October man
JF-Expert Member
- Nov 23, 2017
- 3,631
- 5,023
Kwenye siasa hakuna issue za IQ. Kama IQ ingekuwa inapimwa kwa maamuzi ya kisiasa, mbona US wangekuwa na IQ ndogo sana. Ongelea mengine kama ya kikombe cha babu, lakini sio SIASA. Siasa ni ubishi tu, lakini si akili.
Haujajibu swali langu kwamba kwa mujibu wa hizo takwimu na kanuni uliyoiweka ya kukokotoa IQ, Tanzania inaonyesha raia wake wana wastani wa IQ ya 71 ambayo ni namba kubwa kulinganisha na nchi nyingine lakini bado maelezo yanasema wana uelewa mdogo.
Shida yangu ipo hapo kwenye ukokotoaji, mtu mwenye congnitivu kubwa na umri mdogo lazima IQ itakua kubwa, kwanini wenye 71 umewaelezea kwamba wana IQ ndogo wakati kuna nchi wananchi wake wana IQ ndogo zaidi Afrika Mashariki wakati hata hizo nchi haujaziweka kujua wananchi wake wana IQ ya ngapi?
Kwenye mazingira hayo hayo unayosema kuwa ni mabovu bado kuna watu wana uwezo mkubwa?Mkuu umesema...."Wapo watoto walikuwa na uwezo mzuri juu ya mambo mbalimbali km usemavyo, ila wakifika umri fulani hurudi kuwa wa KAWAIDA kabisa ama VILAZA kabisa (kuanzia chekechea hadi darasa la tatu mpaka la nne huwa vizuri, ilaikshaingia darasa la tano uwezo wake wa kufikiria hushuka,"
Usisahau kwamba kuna factors zinazo determine the development of IQ yamtoto mojayapo ni mazingira anayo ishi Mtoto, nutrition, sera za serikali nk....kwahiyo hao watoto ni victims wa hizo factors....... mfano mzuri watoto tunao wapeleka hizi shule za st Kayumba wanatoka nyumbani wakiwa competitive ila wakianza kuzoea shule wanamaliza kupata div zero.
Hahaaaa[emoji84] [emoji84] [emoji84] [emoji84] [emoji84] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]Ngoja nipime IQ ya bashite hapa haha muone
(03×100 ) ÷ 34 = 08
Naunga mkono hoja maana matendo ya bashite sawa na mtoto wa miaka mitatu kwaiyo IQ 8 inaukweli
Uo utafiti umeufanyia wapi, mwanafunzi aliekuwa wakwanza kisha anakuwa wa mwisho? Wewe umegundua kitu kipya ambacho hata hakijawahi kuwepo.Wakati mwingine kufikiri nje ya box huleta maana sana kwa watu wenye uelewa mzuri na mpana wa kuchambua na kudadavua mambo. Kiuhalisia si kila tafiti ni tafiti sahihi, nami nasema watu hao wapo wrong na hufanya hivyo ku_serve interest zao.
Nataka nikupe mfano na naomba uende ukafanye tafiti yako na wewe uje na majibu na uyalete hapa; Wapo watoto walikuwa na uwezo mzuri juu ya mambo mbalimbali km usemavyo, ila wakifika umri fulani hurudi kuwa wa KAWAIDA kabisa ama VILAZA kabisa (kuanzia chekechea hadi darasa la tatu mpaka la nne huwa vizuri, ilaikshaingia darasa la tano uwezo wake wa kufikiria hushuka, na kuna wengine pia kuanzia kipindi hiki au hadi anapoanza kidato cha kwanza ndipo ufahamu wao unaanza kuwa wa hali ya juu). Je, scenario km hiyo inakuwa vipi? Kafanye tafiti na uje na majibu.
Na watu kushangilia akati mwenzetu katekwa hiyo nn nn?je viongozi wa serikali kuwaziba midomo wananchi kizungumxia ukweli hilo nalo lipo wapi?Na Thadei Ole Mushi.
Niliwahi kufundisha kidogo hapa kuhusu uwezo wa akili au kitaalamu (IQ) yaani Hisa ya akili.
