The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na mamilioni ya watu katika Afrika na kote duniani. Ingawa Kiswahili kimeonekana kupanda chati na kuonekana kuzidi kushika kasi leo, lakini lugha hii ilshapata heshima tangu zamani. Wasanii na watu maarufu walitamani kuizungumza wakiwa na fikra kwamba Kiswahili ndiyo lugha pekee ya Kiafrika inliyozungumzwa na Waafrika wengi, lakini wengine nje ya bara walidhani ni Waafrika wote wanaifahamu.
Leo katika ulimwengu wa burudani duniani, lugha hii imepata kutumika sana. Katika ulimwengu huu, Kiswahili kimehusishwa sana na utamaduni wa Afrika.
Hivi karibuni mwanamama msanii wa Kimarekani Beyonce alitoa wimbo ambao umebeba maneno ya Kiswahili. Kibao hicho kinaitwa Spirit. Kinachosikika katika wimbo huo ni sauti isemayo "Uishi kwa muda mrefu mfalme," huku sauti nzito ikiitikia "uishi kwa". Ni sehemu ndogo tu ya wimbo, alafu unaendelea kwa lugha ya Kiingereza.
Sasa hili la Beyonce ni la juzi tu ambalo huenda ndilo lililowafumbua wengi (wa kizazi hiki) macho kuhusu umaarufu wa Kiswahili. Lakini kiukweli hii lugha ilianza kuthaminiwa tangu kitambo, tena na wasio hata wazawa wa bara hili. Tutakuwa na uzi maalumu katika upande burudani ya kimataifa na Kiswahili.
Huko duniani, hususan Amerika ya Kaskazini na Carribean, wanaharakati, wasomi na wanamuziki wenye mirengo ama nia njema dhidi ya mawazo, falsafa, mitazamo na tamaduni za Kiafrika wamekuwa wakitumia lugha hii kwa aidha kujipa majina ama kuanzisha taasisi au makundi yaliyopewa majina ya Kiswahili.
Kwa mujibu wa gazeti la Omaha World-Herald la huko Jijini Omaha katika jimbo la Nebraska, ni kwamba tangu miaka ya 1960, wazazi wengi wa Marekani wenye asili ya Afrika wamekuwa wakiyageuza maneno ya Kiswahili kuwa majina na kuwapa watoto wao. Baadhi ya majina hayo hayatumiwi kama majina na wenyeji katika Afrika Mashariki.
Leo nitatoa mifano michache ya majina ya watu au makundi maarufu ambayo kwa namna moja au nyingine, Kiswahili kimehusika ndanimwe.
Taraji ni Maarufu kupitia filamu nyingi zikiwemo Karate Kid (2010), Think Like a Man (2012), Hidden Figures (2016), What Men Want (2019) na ile series maarufu sana ya Empire ambamo anafahamika kama Cookie.
2. SANAA LATHAN
Huko New York nchini Marekani, mnamo mwaka 1971, alizaliwa binti ambaye wazazi wake waliamua kumpa jina Sanaa. Mama yake Sanaa, Eleanor McCoy, kwa makusudi aliamua kumpa mwanaye jina hilo la Kiswahili kwani naye alikuwa ni mnenguaji na mwigizaji. Kama tunavyoamini wengi, jina la mtu linaweza kuakisi maisha yake. Baadaye alikuwa muigizaji mkubwa tukamwona kwenye filamu kama vile Blade (1998), Life (1999), The Best Man (1999), The Family That Preys (2008), American Assassin (2017) n.k
Talib amempa mmoja kati ya watoto wake jina la Kiswahili pia, amemuita Amani.
Kwa kutambua bidi yake, Amani alichaguliwa kama Man of the Year na timu yake mwaka 2003. Pia ametambuliwa kwa heshima mbalimbali kutokana na ushiriki wake katika masuala ya kijamii.
Black Uhuru wameshinda tuzo moja ya Grammy na kuteuliwa kuiwania mara nane.
Mnamo mwaka 1998, Baraka alishirikishwa kwenye albamu ya mwimbaji Lauryn Hill iliyoitwa The Miseducation of Lauryn Hill.
Ras Baraka pia ana mtoto aliyempatia jina la Kiswahili, Jua.
Amiri alikuwa ni mwanazuoni na mwandishi wa vitabu vingi vya ushairi na alifundisha katika vyuo vikuu kadhaa, ikijumuisha Chuo Kikuu cha Jimbo la New York huko Buffalo na Stony Brook. Mnamo 1967, pia alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jimbo la San Francisco.
Mnamo 1966, Baraka alioa mke wake wa pili, Sylvia Robinson, ambaye baadaye naye alijipa jina la Amina Baraka.
Ellis alijiunga na NBC News kama ripota wa habari. Kabla ya kujiunga na NBC News alifanya kazi katika vituo kadhaa vya runinga ikiwemo KDKA-Tv na Redio huko Pittsburgh, Pennsylvania.
