Thamani ya Uwekezaji Tanzania Yafikia Dolla za Kimarekani Bilioni 1.6

Thamani ya Uwekezaji Tanzania Yafikia Dolla za Kimarekani Bilioni 1.6

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Thamani ya uwekezaji nchini Tanzania imeongezeka kwa asilimia 60 hadi kufikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.6.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema thamani ya miradi ya uwekezaji imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 hadi kufikia dola bilioni 1.61 katika robo iliyoishia Juni 2024.

Kwenye ripoti iliyotolewa hivi karibuni.

TIC imesema ongezeko la mtaji linaonyesha nia inayoongezeka ya kuwekeza nchini Tanzania, kutokana na miradi 198 iliyoandikishwa katika kipindi hicho, tofauti na miradi 129 yenye thamani ya dola bilioni 1, ya robo iliyopita.

Soma Pia: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinara Tuzo ya Taasisi Bora ya Uwekezaji Afrika

Mkurugenzi mtendaji wa TIC Bw Gilead Teri amesema uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) umechangia sehemu kubwa ukiwa na ongezeko la asilimia 136.35 au dola za kimarekani milioni 938.32.

ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 681.48 milioni katika robo kama hiyo kwa mwaka jana.

Chanzo.CRI Swahili
 
Thamani ya uwekezaji nchini Tanzania imeongezeka kwa asilimia 60 hadi kufikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.6...
It fucking mean nothing, because it doesn't trickel down to common mwananchi pockets, it just on the papers only,
Ni matakwimu ya kujifurahisha na kuombea kura.
 
Thamani ya uwekezaji nchini Tanzania imeongezeka kwa asilimia 60 hadi kufikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.6...
Mmh nchi yetu bado isee tunatakiwa kupambana sana kafulila apige sana kelele kwenye ppp angalau tukifika bil 5 usd kwa mwaka hapo tunaweza sasa kuvimba hapa africa.
 
Back
Top Bottom