Thailand: Idadi 'kubwa' ya watu wauawa kwa kufyatuliwa risasi na mwanajeshi

Thailand: Idadi 'kubwa' ya watu wauawa kwa kufyatuliwa risasi na mwanajeshi

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,060
Mwanajeshi mmoja nchini Thailand amewashambulia kwa kuwafyatulia risasi watu kadhaa na kuua idadi "kubwa" ya watu.

Tukio hilo limetokea katika mji wa Nakhon Ratchasima pia ukijulikana kama Korat kaskazini mashariki mwa jiji la Bangkok.

Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini humo amesema kuwa mwanajeshi huyo, Jakraphanth Thomma, alimshambulia mkuu wake kwanza kabla ya kuanza kufyatua risasi katika kambi ya kijeshi, hekalu la Buddha pamoja na kituo cha ununuzi.

Mamlaka za ulinzi na usalama zimezingira na kukifunga kituo hicho cha ununuzi ili kujaribu kumkamata mtuhumiwa, ambaye inasemekana bado yumo ndani ya jengo hilo. Polisi wamewaonya watu kujifungia ndani ya nyumba zao.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa watu wasiopungua 12 wameuawa katika shambulizi hilo.

Jarida la Bangkok liliripoti kwamba mtuhumiwa huyo, ambaye ametajwa kuwa na umri wa miaka 32, alikuwa amechukua baadhi ya watu kama mateka ndani ya jengo hilo, ingawa bado haijathibitishwa rasmi. Risasi zaidi zimeripotiwa kusikika ndani ya jengo hilo.

Nia na madhumuni ya mtuhumiwa kufanya shambulizi hilo bado haijajulikana wazi.

Hata hivyo, aliweka katika kurasa zake za mitandao ya kijamii matukio ya wakati alipokuwa akitekeleza shambulio hilo, na ujumbe mmoja katika ukurasa wake wa Facebook akiuliza ikiwa inampasa kujisalimisha.

Hapo awali alikuwa ameweka picha ya bastola iliyo na seti tatu za risasi, pamoja na maneno: "Ni wakati wa kufurahi" na ujumbe mwingine ukisomeka "hakuna mtu anayeweza kuzuia kifo".

Ukurasa wake wa Facebook sasa umefungiwa.

Jarida la Bangkok limesema kamanda ambaye ni marehemu ametambulika kama Kanali Anantharot Krasae, na kwamba mwanamke wa miaka 63 na askari mwingine waliuawa katika kambi ya jeshi.

1581169773877.png

Jakraphanth Thomma.

====

Thai soldier kills 'many' in shooting rampage

A Thai soldier has shot dead "many people" in and around city of Nakhon Ratchasima (also known as Korat), north-east of Bangkok, reports say.


A Thai soldier has shot dead "many people" in and around city of Nakhon Ratchasima (also known as Korat), north-east of Bangkok, reports say.

A defence ministry spokesman told BBC Thai that Jakraphanth Thomma attacked his boss before opening fire at a military camp, a Buddhist temple and a shopping centre.

The suspect is hiding in the basement of the shopping centre, he added.

Local media are reporting at least 12 deaths.

The incident is still ongoing.

Posts on social media appear to show the scene of a shooting near a shopping centre.

====

Thailand shooting: Soldier's rampage kills at least 12

A defence ministry spokesman told BBC Thai that Jakraphanth Thomma, a junior officer, had attacked his commanding officer before stealing a gun and ammunition from a military camp.

He then opened fire at a Buddhist temple and at a shopping centre in the city, north-east of Bangkok.

The suspect is still at large.

Local media footage appears to show the suspect getting out of a car in front of the Terminal 21 shopping centre in the Muang district and firing shots as people flee. Other footage showed a fire outside the building.

Authorities have been sealing off the centre as they try to track down the suspect, who is reportedly inside the building. Police have warned people to stay at home.

The Bangkok Post reported that the suspect, who it said was 32 years old, had taken hostages inside the building, but this has not been officially confirmed. More gunshots have reportedly been heard inside the building.

The suspect's motive remains unclear.

However, he posted on his social media accounts during the attack, with one post on Facebook asking whether he should surrender.

He had earlier posted an image of a pistol with three sets of bullets, along with the words "it is time to get excited" and "nobody can avoid death".

His Facebook page has now been taken down.

The Bangkok Post said the dead commander was Col Anantharot Krasae, and that a 63-year-old woman and another soldier had been killed at the military camp.

Source: BBC

1581170511262.png
 
Watu 17 wamekwisha uawa mpaka sasa na majeruhi 21.

Inasemekana kuna ambao bado jamaa kawashikilia mateka.
 
Makomandoo wa kipolisi wamewasili katika eneo la tukio ili kutoa msaada wa kumkamata ama kumuua jamaa.

Ndani ya jengo kuna mamia ya watu na wanajeshi wamekwisha ingia ndani na kuwatoa baadhi ya waliokuwemo humo.
 
Idadi ya vifo imefikia 20. Jamaa bado anaendelea kuua.
 
Idadi ya waliouawa imefikia 21 hadi sasa huku wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa.

Hali bado ni tete, mtuhumiwa bado hajakamatwa.
 
Sajenti wa jeshi la Thailand aliyepandisha mori (berserk) ameuliwa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama baada ya kumuua afisa wake wa jeshi na askari mwenzake juu ya mzozo wa kifedha kisha akapiga risasi angalau 19 wengine katika "shopping mall" wakati huo huo akijipiga picha za "selfie" na kuzituma kwenye Facebook.

Soma zaidi...

 
Hawa wa Thailand walitumika sana Iraq ile vita na marekani walikua wakilipwa dola 33 per hour, inawezekana ni laana ya dam za watu inaanza kumtafuna

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh, pole zao au waliouliwa ni waislamu nini!!
 
Back
Top Bottom