Mnamo 1966 alijiunga na taasisi ya US Organization au Organization Us, kikundi cha uwezeshaji wa watu weusi kilichokuwa mpinzani wa Black Panther Party. James Forman alipokea jina lake, ambalo ni tafsiri ya neno la Kiingereza messenger, yaani "mjumbe" kwa Kiswahili, kutoka kwa Maulana Karenga ambaye aliwapatia wanachama wa taasisi hiyo majina ya kufanana na tabia zao.
Alizaliwa huko Parsonsburg, Maryland, nchini Marekani kama Ronald McKinley Everett.
Baada ya kupata digrii yake katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA) na kuhitimu shahada ya Uzamili katika sayansi ya siasa, alisoma Kiswahili, Kiarabu na masomo mengine yanayohusiana na Afrika. Katika kipindi hiki alijipa jina Karenga (neno la Kiswahili linalomaanisha "mtunza mila") na la kwanza akajiita Maulana (Kiswahili cha asili ya Kiarabu kinachomaanisha "mwalimu mkuu au mwalimu wa juu zaidi").
Hayo ni baadhi tu yanayohusisha watu maarufu. Naamini wapo wengi zaidi wasio maarufu. Kiswahili na utamaduni wake unatukuzwa na kupendwa kote duniani. Tuendelee kuitukuza lugha yetu.
Leo katika ulimwengu wa burudani duniani, lugha hii imepata kutumika sana. Katika ulimwengu huu, Kiswahili kimehusishwa sana na utamaduni wa Afrika.
Hivi karibuni mwanamama msanii wa Kimarekani Beyonce alitoa wimbo ambao umebeba maneno ya Kiswahili. Kibao hicho kinaitwa Spirit. Kinachosikika katika wimbo huo ni sauti isemayo "Uishi kwa muda mrefu mfalme," huku sauti nzito ikiitikia "uishi kwa". Ni sehemu ndogo tu ya wimbo, alafu unaendelea kwa lugha ya Kiingereza.
Sasa hili la Beyonce ni la juzi tu ambalo huenda ndilo lililowafumbua wengi (wa kizazi hiki) macho kuhusu umaarufu wa Kiswahili. Lakini kiukweli hii lugha ilianza kuthaminiwa tangu kitambo, tena na wasio hata wazawa wa bara hili. Tutakuwa na uzi maalumu katika upande burudani ya kimataifa na Kiswahili.
Huko duniani, hususan Amerika ya Kaskazini na Carribean, wanaharakati, wasomi na wanamuziki wenye mirengo ama nia njema dhidi ya mawazo, falsafa, mitazamo na tamaduni za Kiafrika wamekuwa wakitumia lugha hii kwa aidha kujipa majina ama kuanzisha taasisi au makundi yaliyopewa majina ya Kiswahili.
Kwa mujibu wa gazeti la Omaha World-Herald la huko Jijini Omaha katika jimbo la Nebraska, ni kwamba tangu miaka ya 1960, wazazi wengi wa Marekani wenye asili ya Afrika wamekuwa wakiyageuza maneno ya Kiswahili kuwa majina na kuwapa watoto wao. Baadhi ya majina hayo hayatumiwi kama majina na wenyeji katika Afrika Mashariki.
Leo nitatoa mifano michache ya majina ya watu au makundi maarufu ambayo kwa namna moja au nyingine, Kiswahili kimehusika ndanimwe.
Baadhi ya watu maarufu wenye majina au waliojipa majina ya Kiswahili
1. TARAJI PENDA HENSON
Mnamo mwaka 1970, Wakazi wa huko Washington, D.C., Marekani Bernice na Boris Henson walimpa binti yao jina la Taraji Penda. Kwa Kiswahili, taraji ni kutumai au kwa maana iliyomaanishwa na wazazi wake ni "tumaini" na penda wakimaanisha "upendo".1. TARAJI PENDA HENSON
Taraji ni Maarufu kupitia filamu nyingi zikiwemo Karate Kid (2010), Think Like a Man (2012), Hidden Figures (2016), What Men Want (2019) na ile series maarufu sana ya Empire ambamo anafahamika kama Cookie.
2. SANAA LATHAN
3. TALIB KWELI GREEN
Talib ni amezaliwa Brooklyn, New York. Mwanamuziki huyu wa Hip Hop ambaye pia ni mjasiriamali na mwanaharakati alizaliwa mnano mwaka 1975. Jina lake la Kwanza, Talib, ni na asili ya Kiarabu likiwa na maana “mwanafunzi” (student) au “mtafutaji” (seeker). Jina lake la pili ni la Kiswahili, Kweli. Hivyo maana halisi ya jina lake ni Mtafuta Ukweli, yaani kwa Kimombo Truth Seeker. Akiwa mdogo Talib alivutiwa sana na wanamuziki wa Kimarekani waliokuwa wakihusudu asili na mitazamo ya watu weusi kama vile De La Soul, The Tribe Called Quest na Jungle Brothers.Talib amempa mmoja kati ya watoto wake jina la Kiswahili pia, amemuita Amani.
