Thamani ya Mwanamke katika jamii

Thamani ya Mwanamke katika jamii

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
1732304547531.jpg
THAMANI YA MWANAMKE KATIKA JAMII.

Mwanamke amekuwa nguzo muhimu sana ndani ya familia pale ambapo mwanaume anakuwa hajui wajibu wake ndani ya famili ,

Hii imekuwa ina tokea katika nyakati tofauti Tofauti , inafikia Time hadi mwanamke anapambana kuhudumia familia kwa kutafuta chochote kitu ili tu watoto wapate ata mlo mmoja kwa siku,ni wazi kuwa wanaume wamekuwa wakitoroka majukumu yao ndani ya familia,hii inapelekea mama kupambania watoto kwa nguvu zake zote ili tu watoto wapate mlo waione kesho yake.Mwanamke amekuwa akipambana na changamoto nyingi sana kuipambania familia hasa watoto pale tu baba akiwa amekata tamaa kuwajibika.

Mfano
.. sikiliza wimbo wa solid ground family nyimbo inaitwa " Baba jane"
Hii ni nyimbo yenye ujumbe ambao ndio kwa % 75 wanawake wengi katika familia zao , wamekuwa wakipitia changamoto hizi, na mara nyingi ama mara zote ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na lifestyle ama matukio kama haya.

Ndio maana mtaani kuna Ongezeko kubwa sana la ma single mother.

Jambo ambalo linampa wakati mgumu sana mtoto kulelewa na mzazi mmoja, inshu sio mambo ya kiuchumi hapana !! Mtoto anaweza Akawa anapata huduma zote muhimu naza msing kutoka kwa mama yake. Vitu kama vile mavazi, chakula & Elimu lakini kitu kitakacho miss na cha muhimu kwa mtoto ni malenzi ya baba ( upendo) ..

Kwa mtazamo wangu naona malenzi ya upande mmoja huwa hayamjengi mtoto kiakili,..

.. Crew ya Wachuja nafaka waliamua kutoa wimbo wao unaitwa " Dingi" wakimueleza baba yao kuwa vitendo vya kumpinga mother sio fresh..

Pia marehemu mandojo na rafiki yake domokaya walitoa wimbo unaitwa "Dingi" pia hii nyimbo ilizingumzia vituko na kadhia ya mzazi wa kiume ambaye ni Baba anavyoondoa Amani na upendo katika familia yake, kwa sababu ya vituko vyake..

Juhudi hizi za wanawake kuhusishwa na kufanya kazi
kwa ufanisi zimeonwa na msanii wa nyimbo za Zainab Lipangile a.k.a " Zay B" katika wimbo wake Mama Afrika. Msanii huyu anasikika akisema:

... Mimi mama Afrika, Sauti yangu nasikiika, Afrika x 4
Mama Afrika, Nafasi nashika, Machoni pa watu, Nakubalika/
natetea wanawake wa Kiafrika/ Kimawazo kamwe sitafilisiKa/
watoto wa kike wanabakwa kwa ajili ya pipi pipi na ofa/...
... Mimi mama Afrika, Sauti yangu nasikiika/ Afrika x 4
Tumeumbika ulimwengu mzima tunakubalika/
Tunasikitishwa na wasichana wa Kiafrika/
Siku zinavyozidi wanazidi kuharibika,
Sitosita kuwaelimisha ...

Lakini msanii Ay pamoja na msanii stan boy nao hawakuwa nyuma katika hili nao walitoa nyimbo yao inaitwa " madem watafutaji"

CHORUS:
hii ni kwa wote mademu watafutaji,
hii ni kwa wote mademu watafutaji,
zidisha nguvu kwenye kazi, watafutaji,
sasa nasema nao nyie, watafutaji,
zidisha nguvu kwenye kazi, watafutaji.
sasa nasema naooooo

VERSE 01: (Ay)
unavutia si kicheche halafu unanukia kinoma/
unahangaikia maisha yako nakukubali nikikuona/
ngoja sifa nikupe ila usiniangushe, ngoja sifa nikupee/
huchezi mahepe,huna matata, huna mapepe/
ukiwa na mashaka,silent nikupate kama alivyo mashaka/
silencer nikubusu mpaka uamue kusogea/
huyu demu ana misimamo kama Magret/
kila saa anawaza kutafuta peeeesa/
alishawastukia wote wale wanaomzukia/
ofa kibao ameshapewa ye kapuuzia/
alishadanganywa na mamen kibao/
lakini ameshastuka leo wotehawana chao/
hajajitumbukiza kwenye umalaya/
wala kuvuta kaya/
wala kufanya hata mambo mabaya/
hategemei za dingi/
ka-struggle miaka mingi/
na si kwamba kapata mshefa kamuingiza king/
bado unalipa kifaa,simama imara/
kimsimamo kama Mama Getruda Mongela/
wewe ndio mwanamke wa shoka, hujachoka/
bado unadai, unaweza ukawa Oprah au Mama Wangai Mathaaaaiiiiiii

Ushauri..

"Ni wakati sasa wanawake kuanza kujitegemea na kuanza kufanya kazi kwa bidii ndani ya familia. Hapa ni kuangazia wajibu wa mwanamke katika familia na hata jamii husika. Kila fursa inayotokea mwanamke asibaki nyuma na kuanza kumtegemea mwanaume atafanya, baadhi ya wanawake wamekuwa wakitegea kuwa ni lazima mwanaume awajibike kwa kila nafasi lakini si wanaume wote watakuwa na mtazamo wa kuwajibika vyema, hii inawafanya wanawake wazembee katika fursa wakijua ni lazima mwanaume awajibike kwa kila kitu, kwa muda mwingi wanawake wanakuwa hawataki kujituma na mwishowe hushindwa kuendesha biashara pindi tu mwanaume amefariki..

#funguka..

Onyesha upendo kwa kina mama wote ! coz hakuna kama Mama.

Enjoy playlist hii.

Banana zoro - mama
Vick kamata - wanawake na Maendeleo
AY & stan boy - wanawake watafutaji
Ngwea ft mwana fa & lady jay dee - sikiliza.
Zay b - mama Africa.

Ukwaju wa kitambo
0767542202. 📞
 
Hiyo ngoma ya Vick Kamata naikubali kinomanoma. Asante Kwa kunikumbusha.
 
Back
Top Bottom