
Cha ajabu katika Watu waliokamatwa kwa kuandaa na kutekeleza mpango wa Kuunguza Gereza, Kuua Mfungwa asiye na Hatia na kumtorosha Mhalifu, ni Baba ake Mzazi na huyo Doctor!!!
Kama mmeaminishwa kuwa kigezo cha kumtorosha dereva kilikuwa ni kumuogopa Magufuli. Sasa Magufuli ashafariki, na mama utawala wake ni tofauti na ule wa Magufuli.Dreva wa Lissu angebaki nchini angeuliwa na watu wa Magufuli. Tumia akili kwenye argument ya Lissu wacha kuchukua majibu mepesi ya Kamanda Sirro
Ondoa upumbavu hapa. Iko siku utakuja kujuwa kwa nini nimekuita mpumbavu. Tuombe uzima mungu azidi kutuweka hai. Waliompiga rosasi Tundu Lissu watakuja kufika mbele ya Mahakama. Usichukulie maridhiano ya Samia na Mbowe au ukimya wa Samia ukadhani ukurasa umefungwa. Jinai haizeeki wala haifiKama mmeaminishwa kuwa kigezo cha kumtorosha dereva kilikuwa ni kumuogopa Magufuli. Sasa Magufuli ashafariki, na mama utawala wake ni tofauti na ule wa Magufuli.
Mleteni dereva sasa ahojiwe na polisi, mbona Lisu mwenyewe ashakuja?
Mtoa mada Capt Tamar nashauri uendelee kutupa update ya kesi ya huyu muuaji na mbakaji wa South Africa inavyoendelea
ma chadomo mna shida sana yaani povu kama lote ...hapo unakuta unataka kuropoka matusi ila basi tu unaogopa barn...Ondoa upumbavu hapa. Iko siku utakuja kujuwa kwa nini nimekuita mpumbavu. Tuombe uzima mungu azidi kutuweka hai. Waliompiga rosasi Tundu Lissu watakuja kufika mbele ya Mahakama. Usichukulie maridhiano ya Samia na Mbowe au ukimya wa Samia ukadhani ukurasa umefungwa. Jinai haizeeki wala haifi
We nae unatumia akili zako au za mnyama fulaniOndoa upumbavu hapa. Iko siku utakuja kujuwa kwa nini nimekuita mpumbavu. Tuombe uzima mungu azidi kutuweka hai. Waliompiga rosasi Tundu Lissu watakuja kufika mbele ya Mahakama. Usichukulie maridhiano ya Samia na Mbowe au ukimya wa Samia ukadhani ukurasa umefungwa. Jinai haizeeki wala haifi