WLF Tanzania
Member
- Oct 9, 2014
- 38
- 22
Utangulizi :
View attachment 217232
Kumkaribisha mtoto mchanga duniani huwajambo la furaha kwa familia. Lakini nchini Tanzania akina mama wengi wanaendelea kupoteza maisha yao wakati wa kujifungua. Vilevile watoto wengi wachanga hupoteza maisha yao katika wiki zao za mwanzo wawapo duniani.
Kampeni ya "Thamini Uhai"inayozinduliwa Kigoma siku ya Ijumaa tarehe 10 Oktoba 2014, imelenga kuwatia moyo akina mama watarajiwa na familia zao kuweka mipango salama kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa, ambapo akina mama wanaweza kujifungua katika kituo cha afya chini ya uangalizi wa kitaalam na kulindwa dhidi ya dharura zinazotishia uhai. Mkoani Kigoma karibia wakina mama wote wanahudhuria kliniki angalau mara moja wakati wa ujauzito wao. Lakini ni theluthi moja tu ya wakina mama wanajifungua kwenye kituocha afya.
Na kwa kuwa dharura nyingi wakati wa uzazi hazitabiriki, hivyo kujifungua kwenye kituo cha afya chenye wahudumu wenye ujuzi ni njia nzuri ya kuokoa maisha ya mama na mtoto. Kampeni ya "Thamini Uhai" ni ushirikiano kati ya Uongoziwa mkoa wa Kigoma, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na World LungFoundation.
View attachment 217233
Kwa pamoja wameandaa matangazo yaradio yanayoigiza hatari za kujifungua nyumbani, umuhimu wa kupangakujifungua katika kituo cha afya na umuhimu wa kujua mapema daliliza hatari za ujauzito.
Mkoani Kigoma, wakala wa afya ya jamiiwataongea na akina mama na akina baba Wafadhili wa KampeniKampeniimewezeshwa kwa ufadhili kutoka Mfuko wa Swedish InternationalDevelopment Cooperation Agency (SIDA), ukilenga kusaidia mradi waafya ya uzazi wa WLF Tanzania na wafadhili wengine wa mradi niBloomberg Philanthropies na H&B Agerup Foundation.
View attachment 217235
Kuhusu umuhimu wa kujifungua katika vituo vya afya na kuhusiana na njia za kukabiliana na vikwazo vyakujifungua kwenye vituo vya afya. Pia kutakuwa na picha za ukutani,machapisho na njia nyingine ambazo zitasaidia kusambaza ujumbe.
"Kuchelewa kutoa maamuzi sahihi nyumbani, kuchelewa kufika kwenye vituo vya afya na kuchelewa kupata huduma katika kituo cha
afya husababisha akina mama wengi kupoteza maisha yao. Kuongeza tahadhari na kuboresha uwezekano wa kupata huduma za afya za kisasa kwa kiasi kikubwa kitaokoa maisha ya wengi. Hili ndilo lengo la serikali yetu".
Uzinduzi wa "Deliver Now for Women and Children in Tanzania"
22 Aprili 2008
HiSTORIA YA VIFO VYA UZAZI
Tangu 2008, wakati serikali yaTanzania ilipozindua Mpango Mkakati wa Kitaifa wa mwaka 2008 –2015(2008-2015 National Road Map Strategic Plan) kupunguza vifo vyawajawazito na watoto, Tanzania ilionyesha maendeleo duni katikakupunguza vifo vinavyozuilika vya akina mama na watoto. Kilamwaka:
• Takriban akina mama 7,900 wakitanzania hupotezamaisha yao kutokana na matatizo ya uzazi na kujifugua
• Takriban watoto 40,000 wakitanzania hupoteza maisha yao ndani ya siku 28 baada ya kuzaliwa.
• Watoto wa kitanzania takriban100,000 hupoteza maisha yao kabla ya kufikisha miaka mitano.
• Kati ya takriban watoto 50,000 wanaozaliwa mfu, karibia nusu yao hupoteza maisha yao wakati wa kuzaliwa.
View attachment 217238
Huduma ya kitaaluma ya uzazi –Tanzania
View attachment 217225
Utafiti wa Takwimu za Afya Tanzania (Demographic and Health Surveys) www.dhsprogram.org
Mradi wa Afya ya Uzazi wa WLF –Kampeni ya "Thamini Uhai"
Kampeni ya "Thamini Uhai" imebuniwa kuainisha changamoto za kijamii, kitamaduni na kimtazamo ambazo zinapelekea matumizi duni ya vituo vya afya na wadau.
Hii inajumuisha fikra potofu kuhusianana usalama wa kujifungulia nyumbani, ukosefu wa mipango kwa mfanokujua umbali mrefu na suala la usafiri ambalo akina mama wengi wanakabiliana nalo katika kufikia vituo vya afya. Na wakati mwingine, changamoto hizi nipamoja na uwezo mdogo na huduma duni katika vituo vya afya.
