Thamani/umuhimu wa watu.

Thamani/umuhimu wa watu.

Hivi umeshawahi kufikiria siku utakayoamka unajikuta upo peke yako nyumba nzima, njiani hukuti mtu, unafika kwenye kituo cha daladala magari yapo ila hakuna mtu, ofisini napo hukuti mtu.
Unajihisi mpweke unaamua uwapigie simu watu wako ila Simu zinaita hazipokelewi. unafungua JF unakuta threads kibao ila hakuna mtu online.
Unagundua kuwa umeachwa mwenyewe hapo ndipo unaanza kuona umuhimu wa watu.

Umuhimu wa watu huonekana pale tunapowakosa ila hatutakiwi tusubiri hadi tuwakose ndio tuoneshe kuwa wao ni muhimu kwetu.
Wana jf wote ni muhimu kwangu na ninawapenda sana, sitaki kusubiri hadi niwakose ndio mjue mlikuwa muhimu kwangu.
Nawatakia siku njema na mungu awabariki.

Kuna nini hapa wapendwa, am back now
 
Kila mtu anahitaji mtu/watu. Mara nyengine tunakuwa tumeshughulika sana kiasi hatujali umuhimu wa hawa watu. Unaamka, unaenda kazini/chuoni, unarejea nyumbani umechoka, unakoga na kulala. Kitandani unawaza, loh, "nilipaswa kumpigia au kumpitia fulani", lakini saa nyingi, "nitafanya kesho". Kesho ikifika inakuwa leo na leo ilikuwa kama jana. Siku zinaenda... Ukitahamaki unawapoteza mmoja mmoja. Upweke (to be alone) uliokuwa unautaka kwa shughuli zako unageuka na kukufanya ujikute na ujisikie mpweke (to feel lonely).

Wana JF, kama jamii, tuna bahati ya kukutana hapa na kubadilishana mawazo, kusalimiana, kutaniana, kuudhiana, kusameheana. Ndio maisha! Tuwapende, tuwaoneshe upendo, tuwambie kuwa tunawapenda watu wetu na ni muhimu kwetu kabla hatujachelewa. Kazi ni muhimu, lakini maisha ni muhimu zaidi. na maisha ni kuwa pamoja na watu.

Binafsi JF ni familia yangu ya pili. Kwa mimi nyote ni muhimu kwangu na nisingependa kuwakosa wala kuwapoteza. NINAWAPENDA NYOTE. Mubarikiwe.
 
True kabisa Husninyo, Mungu akubariki kwa kutukumbusha
 
Hivi umeshawahi kufikiria siku utakayoamka unajikuta upo peke yako nyumba nzima, njiani hukuti mtu, unafika kwenye kituo cha daladala magari yapo ila hakuna mtu, ofisini napo hukuti mtu.
Unajihisi mpweke unaamua uwapigie simu watu wako ila Simu zinaita hazipokelewi. unafungua JF unakuta threads kibao ila hakuna mtu online.
Unagundua kuwa umeachwa mwenyewe hapo ndipo unaanza kuona umuhimu wa watu.

Umuhimu wa watu huonekana pale tunapowakosa ila hatutakiwi tusubiri hadi tuwakose ndio tuoneshe kuwa wao ni muhimu kwetu.
Wana jf wote ni muhimu kwangu na ninawapenda sana, sitaki kusubiri hadi niwakose ndio mjue mlikuwa muhimu kwangu.
Nawatakia siku njema na mungu awabariki.

Wana JF wenzangu, mnaonaje kama siku moja moja kila mmoja wetu akaamua kutuma sms kwa watu wote ktk phonebook ya simu yake ili yaende sambamba na maneno ya Husninyo???
Siku hizi kuna Extreme za msg kwa bei ndogo tu, so tunaweza kufanya
 
Spanish lady asante sana,nawe ni muhimu sana kwetu.
 
Kazi ni muhimu, lakini maisha ni muhimu zaidi. na maisha ni kuwa pamoja na watu.

kweli mkuu, tunawasahau ndugu na jamaa kisingizio kazi.
Tunashindwa hata kwenda kuwaona japo tunataarifa kuwa wamelazwa.
Wakishatutoka tunalia sana wakati hatukuonesha kujali.
 
Wana JF wenzangu, mnaonaje kama siku moja moja kila mmoja wetu akaamua kutuma sms kwa watu wote ktk phonebook ya simu yake ili yaende sambamba na maneno ya Husninyo???
Siku hizi kuna Extreme za msg kwa bei ndogo tu, so tunaweza kufanya

hivi hufanyagi hivyo??
Anza sasa.
 
Daaah
Shem nimekuelewa mbona, yaani mpaka raha
Nimeshatoa propozo langu hapo juu Shem
Nilienda loliondo shem:wink2:

hujaniletea japo kaglass ka yale maji.
Nimeona propozo shemeji ila binafsi kuna watu lazima niwasiliane nao daily, wengine weekly, monthly. Kifupi huwa siwasahau
 
Nakusifu sana nilipoanza kukusema ulikuwa na 4 mpaka hapo unaendelea vizuri sana,ni msikivu ndio maana nataka kuja Mpwapwa lol!

ha ha ha ha! Lol!
Usipate shida uporoto wangu, nitakufata popote ulipo.
Milima nitapanda, mabonde nitashuka, bahari nitavuka.. Misituni nitapita....
 
Dah! maneno matamu sana ingewezekana ningekugongea thanks 100,leo ntalala vizuri sana asante my angel.
 
Back
Top Bottom