Thabo Mbeki atoa mawazo yake kuhusu mgogoro unaoendelea sasa katika DRC na vikosi vya M23

Thabo Mbeki atoa mawazo yake kuhusu mgogoro unaoendelea sasa katika DRC na vikosi vya M23

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Ni upuuzi Kwa DRC Congo kubagua section ya Raia wake eti Kwa madai kwamba wanazungumza Kinyarwanda hivyo sio Wakongomani wanatakiwa kuwa kicked out au kuuwawa.

Huu ni upuuzi wa Hali ya Juu kiasi kwamba Nchi jirani zikatae kuwasaidia unless kama kusaidia kwenyewe ni kulinda raia na kuiba Mali ya hao Wakongo wasio na akili.

Nyerere amewahi suluhisha huu mgogoro akawapa Elimu Kwa kutumia mfano wake lakini Bado hawataki .

Mandela amewahi suluhisha huu mgogoro akawapa Wakongo Elimu lakini Bado hawataki.

Sasa watu wa jamii hii kinachotakiwa na Umoja wa Mataifa Kuwaunga mkono M23 Ili Wachukue Eneo lote la Kivu kama Nchi huru na kukomesha mauaji ya raia wasio na hatia Kwa sababu za viongozi wajinga wa Kongo.

Kwamba Tanzania tuwatimue Waha Kwa sababu wako Burundi,Tutimue Masai na Wajaluo.kwa sababu wako Kenya?

Kwamba South Africa iwatimue Waswana Kwa sababu Kuna Botswana au?

Binafsi naunga mkono suluhisha la Nchi Mpya badala ya kwenda Kumtoa Tschisekedi Kinshasa Kwa sababu haitamaliza Vita wataviziana mda mwingine wapinduane tena Kwa vile Wakongo wengine walionyqwshwa sumu hawataridhika.

View: https://x.com/News24/status/1884950221907444114?t=-v8DMOfGyRjtW98a2YaH0Q&s=19
 
Ukweli ni kwamba mgogoro huu unaushabiki wa kijinga hasa kwa Watanzania ambao wamezoea ushabiki maandazi wa Yanga Vs Simba,CDM vs CCM,Pro- NATO Vs pro- Urusi na China nk

Huwezi bagua raia wa nchi y'ako ikiwa wao sio walio gawa mipaka miaka ya 1884/85 kisa tu ni tofauti na jamii ya walio wengi na mbaya zaidi wale vinara wa mauaji wa kimbari ya 1994 wamepewa hifadhi Congo na wanajeshi,alafu utegemee Rwanda ikae kimya na wakati hata Idd Amin tu wa hapo Uganda,aliamua kukiwasha baada ya kuona waasi wa serikali yake wapo Tanzania.

Ni muda wa Sisi waafrika kuacha kasumba za kipumbavu za kikabila ili kupata uugwaji mkono wa kujitwalia madaraka ni wakati wa kufanya mazungumzo ya kupata suluhu na sio matumizi ya bunduki.
 
Kongo ni liinchi likubwa ,halitawaliki kwa sasa,, livunjwe kuwa na mataifa matatu ,Kivu republic, Katanga na Congo ,ili kutulie. Ni mawazo tu lakini
 
Kwanini "raia" wasiokuwa na hatia ni hao "Banyamulenge" tu?
Kuna makabila mangapi huko Eastern Congo? Kwanini haki za kabila moja tu zilindwe? Mpaka wapewe nchi yao? Vipi kila kabila likidai nchi yake?
Wengine ni kina nani wanaosakwa?
 
Ukweli ni kwamba mgogoro huu unaushabiki wa kijinga hasa kwa Watanzania ambao wamezoea ushabiki maandazi wa Yanga Vs Simba,CDM vs CCM,Pro- NATO Vs pro- Urusi na China nk

Huwezi bagua raia wa nchi y'ako ikiwa wao sio walio gawa mipaka miaka ya 1884/85 kisa tu ni tofauti na jamii ya walio wengi na mbaya zaidi wale vinara wa mauaji wa kimbari ya 1994 wamepewa hifadhi Congo na wanajeshi,alafu utegemee Rwanda ikae kimya na wakati hata Idd Amin tu wa hapo Uganda,aliamua kukiwasha baada ya kuona waasi wa serikali yake wapo Tanzania.

Ni muda wa Sisi waafrika kuacha kasumba za kipumbavu za kikabila ili kupata uugwaji mkono wa kujitwalia madaraka ni wakati wa kufanya mazungumzo ya kupata suluhu na sio matumizi ya bunduki.
Mnabaguana na Kuuana Kwa visingizio vya kipumbavu harafu wote ni weusi 👇👇

View: https://x.com/zittokabwe/status/1885284574248526140?t=Z3ytP6u339V6B-Jz6cvagQ&s=19
 
Baada ya huu mgogoro kuibuka tena imebidi nijichimbie zaidi kupata ufahamu wa hili jambo. Nimejirisha kwamba serikali ya Congo Kishasa ina matatizo.

Shida iko Congo, Kishasa. M23 wana haki ya kutetea uraia wao kama serikali haiwataki, sasa waende wapi?
 
Hilo tatizo la kubaguliwa lipo sana toka miaka ya 50 + first genocide.na hao waasi wengi wanatumia kuleta machafuko huko huku wanabeba rasilimali.
Utashangaa mpk leo wanaongelea kwamba wanawafuatilia genocider.
Hapo utashangaa miaka 31 bado tu.
 
Ni ujinga kuvagua kabila/kundi moja la watu ktk jamii flani na ni upumbavu zaidi kugawanya eneo Ili jamii flani itulie.
 
Back
Top Bottom