Thamani ya shilingi ya Tanzania inazidi kuporomoka. Tunaelekea wapi?

Tatizo ni kuficha dollar, ila kiuhalisia haijashuka thamani kiasi hicho, maana bei ya kipande cha mhogo bado ni shs.100/= ile ile
 
Unatolea mifano nchi ambazo currency iko chini halaf unaita “maisha yanaenda” , kwa hiyo just because maisha yanaenda huko na sisi huku tu relax , accept failure just because maisha yanaenda?
Tusichukue hatua yoyote because maisha yanaenda?
Burundi,Rwanda Ina currency ya Juu kushinda Tanzania,wametuzidi nini?
 
Kenya kwa dollar vipi!?
 
Kwa hiyo mikakati yao ni kukopa pasipo kurudisha?
 
Shida ni hii...👇👇👇

Dollarization is the term for when the U.S. dollar is used in addition to or instead of the domestic currency of another country. It is an example of currency substitution. Dollarization usually happens when a country's own currency loses its usefulness as a medium of exchange, due to hyperinflation or instability.
 
Mwigulu alisema juzi kuna hatu wanapenda kuchukua ..ngoja tuone.

Na ndio maana Mama anakopa Sana...akienda akirudi anakuta nchi haina hela ..anaondoka Tena...anakopa Tena.
 
Tanzania hii hii ndio inaweza ikajishushia Tsh wakati kila kitu inanunua nje.
 
Vita na majanga ya kidunia pia vinachangia!!Ulimwengu umeendelea kupitia changamoto kubwa za kisiasa na kiasili ambazo zinaathiri uchumi wetu coz na sisi ni sehem ya ulimwengu!!!

Yatatulia hivi karibuni!
 
Mimi natumia exchange rate ya 3000 kupunguza maumivu, chochote ntachoagiza kwa USD natumia 3000.
 
Vita na majanga ya kidunia pia vinachangia!!Ulimwengu umeendelea kupitia changamoto kubwa za kisiasa na kiasili ambazo zinaathiri uchumi wetu coz na sisi ni sehem ya ulimwengu!!!

Yatatulia hivi karibuni!
Hivyo vita na majanga vimeiathiri Tz tuu hapo Kenya tu majirani mbona wasiathirike?!.
Pesa yetu dhidi ya Kenyan kwasasa inapumulia mashine, iko hoi ICU!.
 
Ongea polepole Chawa wake watakusikia - anaupiga mwingi adi unamwagika.
 
Na kuporomoka kwa sarafu yetu kuna impact kubwa sana kwenye ulipaji wa madeni yetu mana yapo quoted in USD na sisi mapato yetu ni madafu hivyo tunapohitaji kulipa lazima tubadili madafu kwenda USD so kunapokua hakuna stability ya currency utakuta kiasi hicho hicho cha USD kwa vipindi viwili au vitatu tofauti basi tunatumia madafu mengi zaidi na hiyo tofauti ya ziada kwa hicho kipindi ndio hasara tunazopata lakini mzee wa black star kwakua zinatoka kwa wananchi dhaifu yeye kwake fresh tu tena anatufokea na kutufokea kifupi wanatuona mapimbi
 
Nchi zenye export kubwa ndio zinafaidika wanapofanya currency devaluation direct mana watu wataagiza zaidi sasa kwa nchi kama yetu ambayo tuna Balance of trade yenye deficit kubwa ukifanya devaluation utaua kabisa uchumi na kuibua inflation ya hatari kwa pesa kukosa thamani na domestic consumer kwasababu ya devaluation watapata shida kwenye kufanya importation bei zitakua juu sana huwezi jifananisha na China au Uturuki devaluation kwao inawasaidia kwakua niwazalishaji wa bidhaa nyingi zinazotumika duniani kote
 
wewe nani kasema au ebu tuambie ni sheria ipi kifungu gani cha BoT kinaongelea devaluation? Au ndo uchawa Promax
 
Hujui kitu kabisa!

Uturuki, kutokana na sarafu yao kudidimia mfululizo, mambo yamekuwa magumu kiasi cha wasomi wengi kukimbilia Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya, tena kwenda kufanya kazi za hadhi ya chini na ambazo zina malipo madogo huko Ulaya, lakini inaonekana ni afadhali ulipwe kidogo katika Euro kuliko Lira nyingi ya Uturuki isiyo na thamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…