Kampeni imedhamiria kupunguzavifo vinavyosababishwa na uzazi wakati wa kujifungua.
KUHUSU WLF:
View attachment 217239
WLF wamesaidia kuboresha na kujengataasisi za afya 15 katika mikoa ya Kigoma, Morogoro na Pwani; naimetoa mafunzo ya huduma mtambuka ya dharura ya uzazi na watoto wachanga (Comprehensive Emergency Obstetric and Newborn Care(CEmONC)) kwa zaidi ya wafanyakazi 100 wa afya (Non-Physician Clinicians) ambao ni madaktari wasaidizi, wakunga na maafisa afya nchini.
Inafanya kazi katika wilaya tano zaKigoma, na imesaidia kuboresha taasisi tisa za afya, ikiwa ni pamoja na kuvipa uwezo vituo sita (6) vya Afya kuwa na huduma mtambuka wa dharura ya uzazi.
Taasisi hizi ni pamoja na vituo vyaafya vya Ujiji, Nguruka, Kakonko, Mabamba, Nyenge, Buhingu nahospitali tatu za Maweni, Kibondo na Kasulu.
World Lung Foundation inaboresha afya kimataifa kwa kuboresha uwezo katika jamii husika. Maeneoyanayotiliwa mkazo na Shirika hili ni kupunguza matumizi ya tumbaku, kuzuia vifo vya akina mama na watoto, kifua kikuu, Ukimwi/VVU, pumuna afya ya mapafu ya mtoto.
Kwa maelezo
zaidi tembelea worldlungfoundation.org
View attachment 217232
Kumkaribisha mtoto mchanga duniani huwajambo la furaha kwa familia. Lakini nchini Tanzania akina mama wengi wanaendelea kupoteza maisha yao wakati wa kujifungua. Vilevile watoto wengi wachanga hupoteza maisha yao katika wiki zao za mwanzo wawapo duniani.
Kampeni ya "Thamini Uhai"inayozinduliwa Kigoma siku ya Ijumaa tarehe 10 Oktoba 2014, imelenga kuwatia moyo akina mama watarajiwa na familia zao kuweka mipango salama kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa, ambapo akina mama wanaweza kujifungua katika kituo cha afya chini ya uangalizi wa kitaalam na kulindwa dhidi ya dharura zinazotishia uhai. Mkoani Kigoma karibia wakina mama wote wanahudhuria kliniki angalau mara moja wakati wa ujauzito wao. Lakini ni theluthi moja tu ya wakina mama wanajifungua kwenye kituocha afya.
Na kwa kuwa dharura nyingi wakati wa uzazi hazitabiriki, hivyo kujifungua kwenye kituo cha afya chenye wahudumu wenye ujuzi ni njia nzuri ya kuokoa maisha ya mama na mtoto. Kampeni ya "Thamini Uhai" ni ushirikiano kati ya Uongoziwa mkoa wa Kigoma, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na World LungFoundation.
View attachment 217233
Kwa pamoja wameandaa matangazo yaradio yanayoigiza hatari za kujifungua nyumbani, umuhimu wa kupangakujifungua katika kituo cha afya na umuhimu wa kujua mapema daliliza hatari za ujauzito.
Mkoani Kigoma, wakala wa afya ya jamiiwataongea na akina mama na akina baba Wafadhili wa KampeniKampeniimewezeshwa kwa ufadhili kutoka Mfuko wa Swedish InternationalDevelopment Cooperation Agency (SIDA), ukilenga kusaidia mradi waafya ya uzazi wa WLF Tanzania na wafadhili wengine wa mradi niBloomberg Philanthropies na H&B Agerup Foundation.
View attachment 217235
Kuhusu umuhimu wa kujifungua katika vituo vya afya na kuhusiana na njia za kukabiliana na vikwazo vyakujifungua kwenye vituo vya afya. Pia kutakuwa na picha za ukutani,machapisho na njia nyingine ambazo zitasaidia kusambaza ujumbe.
Asemavyo Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete
View attachment 217236"Kuboresha afya ya akina mama na watoto ni changamoto ambayo inaisibu sana moyo wangu. Nina furaha kubwa kupata fursa ya kusaidia katika kuokoa maisha na kuboresha hali na maisha ya watoto wengi wasio na hatia na akina mama..."
"Kuchelewa kutoa maamuzi sahihi nyumbani, kuchelewa kufika kwenye vituo vya afya na kuchelewa kupata huduma katika kituo cha
afya husababisha akina mama wengi kupoteza maisha yao. Kuongeza tahadhari na kuboresha uwezekano wa kupata huduma za afya za kisasa kwa kiasi kikubwa kitaokoa maisha ya wengi. Hili ndilo lengo la serikali yetu".
Uzinduzi wa "Deliver Now for Women and Children in Tanzania"
22 Aprili 2008
Sababu za vifo vya wajawazito
View attachment 217237