Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 221
- 197
Ni matumaini yangu ulishawahi kusikia makundi mbalimbali ya vyakula kipindi unasoma elimu ya msingi. Ambapo ulijifunza kuwa kuna Kabohaidreti/wanga, protini, fati, vitamini na madini asilia.
Katika kundi la protini ulisoma kuwa, ni vyakula vinavyosaidia katika ukuaji wa mwili pamoja na kutengeneza kinga za mwili. mfano uliweza kuona vyakula kama vile nyama, maharage, samaki n.k.
Tafiti nyingi zinaonesha kuwa samaki imebeba virutubisho vingi ambavyo baadhi yake ni fati au mafuta yaitwayo (Omega-3- polyunsaturated fatty acids).
Mafuta haya ni muhimu zaidi katika ukuaji/afya ya ubongo (brain development) hivyo huongeza ufanisi wa ubongo katika utendaji kazi pia katika afya ya moyo ambapo husaidia kupunguza magonjwa mbalimbali ya moyo.
Ili kupata virutubisho hivyo ni lazima utumie njia thabiti ambayo ni "Uokaji" au "Uchemshaji" wa samaki suala ambalo ni mtihani kidogo katika jamii zetu. Kwa kufanya hivyo utaweza kuvuna virutubisho hivyo pamoja na virutubisho vya Vitamini D.
Je! Mimi na wewe tunatumia njia gani hasa katika uandaaji wa Samaki kabla ya kumtia kinywani?
Hata kama unakula kwa mama n'tilie unaweza kujiunga na mdahalo huu pia.