Thank you inayoendelea Simba, Yanga na Azam sio ya kiufundi

Thank you inayoendelea Simba, Yanga na Azam sio ya kiufundi

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
It is undisputed facts kwamba Kipa namba 1 wa Timu ya Taifa kwa sasa ni Benno Kakolanya, no doubt.

Lakini katika namna ambayo wengi tulishagundua kitambo tangu alipoanza kukalia benchi vs na Yanga, kipa Beno Kakolanya amepewa mkono wa kwa heri, Bernard Morrison amepewa mkono wa kwa heri.Azam nao wamewapa Thank you akina Kenneth Muguna, Bruce Kangwa na wengineo akiwemo kocha bishoo Kalimangonga Ongalla.

Nikianza na Simba, Tanzania hii ukimuondoa Aishi Manula, hakuna kipa anayefikia uwezo wa Benno, huyo Ally Salim aliyebakia tusubiri kugawana mbao maana huko mbeleni michuano ni mingi sana na sio ya kitoto.Aishi Manula hata akipona hawez tena kuwa kwenye ubora wake, kiufup shughuli yake imeisha.

Sasa sielewi na siwez kuamini kama kweli Robertinho anaweza kupendekeza Benno aachwe.Sio kweli.

Haya viongozi wa Simba mmeshika mpini wenzetu.
 
Simba Ina viongozi wapumbavu wasiojua mpira, ukiwa na kipa kama Benno huitaji kwenda nje kutafuta kipa, wanafanya usajili wa mihemko.

Usajili wa Banda, Sackho, Kanoute na Inonga ulikuwa maalumu kwa kutengeneza timu itakayokaa muda mrefu na baadae kuchukua ubingwa wa Africa lakini kinachoendelea ni kama hawajui Nini wanafanya.
 
Simba Ina viongozi wapumbavu wasiojua mpira, ukiwa na kipa kama Benno huitaji kwenda nje kutafuta kipa, wanafanya usajili wa mihemko.
Usajili wa Banda, Sackho, Kanoute na Inonga ulikuwa maalumu kwa kutengeneza timu itakayokaa muda mrefu na baadae kuchukua ubingwa wa Africa lakini kinachoendelea ni kama hawajui Nini wanafanya.
Kwa hiyo wewe mwelevu unajua Mpira,
 
Mabadiliko makubwa ya wachezaji ni muhimu na hili linaweza kufanyika kwa bachi za awamu tatu kwa misimu miwili ili kuifumua timu upya.

Bachi ya kwanza:
Bocco
Onyango
Sawadogo (mchezaji mzuri ila hatakuja kuwa fit)
Outtara (siasa zinamnyima namba)
Kakolanya (kaondoka mwenyewe)
Nyoni
Mkude
Saidoo
Kyombo

Bachi ya pili:
Zimbwe (wakati wa damu mpya). Sijamsoma vizuri ila nadhani Yahya Mbegu anaweza chukua nafasi yake.

Bachi ya tatu:
Chama (zama zake zinafikia ukingoni)
Manula (au abaki kuwa kipa #2)
Gadiel

Pia Kapombe ahamishiwe kiungo ndiyo ibaki nafasi yake ya kudumu na achukue nafasi ya Nyoni/Bocco kama senior player akirotate na kina Mzamiru/Kanoute. Mwenda aingizwe kwenye kikosi cha kwanza kama FB.

Atafutwe kipa mrefu ambaye baada ya mwaka mmoja kutoka sasa achukue nafasi ya Manula.

Baada ya miaka 2, Simba itakuwa mpya kabisa yenye damu changa lakini haitatetereka kwa mabadiliko haya.

Haya maneno niliyasema miezi miwili iliyopita. Naona wanapita mulemule.
 
Back
Top Bottom