Mwaka jana kuna ripoti ilitoka ikiwa inaitaja Tanzania kushika nafasi ya 9 katika nchi zenye watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri.
Kwa mujibu wa orodha hiyo,Tanzania inashika nafasi ya 9 wananchi wake wakiwa na uwezo wa kufikiri (IQ) 72, Ghana inashika nafasi ya 8 kwa wananchi wake kuwa na kiwango cha chini cha IQ yaani 71. Nafasi ya saba ni Nigeria (67), nafasi ya sita ni Guinea (66), nafasi ya tano ni Zimbabwe (66), nafasi ya nne ni DR Congo (65), nafasi ya tatu ni Sierra Leone (64), nafasi ya pili ni Ethiopia (63) na nafasi ya kwanza ni Equatorial Guinea (59).Katika nchi zote hapo Tanzania pekee ndio inayojitokeza kwenye orodha hiyo ikiwa imetokea ukanda wa Africa Mashariki.
Kuna wengi watashindwa kupata tafsiri ya kilichomo kwenye mabano yaani number zilizomo kwenye mabano hivyo ni vizuri nikafafanua tena hili.
Mwaka 1904 mwanasaikolojia Alfred Banet alitambulisha nadharia ya namna ya kupima Uwezo wa mtu wa kufiki (IQ) Baadaye 1979 alitokea mtu mwingine aliyekuja kuboresha kidogo tu nadharia hii anaitwa Hilgard huyu aliainisha viwango vya akili ya mwanadamu.
Wananadharia hii kwa pamoja hawajawahi kutofautina na maana halisi ya Hisa ya akili. Wote wanakubaliana kuwa hisa ya akili kipimo cha maendeleo ya kitaaluma kwa kuwianisha UMRI wa kuzaliwa wa mtoto na UMRI wa akili.
Ili uweze kupata hisa ya akili ya mtu unatakiwa uchukue UMRI wa akili ×100 halafu gawanya kwa UMRI wa kuzaliwa.
UMRI wa akili hupatikana kwa kukadiria matendo ayafanyayo mtu. Kwa mfano nyumbani una mtoto wa Miaka 10 lakini matendo yake na uwezo wake unalingana na mtoto wa Miaka 15 basi miaka hiyo 15 ndio UMRI Wake kiakili hivyo utachukua (15×100 ) ÷ 10 = 150.
Nini tafriri yake? Wanasaiokolojia hawa katika nadharia hii wameonyesha pia matokeo ya ukokotoaji kwa mfano hapo jibu tumepata ni 150 mtoto huyu atakuwa ni mwenye kipaji maalumu kwani hawa huanzia 139+ .
Chini ya hapo 129-139 ni wenye Akili za juu sana sana, 110-119 hawa wana akili za juu,90-109 wastani, 80-89 wapo chini ya wastani na 70-79 wana akili duni, chini ya 70 hawa wana mtindio wa ubongo (tahira).
Tunapozungumzia hisa ya akili hatumaanishi uwezo alionao mtu katika kukokotoa hisabati au kujibu maswali ya physics kwa ufasaha bali ni ule uwezo wa mtu kutafsiri na kuchambua taarifa mbalimbali zinazofikishwa kwenye ubongo kitaalamu huitwa ABSTRACT REASONING.
Kwa maana hiyo ukichukua mtanzania ukamweka kwenye kundi la wakenya, wanyarwanda nk basi atashika nafasi ya Mwisho katika kutafsiri na kupata ufahamu kwa mambo ambayo yatakuwa mbele yao.
Kuwa na hisa ndogo ya akili hakutokani na kukosa tu elimu ya Darasani japokuwa nayo huchangia bali hutokana na sababu nyingine nyingi kama vile Lishe duni, afya duni, aina ya genes tunazorithi toka kwa mababu zetu nk.
Dr James Watson aliwahi kusema " black people are less intelligent than white people" Huyu Dr alifanya justification ya argument yake kwa kusema kuwa ujinga ni kitu cha kurithi na ni kama ugonjwa. Hili limeshawahi kudhihirishwa na nadharia nyingine nyingi za kisayansi na za kisaikolojia.
