Thamani ya shilingi yetu kulinganisha na Dolla katika kipindi cha wiki 2, nimegundua inaporomoka thamani sana

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Habari ndugu wa JF
Nimefuatilia thamani ya shilingi yetu kulinganisha na Dolla katika kipindi cha wiki mbili na nimegundua kwamba inaporomoka thamani kwa kasi sana.

Kwa mfano leo ubadishwaji wa shilingi yetu kwa wastani ni 1Usd= 2290 Tanzania shilings hali ambayo ni hatari kwa wale wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi mfano Petrol na bidhaa zake, vipuli mbalimbali, magari nk.

Naziomba mamlaka husika kufanya aina yeyote ya Intervention kuiokoa shilingi yetu. Kama shilingi yetu itaendelea kuporomoka kwa kasi hii basi tutarie bei za mafuta ya magari na mashine kuendelea kupaa na hivyo kuathiri bei za bidhaa na kuongeza nauli za mabasi.

Nawasihi mamlaka zote husika kuanzia BOT kufanya kitu haraka iwezekanavyo.

Ahsante
Mzalendo Mkweli

Update 25/04/2018

1 US Dollar equals
2,284.00 Tanzanian Shilling

Update 27/04/2018
1 US Dollar equals
2,296.75 Tanzanian Shilling

Update 30/04/2018
1 US Dollar equals
2,280.15 Tanzanian Shilling

Update 02/05/2018
1 US Dollar equals
2,283.10 Tanzanian Shilling

Leo dolla imepanda dhidi ya shillingi hali ni tete ndugu zangu
 
kweli kabisa bwana Mzalendo, hii issue naona inapoenda ni hatari. Fikiria kwa ambao wanfanya local supply kwa TZS wakati manunuzi ni kwa USD.
 
Kuporomoka kwa shilingi vs dollar umekua unafwatilia kwa chanzo/ source gani?
 
Kama BOT ndio wanamchango mkubwa kwenye kudhibi haya mambo na huyu Gavana mpya tuhesabu maumivu.
 
Sasa iyo ndogo kama unakumbuka ilikuaga 1usd= 2500tsh....c ushukuru tunapanda ...tutafika tu 1usd=1000tsh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…