“Thank You” itamfuata muda si mrefu Kocha wa Simba

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Huyu Kocha wa Simba kwa kitendo cha kuchelewa kufanya maamuzi katika SUB haina afya kwake na hii inakwenda kumpa kadi nyekundu ya "THANK YOU"

Lakini pia kitendo cha kufanya majaribio ya nafasi za wachezaji kwa timu kama Simba ambayo ina njaa ya mafanikio kimataifa na Makombe ya ligi za ndani iliyoyapotezea kwa Mtani haina afya na hiyo inakwenda kumpa kadi nyekundu ya "THANK YOU"

Mfano mzuri ni ule wa BALEKE kwenye mchezo wa jana wa kirafiki dhidi ya POWER DYNAMO katika Tamasha kubwa la SIMBA DAY

#solomatv_updates
 
Pamoja na wanaomtetea kocha ila ameshindwa kuuma na kupuliza.

Angekuwa anawapa nafasi japo kidogo wachezaji vipenzi vya mashabiki.
Ni ukweli usiopingika yeye anaweza asifike December kama hatakuwa na mwendelezo mzuri wa ushindi
 
Sub ni response ya kinachotokea Uwanjani.
Either tactical au Health.
Unaposema alichelewa kufanya Sub unamaanisha nini?
Upi ulikuwa mda sahihi? Kuna tukio gani lilihitaji response ya haraka mpaka useme kocha amechelewa?
Ujinga wenu wabongo unasikitisha, mna ujuaji wa kishamba sana.
Mpaka kuna mda naona aibu kuwa Mtanzania.
 
Nadhani benchi Zima la Kolowizard halifai, hata usajili ni tia maji tia maji Makolo bora watafute kocha mwingine haraka hata Mgunder atawafaa bado mapema!

Kwa ubovu wa kocha Robert na usajili wa ndondo wa Simba huku mbavu zote mbili zikimilikiwa na wazee , ukweli bila kupepesa naiona Azam ikibeba point zote sita kwa Simba, naiona Yanga ikibeba points zote sita kwa Simba, naiona Singapore Fountain Gate ikibeba points zote sita, hapa tayari Simba ishakandwa mara sita na kudondosha points 18 kabla ya ligi kuanza!

Ngao ya jamii itaonesha wazi panapovuja kolokoloni!

Kama kawaida nimekaa zangu paleeeee Buza kwa Mpalanger nawa zoom Makolo tu!! Matusi yaishe kabla ligi kuanza maana ndilo kombe jipya walilonalo Makolo, makombe mengine ni kufa kiume na kujaza uwanja huku Yanga iliyoingiza mashabiki wachache ikiwazidi mapato, taarifa imevuja, aibu iliyoje! Kibegi kinaunajisi mlima wa Mungu, Makolo wameambiwa na Mazeri wakishushe waache sifa za kijinga!
 
Anaonekana kua muoga wa kufungwa anaona kama akifanya sub atakua anavuruga match na mchezo ni kitambulisha wachezaj wanashindwa hata na singida wakichange kikos chote
 
Kinachombeba sana Robertinho ni.

1. Kuifunga yanga msimu uliopita 2-0
Historia yake ya kuifunga yanga akiwa
Uganda (vipers) ( na Rwanda (APR).

2. Simba Kutaka KUIGA NABI alivyokaa yanga na kuwa na mipango ya muda mrefu na Robertinho.

3. Kuonekana ana mbinu nzuri za timu yake hususa ni kwenye mashindano ya kimataifa.
Simba WANAAMINI kama si makosa ya Onyango na Ally SALUM wangefika Nusu Fainali au Fainali.

4. Kutofungwa kwenye Mchezo wowowte WA League MSIMU uliopita .

ROBERTINHO YUPO SANA SIMBA.
LABDA AZINGUE KWENYE NGAO
 
Unaharibu sana jina la kampuni yako kwa kuandika habari za kizushi kuihusu Simba...kumbuka huku unakopost siyo Facebook
 
Hiyo aibu unalazimishwa kuiona, watu kama nyie hamfai kuwa watanzania , haya nambie wapi huko ambako watu wake wote wako smart unakoona fahari tukuombee uraia ukwende zako.
 
Hiyo aibu unalazimishwa kuiona, watu kama nyie hamfai kuwa watanzania , haya nambie wapi huko ambako watu wake wote wako smart unakoona fahari tukuombee uraia ukwende zako.
Kama mtaendelea na Ujuaji wa Kishamba huu, hakika sifai kuwa Mtanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…