Thadey Kweka apandishwa mahakamani leo Desemba 31, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi

Thadey Kweka apandishwa mahakamani leo Desemba 31, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi

Asijipe sana kuburi eti kwa kuwa ana Passport ya USA. Kwa Marekani ya Donald Trump as long as ni raia mweusi, sidhani kama atapata usaidizi.

Trump amekuwa anawapiga sana vita raia wa kuandikisha. Hivyo huyu Mchagga ambaye amedakwa huku, itakuwa ni nafuu kwa America
 
Ha ha haa 🤣🤣🤣
Huyo chawa alitamani kuona unateswa na kusumbuliwa na watekaji.
Imekuwa dua ya kuku, au ile hadithi ya fisi anatamani mkono wa binadamu udondoke aokote.
Bora ubaki huko huko. Huku ujinga mwingi.
Kwa sasa hata likizo nakwenda visiwa vya Turks and Caicos.

Na badala ya mimi kuja Bongo kuiona familia yangu, familia yangu inakuja US kila mwaka kuniona mimi.

Sitaki ujinga.
 
Asijipe sana kuburi eti kwa kuwa ana Passport ya USA. Kwa Marekani ya Donald Trump as long as ni raia mweusi, sidhani kama atapata usaidizi.

Trump amekuwa anawapuga sana vita raia wa kuandikisha. Hivyo huyu Mchagga ambaye amedakwa huku, itakuwa ni nafuu kwa America
Unamaanisha raia wa kujiandikisha Melania Trump? Bilashaka unatambua kwamba kwa wenzetu rais hatekelezi sheria kwa utashi wake mkuu. Hata kama hataki kukutetea sheria ikimtaka akuteteee atakutetea. Halafu hii ni issue minor sana kwao. Itashuhulikiwa na career staff wa kawaida tu wa state department na wala siyo rais.
 
Baada ya kushikiliwa kwa siku 3 kituo kikuu cha polisi (Central) Moshi, hatimaye Thadei Kweka amepandishwa mahakamani mchana huu, leo Desemba 31, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

Ikumbukwe Thadei ni raia wa Marekani (alishaukana uraia wa TZ). Hata alipokuja aliingia kama mgeni kwa kutumia Tourist Visa (Single Entry) ambayo hutolewa kwa raia wa kigeni kwa ukaaji usiozidi siku 90.

Serikali ya Marekani imetaka kujua kuhusu shauri hili baada ya kusikia raia wake amekamatwa. Jana Ubalozi wa Marekani umetuma fomu maalumu (Consular Notification and Access Form) ambayo Thadei anatakiwa kusaini ili Serikali ya Marekani iweze kuwa involved katika kesi hiyo. Lakini polisi wamekataa asisaini.

Aidha, polisi walimzuia Wakili wake asionane naye, jambo ambalo ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa kifungu cha 50(1)(b) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA Cap20) kinacholinda haki ya mtuhumiwa kuwasiliana na wakili wake. Ndugu zake wanadai jana walimpelekea chakula lakini wakazuiwa kumuona na hata chakula chao kilikataliwa.

Leo polisi wamempeleka Mahakamani bila kujulisha ndugu wala Wakili wake. Hii ni kinyume na Kifungu cha 50(2) CPA kinacholinda haki ya mtuhumiwa kupewa taarifa na kuandamana na wakili wake wakati wa kupelekwa mahakamani.

Sidhani kama Polisi wanajua hiki wanachofanya kinaweza kuleta mgogoro wa kidiplomasia. Kwa mujibu wa Vienna Convention on Consular Relations (1963), Articles 36 & 37 nchi mwenyeji inalazimika kutoa taarifa kwa ubalozi mara tu raia wa kigeni anapokamatwa. Pia inatakiwa kuruhusu ubalozi wake kuwasiliana naye.

Kumzuia Thadei kusaini Consular Notification and Access Form na kuzuia mawasiliano na ubalozi wake ni ukiukwaji wa moja kwa moja wa mkataba wa Vienna.

Matokeo yake ubalozi wake unaweza kutoa "Diplomatic Protest note" ambayo itazuia raia wa bongo kuja US na raia wa US kwenda bongo mpaka hilo shauri litatuliwe. Kwa luga rahisi kama una kampuni ya utalii umechukua hela za wageni wa Marekani anza kuwarudishia. Na kama wewe ni mwanafunzi umepata chuo Marekani na bado hujaja, anza kutafuta admission Theofilo Kisanji University. Ngoma inakaribia kuwa ngumu kwa ujinga wa Polisi.!

Pia Soma: Thadei Kweka achukuliwa na watu wanaodaiwa kuwa Polisi baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Moshi

Wanaoishi marekan wote kama wavuta bangi wakiongozwa mange kimambi.
 
