Hutaki kulipa tozo na Kodi halafu unataka maendeleo, kwa Taarifa yako ni kuwa mataifa unayooona yameendelea yalipitia njia hii tupitayo, walitozana Kodi kuzijenga nchi zao, walijifunga mikanda ili kuijenga kesho yao iliyo Bora
Njia ya kupata maendeleo siyo mteremko Wala Tambalale Wala mtelezo, Ni Kama dawa chungu ambayo ukimaliza kuinywa unapona, Sasa hatuwezi tukasema usinywe dawa kwa kuwa Ni chungu wakati tunajuwa hutapona, hii ndio dawa ya kuondoa umaskini, ndio dawa ya kuijenga nchi yetu ikapendeza na kuwa ya mfano
lazzima tujifunge mikanda, lazima tujibane kidogo, lazima tupunguze kidogo katika vipato vyetu ili kupeleka katika kuijenga Tanzania yetu tutakayo jivunia sote