Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Moja kati ya mambo ninayomiss sana kuhusu my home town MWANZA A.K.A. THE ROCK CITY ni Samaki.Samaki wanaopatikana ziwa Victoria wana sifa kubwa sana kitaifa na kimataifa.Ukiishi mikoa ya
kanda ya ziwa huwezi jua thamani ya samaki hao adi utoke nje ya mkoa uwakose kwa muda.
Samaki wa maji baridi si kama wa maji chumvi,wanatofautiana ladha na zaidi ya yote wanatofautiana
aina na wingi wa virutubisho.Samaki kwa ujumla ni chanzo kikubwa cha protini na madini mwili,samaki wa maji baridi wana Omega -3 na fatty acids kidogo ukilinganisha na samaki wa maji chumvi,ata ivyo samaki
wa maji baridi ana protini nyingi na mafuta kidogo,pia anamadini mwili kama calcium,madini chuma pamoja na manganese.
Samaki hutumika kama kitoweo kwa chakula cha mchana na jioni kwa familia nyingi.Kwa wakazi wa maeneo ya ziwani samaki huliwa ata asubuhi kama kifungua kinywa kwani hupatikana kwa wingi katika maeneo hayo.
Kichwa cha sangara kina sifa ya kutoa supu au mchuzi mzito,kina mafuta na kwa ujumla ni kitamu.
Kwa miaka mingi kumekua na imani iliyojengeka kwenye makabila ya kanda ya ziwa kwamba ukila kichwa cha samaki unakua na akili nyingi.Watu wengi sana hawakubaliani na imani hii ata kidogo na mara nyingi
nimesikia watu wakiongelea vibaya au kutania juu ya imani hii.
Ukweli ni kwamba,imani yao ni ya kweli na inathibitika kisayansi.kichwa cha samaki hubeba asilimia kubwa ya madini na mafuta mengi kuliko sehem yoyote ya samaki ,mafuta hayo hubeba essential Fatty
acids(Omega -3 na omega-6) na madini mwili aina ya calcium,madini chuma,manganese.Madini haya pamoja na assential fatty acids ni virutubisho muhim sana katika ujenzi na ukuaji kwa ubongo.kilakirutubisho kina kazi yake maalum.Hivyo kwakua wakazi wa kanda ya ziwa hupata virutubisho
hivyo kwa wingi basi ubongo wao hukua vizuri na kuwapa uwezo wa kua na akili zaidi.
Ni vyema kujua kwamba ukuaji wa Ubongo wa mtoto huwa katika kiwango cha juu kabisa ndani ya miaka
miwili ya kwanza ya maisha ya mtoto,hata ivyo virutubisho hivi na vingine vingi huendelea kua muhim katika utendaji na ukuaji wakilasiku wa ubongo.Kwa upande mwingine Akili hukua na kuongezeka sawasawa na akuavyo mtoto.kumbuka tu,endapo ubongo wake ulikua vizuri na unapata virutubisho muhim
ili kuuwezesha kufanya kazi vizuri basi akili yake huwa na uwezo wa kukua na kupanuka kwa haraka zaidi.niishie hapa nisijeingilia fani ya madaktari
Nilipokwenda Mwanza kwa ajili ya christmass mwaka jana,sikufanya kosa,nilikula samaki kwa wingi,na nilianda,nikapika na kula kichwa cha sangara kwa hamu sana.Kuna namna na njia nyingi za kupika na kuanda kichwa cha samaki,nah ii ni namna moja wapo.
Mahitaji
- Kichwa cha sangara.kipasue vipande
- Maji
- Nyanya
- Kitunguu maji
- Kitunguu swaumu
- Limao au ndimu
- chumvi
Njia
1.Osha kichwa cha sangara vizuri,zingatia sana mashavu kwani hubeba uchafu mwingi
2.Weka samaki ndani ya sufuria zito,kisha ongeza maji adi yafunike samaki na kuzidi kidogo.
3.kisha ongezamvitunguu maji,vitunguu swaumu,nyanya na chumvi kisha bandika jikoni vichemke kwa muda mrefu na kwa moto wa wastani.moto ukiwa mkali hutapata mchuzi au supu nzuri na wakati kinatokota kichwa kitameguka meguka.
4.Chemsha adi kiive,kisha ongeza limao kabla tu ya kuepua .kama ni kwa ajili ya mtoto usiongeze limao,ila mpe juice ya chungwa baada ya kula mlo wenye samaki.
Wingi wa supu au mchuzi ni chaguo la mpishi,kama unataka supu/mchuzi mwepesi basi hakikisha
umeweka maji mengi zaidi unapoanza kuchemsha,ni vyema upima maji ya kutosha unapoanza kuchemsha ili uepuke kuongeza maji baada ya kuchemka,maji ya nyongeza siku zote huaribu ladha na ubora wa supu na hata mchuzi.
Mambo ndio kama hivyo,Kichwa cha sangara tayari kwa kula,unaweza ukanywa supu yake na kula kichwa bila kusindikiza na chakula kingine,na ukipenda unaweza kutumia kama mboga au kitoweo.
Ipe familia yako chakula bora si bora chakula.