Tuangalie sasa ni mambo gani ambayo hata hivyo yanaweza kuwa ni ushahidi wa ujinga wetu:-
1. Pitia scandal ya UPATU ya DECI.
2. Agalia jinsi ukawa ilivyomtukana Lowassa na baadaye wanamsafisha.
3. Angalia jinsi babu wa Loliondo alivyo tuburuza
4. Angalia michango ya wabunge wetu bungeni na jinsi tunavyowashangilia.
5. Angalia rasilimali tulizonazo na uchumi wetu kama vinaendana.
6. Angalia kwa nini Sumaye alihamia Chadema na bado tunaendelea kushangilia na kupiga makofi
Kuna mambo mengi tu yanayodhihirisha ujinga wetu hata wewe unaweza kuyaongeza katika huo mtiririko.Hata comment yako pia inaweza kukutambulisha aina ya IQ uliyonayo.
Sio kweli, Awamu ya tano inawabunge wengi wasomi kuliko awamu yeyote, darasa la saba ni wa kuhesabu tofauti na zamani.Hata hivyo kamati nyingi huongozwa na wabunge waliobobea katika mambo husika.Naomba unitajie ni mkoa gani unawabunge wote darasa la saba.Hata wakiwa darasa la saba serikali ina wasomi ambao huibua hizo sera na kuzipeleka zipitishwe bungeni kwa hiyo kama wasomi wa wizara mbalimbali wako makini wabunge si wa kuwalaumuumasikini na ujinga vinakwenda sambamba, hata tukiwa na rasilimari nyingi kiasi gani bado tutaendekea kuburuta mkia kwakua nchi imejaa mbumbumbu wengi kuliko werevu. natumaini JF tutapiga kampeni ya kufa mtu 2020 kuhamasisha vijana wasomi wachukue fomu za kugombea ubunge na udiwani kwenye vyama vyote!! ni wakati sasa umefika tuwe serious na hatma ya nchi yetu badala ya kuiacha mikononi mwa watu kama kina nkamia, kibajaji, msukuma n.k (na wazee wanaojali matumbo yao kama vile mwakyembe, chenge n.k wapigwe chini, hawana jipya)
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kumbe ndio maana cape verde wametufunga
94% walio kilingeni ni tumbo kwanza,wakiambia ni Miaka 7 saba watasema ndiooo!!Kiongozi ukifatilia siasa uta utapasuka kichwa
Wachache unao ona wapo chini ya tumbo niwachache tu ndo wanajenga Tanzania
Wanao jua kuusu kesho ya Tanzania sio wanao jua Leo zao na sio Tanzania niayo tu
Sababu ya chama kinachoongoza plus moto ule wa matambiko alioutoa kuzimu forojo ganzeKuna ukweli kiasi fulani katika hili aisée maana hata jinsi wabongo reasoning zetu ni za ajabu tu kama ukifuatilalia kiundani si viongozi si wananchi wote walewale
Kuna mkakati wa 'kimataifa' wa kuzivuruga IQ za mataifa masikini zibakie duni milele! Unasemaje hapa Paskali?Wakati mwingine kufikiri nje ya box huleta maana sana kwa watu wenye uelewa mzuri na mpana wa kuchambua na kudadavua mambo. Kiuhalisia si kila tafiti ni tafiti sahihi, nami nasema watu hao wapo wrong na hufanya hivyo ku_serve interest zao.
Nataka nikupe mfano na naomba uende ukafanye tafiti yako na wewe uje na majibu na uyalete hapa; Wapo watoto walikuwa na uwezo mzuri juu ya mambo mbalimbali km usemavyo, ila wakifika umri fulani hurudi kuwa wa KAWAIDA kabisa ama VILAZA kabisa (kuanzia chekechea hadi darasa la tatu mpaka la nne huwa vizuri, ilaikshaingia darasa la tano uwezo wake wa kufikiria hushuka, na kuna wengine pia kuanzia kipindi hiki au hadi anapoanza kidato cha kwanza ndipo ufahamu wao unaanza kuwa wa hali ya juu). Je, scenario km hiyo inakuwa vipi? Kafanye tafiti na uje na majibu.
