Ridhiwan36
New Member
- Oct 27, 2018
- 2
- 2
Tumeaminishwa kwa kipindi kirefu sana juu ya umuhimu wa kijana katika taifa linaloendelea. Tumeambiwa kuwa kijana ni nguvu ya taifa la sasa na lijalo, na kuwa ni juu ya kijana kuendeleza taifa lake. Zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ni wa umri chini ya miaka 45, nchi hii imejaaliwa vijana wengi mno wa sasa na wa baadae. Ni kwa namna ipi hatuoni hayo maendeleo ambayo yanatakiwa kuletwa na vijana? Je, ni kila kijana anaweza kuleta maendeleo kwenye taifa? Au je, si kweli kwamba kijana ni muhimu katika ujenzi wa Taifa? Haya ni maswali ambayo inafaa kujiuliza kila ambapo kauli mbiu ya umuhimu wa vijana ikitamkwa kwenye makumbi, mihadhara na mitandaoni.
Tuanze kwa kupitia nini kinamaanishwa likisemwa neno vijana. Vijana ni watu wenye miaka kati ya 15 mpaka 45 na hii hubadilika kutokana na nchi au bailojia ya watu husika. Vijana ni watu waliomaliza utoto na sasa wanaweza kuchanganua mambo kadhaa katika maisha, kubaini zuri na baya, kutii sheria, kufanya kazi na kuchangia katika uchumi wa majumbani kwao, jamii zao na taifa lao. Maana hii hujumuisha wanaume na wanawake ingawa katika mataifa ya kiafrika yenye mfumo dume, basi vijana hulenga zaidi wanaume wenye sifa zilizotajwa hapo awali haswa akihusishwa na ujenzi wa familia na utafutaji wa mali. Haitakuwa maana kamili bila kutambua mzee na mtoto ni nani, na kipi kinawatofautisha na kijana. Kwa ufupi mzee ni yule aliyepita umri wa miaka 45 na mchango wake kwa familia, jamii na taifa unaelekea ukingoni, mtoto ni yule aliye chini ya miaka 15 ambaye yupo katika mafunzo ya kumfanya awe kijana wa siku zijazo na ni tegemezi kwa vijana na wazee kwa mahitaji yake ya kila siku. Tunaweza kuona kutokana na maana hii ya vijana ni kwanini yeye hutajwa kama mjenzi mkuu wa taifa la leo na la kesho. Vijana wametangulizwa kwenye vita ya maendeleo wapigane bila kuchoka kwa miaka zaidi ya 30 ya maisha yao.
Tukiweka nchi au taifa katika mfano wa chombo cha moto basi injini ya taifa hilo ni vijana. Injini ya chombo cha moto itaundwa kiwandani kwa matumizi husika na matumizi yake yakibadilishwa au kukiukwa basi injini hiyo haiwezi kuleta matokeo yanayotegemewa kwenye chombo cha moto. Injini yako ukiipa mafuta ambayo hayajaelekezwa kiwandani basi nguvu yake hupungua au kuharibika kabisa. Vijana nao huundwa na taifa lao na hutengenezwa kwa malengo husika ya taifa. Kwahiyo ni kweli kwamba sio kila kijana anaweza kuleta maendeleo kwenye taifa sababu ni wale tu, walioundwa na kuandaliwa na taifa ndo wataweza kuleta mchango. Taifa linalomuunda kijana linajumuisha familia, majirani, jamii na serikali ya nchi. Taifa la Tanzania linaunda vipi vijana wao? Taifa letu vijana huundwa kupitia malezi ya asili yenye kufundisha tabia njema, nidhamu na heshima kwa wote, ukiona tabia za vijana hazieleweki basi ujue ngazi ya jamii katika taifa imelega na kushindwa kufanya wajibu wao wa kuunda vijana. Taifa letu vijana hutengenezwa kwa kupewa elimu ya msingi mpaka chuo kikuu, ili wapate maarifa na ujuzi wa mambo na kuleta uvumbuzi na suluhu kwenye changamoto zinazolikabili taifa, ukiona vijana hawafanyi haya basi ujue ngazi ya serikali imelega na kushindwa kufanya wajibu wao kikamilifu wa kutengeneza vijana. Ukiangalia vijana wengi leo ,utaona kuwa tabia na nidhamu zao sio za kuridhisha kwa kiwango kikubwa na uwezo wao pia wa uvumbuzi wa suluhu kwenye changamoto za kila siku ni mdogo. Kuna mfumo ulijitokeza na kujipandikiza katika ngazi zote za jamii na serikali ambao umepelekea vijana hawa kufikia hapa. Huwezi kuilaumu injini kutokuwa na nguvu baada ya kuijaza mafuta yasiyokuwa yake.
Thamani ya kijana ni kubwa mno katika taifa kutokana na maana ya kijana lakini uhalisia wa thamani ya kijana umeshuka kutokana na aina ya vijana waliotengenezwa na taifa letu. Ndio maana vijana wengi hushindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu wakipewa nafasi za kujishughulisha na kuchangia jamii. Na wale ambao hunyimwa nafasi basi huona kuwa wazee ndo hawataki wapate nafasi, wakati wazee wanaona kuwa vijana hawawezi kazi. Ni vuta nikuvute ambayo haina mwisho mwema kwa vijana, wazee wala taifa. Kiujumla hatujatengeneza vijana kwa ajili ya haya majukumu tunayotaka kuwapa ndani ya taifa, hatujawaunda vijana kwa ajili ya taifa la leo na la kesho. Lakini hili kosa ni kosa linalorekebishika kwa kugeuza meza na kuanza kuwathaminisha vijana wa sasa na kuwaandaa watoto kuwa vijana bora na mahiri. Ni kivipi tunaweza kuwapa thamani husika vijana wa sasa?
Vijana wanaweza kurudishiwa thamani yao kwa kupewa kipaumbele katika maendeleo ya taifa, kipaumbele sio kuwapa pesa au mikopo sababu hawajui namna ya kutumia hizo pesa kujiendeleza kwakuwa hawakuandaliwa kwa hayo, na pia hakuna pesa au mikopo ya kuwatosha vijana hata asilimia 10 tu ya taifa letu. Vijana wote huwezi kuwapa ajira lakini unaweza kuwapa kazi, nchi yetu inahitaji vitu vingi sana kuimarika na waimarishaji ni vijana. Vijana waelekezwe kulikopesha taifa nguvu kazi yao kwa malipo ya baadae, siku zote anayekukopesha utamuheshimu na kumpa thamani kubwa kwa msaada wake. Jamii na serikali ifahamu thamani hiyo ya vijana na kuwapa heko kwao kwa kuliendesha taifa kipindi halina uwezo wa kuwalipa stahiki zao. Tukisubiria vijana wachangie taifa kwa kufanya kazi za malipo pekee basi ni vijana wachache mno watajihusisha na maendeleo kwasababu pesa ni chache na pia wanaostahiki au wanaokidhi vigezo ni wachache. Mkopo wa nguvu kazi wanaoutoa vijana utarekodiwa na kulipwa baadae kama pesa, bima mbalimbali, kupunguziwa kodi, uongozi katika jamii n.k.
Kiujumla vijana wote ni lazima waipate thamani yao kupitia maana ya wao kuitwa vijana, lazima wajihusishe na wahusishwe kikamilifu katika shughuli zote za maendeleo ya nchi, iwe kwa malipo au kwa mkopo wa nguvu kazi watakayoitoa kikamilifu. Mthaminishe kijana kwa ujenzi wa taifa la leo na la kesho.

Upvote
3