Olaigwanani lang
JF-Expert Member
- Apr 26, 2012
- 547
- 181
WABUNGE WA CCM WANAHITAJI KUFANYA TATHIMINI YA KINA KUHUSU 2025.
Na Thadei Ole Mushi.
Wanachokifanya Chadema kwa Sasa ni kutokumshambulia Rais Samia kabisa kwenye Siasa zao badala yake wanadili kushambulia wabunge na Majimbo yao. Mfano Sugu anamenyana na Tulia, Lema anamenyana na Gambo, yaani ni Sawa na Jirani yako anakusifia kuwa wewe ni Mwema mnakunywa naye Chai lakini akikutana na watoto wako anawabamiza vilivyo. Na kwa Sasa CCM haswa watendaji wake hawana kazi ya kufanya kisiasa kwa sababu kila wakitaka kujibu hoja za wapinzani wanakuta wao hawana ugomvi na mwenyekiti wa CCM na ndiye anayekwenda kuwa mgeni Rasmi kwenye mkutano wa BAWACHA. Katika hali kama hiyo CCM inakosa uhalali wa kukabana Koo na Upinzani wanaamua kuacha.
Nitoe Ushauri kwa baadhi ya maeneo.
Nilisema hapa kuwa maridhiano ili yakamilike lazima baadhi ya majimbo ya CCM yarudi Chadema. Ni wakati sasa kwa wabunge wa CCM kuanza kujihami kama unaona jimbo lako CCM huwa inashinda kwa Shida au mazingira yanakuonyesha kuwa CCM haitashinda ni bora na wewe ukafanya maridhiano na CHADEMA mezani. Kama Mwenyekiti wako wa Chama hana matatizo na Chadema wewe mbunge unapata Shida gani ya kutengeneza Kesho yako kupitia Chadema? kwa mazingira yaliyopo inawezekana kabisa Ukatoka CCM ukaenda Chadema na Ukashinda Uchaguzi.
Jambo la pili ambalo naliona kwa aina ya Siasa zilivyo Kura za Maoni ndani ya CCM zitakiacha CCM Kikiwa kimedhoofu kabisa. Kipindi cha JPM ilikuwa ukishindwa kura za maoni ndani ya Chama huthubutu kuhamia upinzani maana kuhamia upinzani kulikuwa na Garama kubwa sana kwako na familia yako. Watu wenye uwezo walishinda ndani ya CCM kwenye kura za Maoni lakini CCM mpya ya Kina JPM walileta jina wanalolitaka na aliyeshinda anaufyata mkia. 2025 itakuwa mwaga ugali nimwage mboga na eneo hili litawapatia upinzani wagombea wengi sana waliohama toka CCM na wafuasi wao. Siasa za sasa zinaruhusu hayo kutokea hali haitakuwa kama awali.
Jambo la tatu ni kwamba Kanda zetu zimegawanyika katika hoja za uchaguzi 2025. Kuna makosa upinzani wanayafanya wanatakiwa waachane nayo mara moja kama wanataka kuimarika zaidi 2025.
Mfano Upinzani Kanda ya Ziwa wanatakiwa waachane kabisa na hoja za kumshambulia JPM. Yoyote atakayeshambulia Kivuli au Kaburi la JPM hatobaki salama eneo hili. Kwa bahati Mbaya CCM hatujaweza kuitumia vizuri fursa ya JPM eneo hili vivyo hivyo upinzani nao wameingia kwenye Siasa za kumshambulia JPM. Chadema wakitaka kuwin eneo hili wasimshambulie bali wamtumie kupata kura. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya JPM na kura za Ukanda huu.
Majimbo ya Mjini baada ya vurugu za kura za maoni ndani ya CCM tutaelekea kwenda kujibu hoja za vijana kuhusu ajira. Kwa historia Chadema wamekuwa wakishinda kirahisi sana majimbo ya Mjini nitakuja kuwaambia kwa nn siku za nyingine, ni majimbo ambayo hayana agenda nyingi zaidi ya ajira na Mzunguko wa Fedha.
Majimbo ya Kusini tutaenda kuwainyesha ni wapi wauze Korosho zao jambo ambalo pia itakuwa shughuli…..
Majimbo ya Kaskazini wao hawajaamini kinachoendelea kama ni kweli kuhusu Maridhiano otherwise hapa wanasubiri tu Iyena iyena za Chopa. Ni moja ya majimbo magumu sana kwa CCM. JPM aliyachukua kibabe 😀😀😀😁 ila nao hawana agenda za kuwadanganyia. Majimbo haya huwezi kuwaahidi Umeme kwa kuwa upo, barabara zipo, maji yapo, shule zipo, zahanati na hospitali zipo, wazee wana watoto mjini wanawatumia hela ya kula nk. Siasa upande huu ni mchezo kama ulivyo mchezo wa Soka.
Majimbo ya Katikati mwa Nchi kuna Migogoro Mikubwa sana kati ya Wafugaji na wakulima. Hii ndio agenda kubwa kwao…. Nani mwenye uwezo wa kuwasaidia ndiye atakaye chukua Jimbo.”
Niwashauri sana wabunge wa CCM wafanye Tathimini ya Kina kabla ya kurusha karata yake 2025 kama hali itakuwa hivihivi. Hakuna Polisi atakayeshughulika na mambo yako kisiasa, hakuna Mkurugenzi atakayekata jina la mtu kisa kajaza fomu vibaya, hakuna mtu atakusaidia kumpora mgombea fomu wakati wa kurudisha.
Siasa inayoendelea sasa ni kati ya Mwenyekiti wa CCM na Chadema sio Chadema na CCM kwa ujumla wake. Zama zimebadilika….
Ole Mushi
0712702602