Nadhani si kwa watanzania wote. Binafsi nikiwa nje ya nchi nilishawagi kutake IQ test.. a real test inayotambulika kimataifa. Lakin niliscore zaidi ya hapo.Na Thadei Ole Mushi.
Niliwahi kufundisha kidogo hapa kuhusu uwezo wa akili au kitaalamu (IQ) yaani Hisa ya akili.
Mwaka jana kuna ripoti ilitoka ikiwa inaitaja Tanzania kushika nafasi ya 9 katika nchi zenye watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri.
Kwa mujibu wa orodha hiyo,Tanzania inashika nafasi ya 9 wananchi wake wakiwa na uwezo wa kufikiri (IQ) 72, Ghana inashika nafasi ya 8 kwa wananchi wake kuwa na kiwango cha chini cha IQ yaani 71. Nafasi ya saba ni Nigeria (67), nafasi ya sita ni Guinea (66), nafasi ya tano ni Zimbabwe (66), nafasi ya nne ni DR Congo (65), nafasi ya tatu ni Sierra Leone (64), nafasi ya pili ni Ethiopia (63) na nafasi ya kwanza ni Equatorial Guinea (59).Katika nchi zote hapo Tanzania pekee ndio inayojitokeza kwenye orodha hiyo ikiwa imetokea ukanda wa Africa Mashariki.
Kuna wengi watashindwa kupata tafsiri ya kilichomo kwenye mabano yaani number zilizomo kwenye mabano hivyo ni vizuri nikafafanua tena hili.
Mwaka 1904 mwanasaikolojia Alfred Banet alitambulisha nadharia ya namna ya kupima Uwezo wa mtu wa kufiki (IQ) Baadaye 1979 alitokea mtu mwingine aliyekuja kuboresha kidogo tu nadharia hii anaitwa Hilgard huyu aliainisha viwango vya akili ya mwanadamu.
Wananadharia hii kwa pamoja hawajawahi kutofautina na maana halisi ya Hisa ya akili. Wote wanakubaliana kuwa hisa ya akili kipimo cha maendeleo ya kitaaluma kwa kuwianisha UMRI wa kuzaliwa wa mtoto na UMRI wa akili.
Ili uweze kupata hisa ya akili ya mtu unatakiwa uchukue UMRI wa akili ×100 halafu gawanya kwa UMRI wa kuzaliwa.
UMRI wa akili hupatikana kwa kukadiria matendo ayafanyayo mtu. Kwa mfano nyumbani una mtoto wa Miaka 10 lakini matendo yake na uwezo wake unalingana na mtoto wa Miaka 15 basi miaka hiyo 15 ndio UMRI Wake kiakili hivyo utachukua (15×100 ) ÷ 10 = 150.
Nini tafriri yake? Wanasaiokolojia hawa katika nadharia hii wameonyesha pia matokeo ya ukokotoaji kwa mfano hapo jibu tumepata ni 150 mtoto huyu atakuwa ni mwenye kipaji maalumu kwani hawa huanzia 139+ .
Chini ya hapo 129-139 ni wenye Akili za juu sana sana, 110-119 hawa wana akili za juu,90-109 wastani, 80-89 wapo chini ya wastani na 70-79 wana akili duni, chini ya 70 hawa wana mtindio wa ubongo (tahira).
Tunapozungumzia hisa ya akili hatumaanishi uwezo alionao mtu katika kukokotoa hisabati au kujibu maswali ya physics kwa ufasaha bali ni ule uwezo wa mtu kutafsiri na kuchambua taarifa mbalimbali zinazofikishwa kwenye ubongo kitaalamu huitwa ABSTRACT REASONING.
Kwa maana hiyo ukichukua mtanzania ukamweka kwenye kundi la wakenya, wanyarwanda nk basi atashika nafasi ya Mwisho katika kutafsiri na kupata ufahamu kwa mambo ambayo yatakuwa mbele yao.
Kuwa na hisa ndogo ya akili hakutokani na kukosa tu elimu ya Darasani japokuwa nayo huchangia bali hutokana na sababu nyingine nyingi kama vile Lishe duni, afya duni, aina ya genes tunazorithi toka kwa mababu zetu nk.
