Thamani ya shilingi ya Tanzania inazidi kuporomoka. Tunaelekea wapi?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Kila kukicha shillingi ya Tanzania inazidi kuporomoka huku tuna Waziri wa Fedha mahiri, tuna Gavana wa Benki mahiri na wachumi mahiri. Leo fedha ya Tanzania inabadilishwa kwa Tshs. 2,675 kwa dollar moja kutoka Tshs.2,300 miezi michache iliyopita.

Siku za karibuni fedha ya Tanzani ilikuwa inabadilishwa kwa 1 ke(Kenya) = Tshs.16 na leo hii 1 ke(Kenya) = Tshs. 20.26. Ninajiuliza kama nchi tunaelekea wapi?

Ni vema Mhe. Rais akaliona hili na kuwabadili Mhe. Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki na kuwapangia majukumu mengine.

====

Pia soma: Kushuka kwa thamani ya shilingi, zigo lililomshinda Mwigulu kulielezea kiuchumi
 
👏👏👏
 
Shilingi ya Uganda vs Dola ni 3,800 na maisha yanaenda safi kabisa,2,675 ni nini?

View: https://twitter.com/UchumiForum/status/1801573821041848825?t=Ig7OOZ-Bs8hsG76ZG-RUHA&s=19
 
Uchumi wa bwana rameck maderu alosomea chuo cha nyerere pale kigamboni
 
ngoja nikupe mbinu moja ya kijeshi alafu next time usijichoshe kuwaza haya mambo
_muda mwingine wanashusha wenyewe serikali ili wakope madollars huko nje wakija kuyacovert huku wanakuwa na pesa nyingiiii zaidi. ambapo athari za kupanda kwa dollor dhidi ya tsh. inakuwa ni ndogo kiunchumi kuliko mpunga ulioingia nchini.
 
Unatolea mifano nchi ambazo currency iko chini halaf unaita “maisha yanaenda” , kwa hiyo just because maisha yanaenda huko na sisi huku tu relax , accept failure just because maisha yanaenda?
Tusichukue hatua yoyote because maisha yanaenda?
 
Unatolea mifano nchi ambazo currency iko chini halaf unaita “maisha yanaenda” , kwa hiyo just because maisha yanaenda huko na sisi huku tu relax , accept failure just because maisha yanaenda?
Tusichukue hatua yoyote because maisha yanaenda?
Huyo ndie mfano wa chawa wasio na akili yoyote kichwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…