4. ZURI HALL
Zuri ni mtangazaji maarufu wa televisheni nchini Marekani, akiwa amejikita zaidi katika upande wa burudani. Zuri alizaliwa Toledo huko Ohio mnamo Juni 2, 1988. Wazazi wake walimpa jina hilo likiwa ni tafsiri ya Kiswahili ya neno “beautiful”. Wale wapenzi wa burudani, urembo na udaku mtakuwa mmewahi kumuona kupitia E! News, The Challenge ya MTV, na wakati fulani kupitia 106 & Park ya BET.5. AMANI ASKARI TOOMER
Amani alikuwa mchezaji wa American Football akiwa na timu yake ya New York Giants inayoshiriki National Football League (NFL). Amani alizaliwa huko Berkeley, California.Kwa kutambua bidi yake, Amani alichaguliwa kama Man of the Year na timu yake mwaka 2003. Pia ametambuliwa kwa heshima mbalimbali kutokana na ushiriki wake katika masuala ya kijamii.
6. BLACK UHURU
Black Uhuru ni kikundi cha muziki wa reggae kilichoundwa nchini Jamaica mnamo 1972, mwanzoni kikijulikana kwa jina la Black Sounds Uhuru. Kikundi kilijumuisha majina makubwa kama vile Garth Dennis, Don Carlos, na Derrick "Duckie" Simpson. Kundi hili lilijumuisha neno Uhuru katika jina lao kwa kusudi maalum kwani ni kikundi ambacho kilifanya muziki wa Roots Reggae, muziki ambao unahubiri fahari ya ngozi nyeusi na Afrika kama nyumbani kwa watu weusi wote.Black Uhuru wameshinda tuzo moja ya Grammy na kuteuliwa kuiwania mara nane.
7. RAS JUA BARAKA
Ras Baraka ni mwalimu, mwandishi, na mwanasiasa ambaye ni Meya wa 40 wa sasa wa Newark, New Jersey, mji ambao ndiyo alipozaliwa mnamo mwaka 1970.Mnamo mwaka 1998, Baraka alishirikishwa kwenye albamu ya mwimbaji Lauryn Hill iliyoitwa The Miseducation of Lauryn Hill.
Ras Baraka pia ana mtoto aliyempatia jina la Kiswahili, Jua.
8. AMIRI BARAKA
Huyu ni baba mzazi wa Ras Jua Baraka na ndiye aliyempatia mwanawe jina hilo. Amiri alizaliwa mnamo mwaka 1934 na kupatiwa jina la Everett LeRoi Jones, ambalo aliamua kulibadilisha baadaye na kujipa jina la Kiswahili.Amiri alikuwa ni mwanazuoni na mwandishi wa vitabu vingi vya ushairi na alifundisha katika vyuo vikuu kadhaa, ikijumuisha Chuo Kikuu cha Jimbo la New York huko Buffalo na Stony Brook. Mnamo 1967, pia alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jimbo la San Francisco.
Mnamo 1966, Baraka alioa mke wake wa pili, Sylvia Robinson, ambaye baadaye naye alijipa jina la Amina Baraka.
9. REHEMA ELLIS
Rehema Ellis ni mwandishi wa habari wa TV nchini Marekani. Alizaliwa mnamo 1954 huko Kaskazini mwa jimbo la Carolina na kukulia huko Boston, Massachusets. Kwa sasa anafanya kazi NBC News.Ellis alijiunga na NBC News kama ripota wa habari. Kabla ya kujiunga na NBC News alifanya kazi katika vituo kadhaa vya runinga ikiwemo KDKA-Tv na Redio huko Pittsburgh, Pennsylvania.
10. JAMES MTUME
James Mtume ni mwanamuziki wa jazz, RnB, mtayarishaji wa nyimbo mwanaharakati na mtangazaji wa redio. Mtume alizaliwa mnamo mwaka 1943 kama James Forman.Mnamo 1966 alijiunga na taasisi ya US Organization au Organization Us, kikundi cha uwezeshaji wa watu weusi kilichokuwa mpinzani wa Black Panther Party. James Forman alipokea jina lake, ambalo ni tafsiri ya neno la Kiingereza messenger, yaani "mjumbe" kwa Kiswahili, kutoka kwa Maulana Karenga ambaye aliwapatia wanachama wa taasisi hiyo majina ya kufanana na tabia zao.
11. MAULANA NDABEZITHA KARENGA
Ni mwanaharakati, mwandishi, na muumini wa Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism) ambaye pia anajulikana kwa kuwa muanzilishi wa sikukuu ya Kwanzaa, ambayo inahamasisha kusherehekea historia ya mtu mweusi badala ya kushikilia, kuenzi na kufuata mienendo ya tamaduni za kigeni.Alizaliwa huko Parsonsburg, Maryland, nchini Marekani kama Ronald McKinley Everett.