Wewe dada muache mchaga wa watu aliyekimbia mateso ya bongo, anenepe,

Marekani hawanywi maji ya matope kama Dar, wala stress na hofu ya kumiminiwa risasi kama wanauwa mbwa kichaa.
 
Unamaanisha raia wa kujiandikisha Melania Trump? Bilashaka unatambua kwamba kwa wenzetu rais hatekelezi sheria kwa utashi wake mkuu. Hata kama hataki kukutetea sheria ikimtaka akuteteee atakutetea. Halafu hii ni issue minor sana kwao. Itashuhulikiwa na career staff wa kawaida tu wa state department na wala siyo rais.
Hawezi kuhangaika na weusi kutoka shithole countries. Hao ndiyo hawataki kuwaona huko USA, sasa mkishamsaidia kumzuia huyo asirudi kwake ni furaha
 
Pale wasimamizi wa sheria wanapokuwa wa kwanza kuvunja sheria, nani anapona
 
..kama ana pasi ya marekani basi uhamiaji wanapaswa kumfukuza nchini na sio kusumbuana naye.
Kuna uwezekano bado pia ana passport ya TZ. Diaspora wengi wanakuwa na Passport mbili za TZ na nchi ya Kigeni hasa nchi zinazoruhusu dual citizenship wakati sisi TZ hairuhusiwi hivyo labda ndio maana Polisi wamemng'ang'ania. Kitu cha kushangaza hata huyo Malisa hajaeleza amepelekwa mahakamani kwa kosa gani bali ametoa malalamiko tu eti USA watatunyosha ana slavery mentality inamsumbua.
 
Kwa sasa hata likizo nakwenda visiwa vya Turks and Caicos.

Na badala ya mimi kuja Bongo kuiona familia yangu, familia yangu inakuja US kila mwaka kuniona mimi.

Sitaki ujinga.
Baki huko huko huna faida kwa TZ 😀
 
Unamaanisha raia wa kujiandikisha Melania Trump? Bilashaka unatambua kwamba kwa wenzetu rais hatekelezi sheria kwa utashi wake mkuu. Hata kama hataki kukutetea sheria ikimtaka akuteteee atakutetea. Halafu hii ni issue minor sana kwao. Itashuhulikiwa na career staff wa kawaida tu wa state department na wala siyo rais.
Hivi karibuni tu kamrudisha Marekani mtoto wa Christian Malanga aliyeshirikiana na baba yake ktk jaribio la kumpindua Rais Tshisekedi wa Congo. Alimrudisha pia Abrego Garcia Marekani kutoka El Salvador maximum security prison baada ya shinikizo la mahakana na umma. Mpaka sasa anajaribu kum deport tena Garcia ila kila akijaribu anashindwa mahakamani. Kumbuka Garcia is a real "criminal immigrant". Tena anatuhumiwa kuwa gang member. Iwe Kweka ambaye anatuhumiwa kwa uchochezi alioufanya Marekani ambako kwao hiyo ni free speech? Siungi mkono uanaharakati uchwara Ila huyu Kweka wangenwacha tu. Ni kesi dhaifu sana.
 
Marekani katu haiwezi kuharibu uhusiano wake na Tanzania kisa kweka.
Tungekua Rwanda au Congo yes. Wale wana rare earth minerals. Tz hatuna kitu unique cha kuwapa Wamarekani. Gas hawana mpango nayo. Gold tunazidiwa na nchi nyingi Africa. Hatuna hata magaidi wa kuwatisha kama walivyo wenzetu Nigeria , Somalia, Niger etc.
 
Asijipe sana kuburi eti kwa kuwa ana Passport ya USA. Kwa Marekani ya Donald Trump as long as ni raia mweusi, sidhani kama atapata usaidizi.

Trump amekuwa anawapuga sana vita raia wa kuandikisha. Hivyo huyu Mchagga ambaye amedakwa huku, itakuwa ni nafuu kwa America
Tena wanasema one less nigger to worry about
Huyu hata kama ataachiwa hii itakuwa ni lesson learned the hard way, na sijui kama atarudi bongo tena kama CCM bado wapo.
 
Unamaanisha raia wa kujiandikisha Melania Trump? Bilashaka unatambua kwamba kwa wenzetu rais hatekelezi sheria kwa utashi wake mkuu. Hata kama hataki kukutetea sheria ikimtaka akuteteee atakutetea. Halafu hii ni issue minor sana kwao. Itashuhulikiwa na career staff wa kawaida tu wa state department na wala siyo rais.
Soma hapa sio unajipa umuhimu kwa uraia wa nchi za wazungu
Hivi unadhani wakati wanafanya hivi hawajui kuwa hawa ni raia wa US, wanajua sana na wanafanya makusudi

1767225133445.png

1767225187781.png
 
Back
Top Bottom