Dr James Watson aliwahi kusema " black people are less intelligent than white people" Huyu Dr alifanya justification ya argument yake kwa kusema kuwa ujinga ni kitu cha kurithi na ni kama ugonjwa. Hili limeshawahi kudhihirishwa na nadharia nyingine nyingi za kisayansi na za kisaikolojia.
Tuangalie sasa ni mambo gani ambayo hata hivyo yanaweza kuwa ni ushahidi wa ujinga wetu:-
1. Pitia scandal ya UPATU ya DECI.
2. Agalia jinsi ukawa ilivyomtukana Lowassa na baadaye wanamsafisha.
3. Angalia jinsi babu wa Loliondo alivyo tuburuza
4. Angalia michango ya wabunge wetu bungeni na jinsi tunavyowashangilia.
5. Angalia rasilimali tulizonazo na uchumi wetu kama vinaendana.
6. Angalia kwa nini Sumaye alihamia Chadema na bado tunaendelea kushangilia na kupiga makofi
Kuna mambo mengi tu yanayodhihirisha ujinga wetu hata wewe unaweza kuyaongeza katika huo mtiririko.Hata comment yako pia inaweza kukutambulisha aina ya IQ uliyonayo.
Ukiniambia chadema IQ yao ipo juu nakataa kwa % buku tatuCHADEMA na Lowassa hiyo ni siasa ambapo waliangalia nguvu ya kisiasa mhusika katika jamii na nguvu hii ilijidhihirisha katika kura alizopata ukilinganisha na kura za wagombea wa CHADEMA wa uraisi kwa miaka yote iliyotangulia.
Kwa msingi huo huo wa ushawishi alionao mtu kisiasa,ndio maana leo hii CCM wanamtukuza na kumkubali Dr.Slaa ingawa wakati yuko CHADEMA aliitwa muongo na mzushi ila leo na cheo wamempa na wanamuamini kwa kila akisemacho hasa anaposhambulia upinzani(hii nayo ni siasa)
Hapa utagundua kuwa wanasiasa wanachofanya ni kufanya maamuzi kulingana na akili za watu wao na si kutokana na kile wanachokijua wao(ni sawa na mfanyabiashara ambae yeye huangalia bidhaa inayopendwa na walaji basi hiyo ndio ataiingiza sokoni hata kama anajua ina mapungufu).
Ukweli ni kwamba,kama watanzania wangekuwa wanajali ufisadi,basi CCM ingekuwa imeshapoteza dola tangu chaguzi za nyuma na hata wabunge wa CCM kama kina Chenge wasingekuwa wanashinda ubunge.CHADEMA walilijua hilo na ndio maana wakampa nafasi Lowassa(kumbuka hata wana-CCM waliimba kuwa wana imani na Lowassa mbele ya JK).
Binafsi nililiona hili na ndio maana nilisema CHADEMA wamefanya uamuzi sahihi kulingana na mahitaji wa wapiga kura(walaji) na kwakuwa adui yetu mkubwa ni CCM kuliko Lowassa,basi niliona tumpe nafasi huyo Lowassa mradi tu anakubalika tuiondoe CCM madarakani kwanza alafu ndio mambo mengine yafuate baadae.
Kwahiyo kwa kifupi utagundua,viongozi wa CHADEMA IQ yao iko juu(waliangali bidhaa inayouzika pande zote wakaiingiza sokoni) na matokeo yalionekane kwenye ule uchaguzi kwa kupata kura nyingi za uraisi kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma na tungekuwa na tume huru si ajabu Lowassa angeshinda uraisi na hapa tungeseme "the end justifies the means."
In short,tatizo ni IQ ya wapiga kura na ndio maana wengi pia waliamini Ngosha anachukia ufisadi kumbe nae ni wale wale wakasahau kashifa zake nyingi na maamuzi yake ya hovyo hovyo matokeo yake leo wote tunalalamika.
Nikiri IQ ya wabongo iko chini na hata EL leo akitangaza kurudi CCM atapokewa kwa mbwembwe nyingi tena tukio hilo linaweze kurushwa live.